MABINGWA watetezi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga leo wamepata ushindi wao wa kwanza katika ligi hiyo baada ya kuifunga African Lyon mabao 2 – 1 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Davis Mwape dakika ya 35 ya kipindi cha kwanza na Rashid Gumbo dakika ya 66 ya kipindi cha pili.
Bao la kujifariji la Lyon lilifungwa na Shengo kwa mpira uliokufa (freekick) dakika ya 44 kipindi cha kwanza.
Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi sasa wamefikisha pointi sita katika michezo mitano waliyocheza hadi sasa.
Ushindi huo umeleta ahueni kubwa kwa Yanga kwani iwapo ingepoteza mechi hiyo ama kutoka sare, huenda mgogoro uliopo sasa kati ya uongozi na wachezaji ungeongezeka zaidi.
Katika mechi za awali, Yanga ilipoteza mechi moja na kuambilia sare katika mechi tatu, hali iliyosababisha baadhi ya wachezaji watuhumiwe kwamba walicheza chini ya kiwango kutokana na uongozi kushindwa kuwalipa fedha wanazodai.

No comments:
Post a Comment