KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, September 23, 2011

MBWA WA POLISI ALIYEINGIA UWANJANI



Huyu ndiye mbwa wa polisi aliyemponyoka polisi na kuingia uwanjani wakati za soka za Simba na Toto African zilipokuwa zikimenyana katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara Jumatano iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza. Timu hizo zilitoka sare ya mabao 3-3. Je, ni nani wa kulaumiwa?


Jeshi la Polisi mjini Mwanza limesema limeshamuhoji askari aliyekuwa na mbwa huyo na litamchukulia hatua kulingana na taratibu za kijeshi. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) nalo limeomba maelezo kutoka Polisi kuhusu tukio hilo. Tusubiri tuone.

No comments:

Post a Comment