KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 29, 2013

HAYA NDO MAMBO YA EXTRA BONGO NDANI YA MAEDA


Mkurugenzi wa Extra bongo Ally Choki akiimba mbele ya mashabiki wake (hawapo pichani) ndani ya ukumbi wa Meeda, Sinza, Dar es Salaam jana usiku wakati bendi yake ilipokuwa ikiburudisha pande hizo
Kushoto ni mwimbaji mahiri wa bendi ya Extra Bongo, Athanas akiwa na mwimbaji pekee wa kike wa bendi hiyo, Khadija Mnoga a.k.a 'Kimobitel', ambaye anatamba kwa sasa na wimbo wake wa 'Mgeni' wakishoo luv mbele ya kamera yetu ndani ya ukumbi wa Meeda ,Sinza, Dar es Salaam jana usiku.
Kushoto ni mmoja wa marapa bora wa muziki wa dansi nchini, Totoo Ze Bingwa akirap ndani ya Meeda Sinza, Dar es Salaam wakati bendi anayopigia mzigo, Extra Bongo ilipokuwa ikitumbuiza pande hizo. Kulia ni Banza Stone a.k.a Generale akimpa big up.
Maua ya Extra Bongo mzigoni
Wakata nyonga maarufu kwa sasa wa Extra Bongo wakiongozwa na Super Nyamwela wakiwapagawisha mashabiki waliohudhuria shoo hiyo ndani ya Meeda  jana usiku
Waimbji bora wa Extra bongo kulia ni Rogert Hega a.k.a Katapila wakiimba ndani ya Meeda Sinza jana usiku
Rapa bora wa Extra bongo Kabatano (Kulia) akigani moja ya jimbo zao bora huku akipewa sapoti na nguli wa muziki wa dansi Banza Stone mwana masanja wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitumbuiza maeneo ya Sinza katika ukumbi wa Meeda jana usiku.

No comments:

Post a Comment