KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 9, 2011

Dewji amshukia Poulsen



MFADHILI mkuu wa zamani wa klabu ya Simba, Azim Dewji amesema Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Jan Poulsen hana uwezo wa kuipa mafanikio timu hiyo.
Akizungumza na Burudani mjini Dar es Salaam wiki hii, Dewji alisema tangu Poulsen alipoanza kuifundisha timu hiyo mapema mwaka huu, hajaweza kuwa na mfumo unaoeleweka.
Dewji, ambaye kwa sasa anamiliki timu ya Moro United, inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara, alisema inawezekana tatizo hilo linatokana na wachezaji kushindwa kumuelewa kocha huyo.
“Mimi hadi sasa nashindwa kuelewa Taifa Stars inatumia mfumo gani. Lakini nilichokigundua ni kwamba, Poulsen ameshindwa kuipa mafanikio timu yetu ya taifa,”alisema mfadhili huyo.
Alisema kufungwa kwa Taifa Stars katika mechi nyingi ilizocheza ikiwa chini ya kocha huyo kutoka Denmark, kumedhihirisha wazi kuwa, uwezo wake wa kufundisha soka ni wa kiwango cha chini.
Alitoa mfano wa vipigo ilivyovipata timu hiyo katika mechi tatu mfululizo dhidi ya Msumbiji, Afrika Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kauli hiyo ya Dewji imekuja siku chache baada ya Taifa Stars kujiweka kwenye mazingira magumu ya kufuzu kwa fainali za Afrika za 2012, kufuatia kuchapwa mabao 2-1 na Jamhuri ya Afrika ya Kati mwishoni mwa wiki iliyopita.
"Kwa kweli mimi nashindwa kuelewa Poulsen anafanya kazi gani katika kikosi cha Taifa Stars kwa sababu tangu alipoanza kuifundisha, imekuwa ikifanya vibaya, tofauti na miaka ya nyuma,"alisema.
Dewji ameishauri Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kufuatilia mwenendo wa timu hiyo na ikiwezekana kuchukua hatua za kuinusuru badala ya kuiacha iendelee kuvurunda. “Haiwezekani timu iendelee kuvurunda, lazima kuna tatizo ndani ya kikosi cha Taifa Stars au benchi la ufundi, hivyo hatua zichukuliwe kuinusuru.

No comments:

Post a Comment