KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, October 31, 2016

MREMBO WA TANZANIA 2016 AKANA KUWA NA SHAHADA YA CHUO KIKUU



Diana ameamua kuweka kila kitu wazi kwa kusema: ‘Jina langu ni Diana Loi Lukumay, mmasai na umri wangu ni miaka 18, nilizaliwa Arusha Mount Meru Hospital na ni mtoto wa tatu kwenye familia ya watoto wanne’

‘Nilisoma shule ya msingi ya serikali Levolosi 2005-2011, sekondari ya kutwa ya serikali Arusha 2012 -2015,  matokeo ya kidato cha nne nilipata darala la pili… nilichaguliwa kujiunga na kidato cha tano mchepuo wa Sanaa kwenda shule ya Wasichana Bwiru Mwanza‘

‘Kwakuwa nilikua tayari nipo kwenye tasnia ya urembo niliamua kutojiunga na masomo hayo kwakuwa yalishaingiliana na ratiba za mashindano haya katika ngazi ya kitongoji ambapo nilijiunga na kambi ya Miss Ubungo 2016/2017)‘ – Diana

‘Baada ya kuahirisha masomo ya kidato cha tano niliomba kujiunga na masomo ya ngazi ya cheti kozi ya maswala ya kodi katika chuo cha usimamizi wa fedha ambapo mpaka masomo yanaanza mwanzoni mwa October 2016 tayari nilikua kwenye kambi ya Miss Tanzania, mafanikio ambayo niliyapata baada ya kuibuka mshindi na kutangazwa kuwa lete Raha Miss Kinondoni 2016/2017′

‘Juhudi zangu hazikuishia hapo, nilipotangazwa mshindi sikubweteka na taji hilo bali niliendelea na kazi zangu za kijamii katika jamii yangu ya kimasai‘ – Diana

ALICHOSEMA FARAJA KOTTA KUHUSU MREMBO WA TANZANIA 2016



Niliposhinda Miss Tanzania, kuna mtangazaji fulani (tena wa kiume) wa kipindi cha redio cha asubuhi alitumia kama saa nzima hewani kusema ambavyo sikustahili kushinda. Asubuhi ya Jumatatu kama leo baada ya weekend ya shindano. Nilipigiwa simu kuamshwa. Nakumbuka niliamka nikawasha redio na nikasikiliza kipindi chote, peke yangu, chumbani. Nilitetemeka, nilishindwa kuoga, kula, nilijifungia ndani siku nzima nikilia. Niliwaza sana ambavyo pengine ni kweli sikustahili. Nilijuta kushiriki Miss Tanzania. I was young and naive. I had just turned 19, coming straight from the safety nets of Catholic nuns boarding schools. Sikujua kuna watu wanaweza kuwa na roho mbaya hata kwa watu wasiowajua. It took my parents (RIP) na kila busara waliyonayo kunifanya nijisikie vizuri. I had to dig deep inside me to regain my purpose. I was exposed to a cruel world and yes, I quickly learnt, it is what it is. Leo hii hakuna binadamu mwenye hiyo nguvu niliyompa yule mtangazaji. I learnt the hard way but I am grateful for the lesson. Thank God I learnt early. Kuna sehemu ya nguvu niliyo nayo leo iliyotokana na kujeruhiwa na binadamu na kupona. Lakini si kila mtu atapata bahati ya kupona, unaweza kumjeruhi mtu na akapotea moja kwa moja. Usijitafutie laana za reja reja. To the newly crowned Miss Tanzania, Do you honey! To the rest of us, tujenge zaidi ya kubomoa. Love doesn't cost a thing! God bless, Faraja 


BREAKING NEWSSSSS...BONDIA THOMAS MASHALI AFARIKI DUNIA KWA KUSHAMBULIWA NA WATU WASIOJULIKANA



Bondia mtanzania Thomas Mashali maarufu kama (Simba Asiyefugika),amekutwa amekufa huku akiwa na majeraha  usiku wa kuamkia leo huko maeneo ya Kimara jijini Dar es salaam kutokana na sababu ambazo hazijajulikana mpaka sasa.
Kwa mujibu wa katibu mkuu wa Oganization ya ngumi za kulipwa nchini PST Antony  Lutta,ameiambia blogu hii kwamba, taarifa walizozipata ingawa bado  hazijathibitishwa inaonyesha Thomas Mashali ameuwawa.
Lutta ameongeza kwamba marehemu enzi za uhai wake amekuwa na tabia ya kufanya vurugu akiwa amelewa sasa hatujui nini kimempata ambapo  mwili wake umekutwa maeneo ya Kimara jijini Dare s salaam ukiwa na majeraha baada ya hapo  ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa katika  hospitali ya taifa muhimbili.
Marehemu Mashali kabla ya kifo chake alikuwa  acheze na bondia Chimwemwe kutoka nchini Malawi ,pigano ambalo lilipangwa kufanyika mkoani  morogoro siku ambayo bondia mwenzake Dullah Mbabe alipangwa kucheza pigano la utangulizi.
Mashali ambaye  jina lake la  kuzaliwa ni Christopher Fabian Mashali,aliyezaliwa Septemba 09 mwaka 1989,ameacha rekodi ya kushinda mapambano 19 kati ya hayo 9 akishinda kwa KO,amepoteza mapambano 5 kati ya hayo amepigwa kwa KO mapambano 4 huku akitoka sare pigano moja tu.
Marehemu ameacha mke na watoto

YANGA YAIFUMUA MBAO FC MABAO 3-0



YANGA leo imemrejesha Kocha wake, Hans van der Pluijm kwa furaha baada ya kuitandika Mbao FC mabao 3-0 katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kutokana na ushindi huo, Yanga sasa imefikisha pointi 27 baada ya kucheza mechi 12, ikiwa kwenye nafasi ya pili nyuma ya Simba, inayoongoza kwa kuwa na pointi 32.

Mabao yaliyoiwezesha Yanga kutoka uwanjani na pointi zote tatu yalifungwa na beki Vicent Bossou, Mbuyu Twite na Amisi Tambwe.

Licha ya Yanga kuibuka na ushindi huo mnono wa mabao, timu hizo zilimaliza kipindi cha kwanza zikiwa suluhu, huku kila moja ikiwa imeonyesha uwezo mkubwa.

Sunday, October 30, 2016

DIANA EDWARD NDIYE MISS TANZANIA 2016






SIMBA YAZIDI KUNG'ARA


SIMBA jana ilizidi kupaa kileleni mwa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuicharaza Mwadui mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali, Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-0.

Simba ilipata bao la kwanza kupitia kwa Mohamed Ibrahim kabla ya Shiza Kichuya kuongeza la pili. Bao la tatu lilifungwa tena na Ibrahim.



Saturday, October 29, 2016

BOCCO AITOA KIMASOMASO AZAM


AZAM jana iliendelea kujitutumua katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara, baada ya kuitandika Kagera Sugar mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Mshambuliaji na nahodha John Bocco ndiye aliyeiwezesha Azam kutoka uwanjani na pointi zote tatu baada ya kuifungia bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya pambano hilo kumalizika.

Ushindi huo ulikuwa wa pili mfululizo kwa Azam baada ya kupokea vipigo katika mechi zake zilizopita huku ikiwa imejikusanyia poiti 19 baada ya kucheza mechi 12.

Kagera ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 32 kupitia kwa Themi Felix kabla ya Mudathir Yahya kuisawazishia Azam dakika tano zilizofuata. Mabao hayo yalidumu hadi mapumziko.

Felix aliiongezea Kagera bao la pili kwa njia ya penalti baada ya beki Aggrey Morris wa Azam kumchezea rafu Ally Nassoro ndani ya eneo la hatari.

Frank Domayo aliisawazishia Azam dakika ya 80 kwa shuti kali baada ya kipa wa Kagera kutema shuti la Bocco.

SERIKALI YAMREJESHA PLUIJM YANGA



HATIMAYE klabu ya Yanga imeamua kubadili gea angani kwa kumuandikia barua Kocha wake, Hans van der Pluijm, kumtaka abadili uamuzi wake wa kujiuzulu kuifundisha timu hiyo.

Barua hiyo iliyotiwa saini na Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, imeeleza kuwa hawaoni sababu ya kuachana na Pluijm baada ya kuwa ameiletea mafanikio makubwa timu hiyo.
 
Kocha huyo kutoka Uholanzi, alijiuzulu mapema wiki hii baada ya kukerwa na uongozi wa Yanga, kumleta kocha mpya, George Lwandamina kutoka Zambia bila kumtaarifu, akisema huko ni kumvunjia heshima.

Aidha, Pluijm alikataa kutumikia wadhifa wa mkurugenzi wa ufundi, ambao Yanga ilimtunukia baada ya kumleta Lwandamina kuwa kocha mkuu.

Hatua hiyo ya Yanga kumrejesha Pluijm imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kuamua kuingilia kati sakata hilo.

Waziri huyo kijana, ambaye ni mwanachama wa Yanga, aliushauri uongozi wa Yanga kumrejesha Pluijm na baadaye kumshawishi kocha huyo abadili uamuzi wake.

LIGI YA WANAWAKE KUCHEZESHWA NA WAAMUZI WA KIKE



WAAMUZI wa kike ndiyo watakaopewa nafasi zaidi kuchezesha Ligi ya soka la Wanawake Tanzania, inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Novemba Mosi katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma huku viwanja vitatu vikitarajiwa kuwaka moto.
Hayo yamesemea na Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas alipokuwa anazungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Saaalam jana Dar es Salaam.
Ligi huyo inayotarajiwa kuanza Novemba 1, mwaka huu kuwa wanaamini katika uzinduzi huo utakuwa wa pekee kwa sababu utahudhuriwa na wabunge wa Bunge la Tanzania.
Ligi hiyo ambayo inatarajiwa kuwa na ushindani kutokana na kuwakikishwa na nyota mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara imegawanyika katika makundi A na Bekee kwa sababu utahudhuriwa na wabunge wa Bunge la Tanzania.
Alizitaja timu ambazo zitafungua ligi hiyo kuwa ni Baobao Queens ya Dodoma itawakaribisha Victoria ya Iringa mchezo ambao utacgezwa uwanja wa Jamhuri Dodoma, Marsh ya Mwanza itakuwa wageni wa Majengo ya Kigoma Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Mchezo mwingine utakuwa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ambapo wenyeji JKT Queens watakuwa wenyeji wa Mlandizi Queens.
Alisema kuwa benchi la ufundi la timu ya taifa ya wanawake, litagawanywa katika mikoa hiyo ili kuangalia wachezaji wenye uwezo ambao wataunda kwenye kikosi cha timu ya taifa.
"Timu ya taifa itatolewa na mashindano haya, hatutakuwa na wachezaji wale wale kila siku na pia ligi hii itatisaidia kupata kikosi cha vijana U-20," alisema.

SERIKALI YASHTUKIA MCHEZO MCHAFU SIMBA NA YANGA, YAWATAKA MANJI NA MOO KUANZISHA TIMU ZAO




SERIKALI imeshtukia mchezo mbaya uliotaka kufanyika katika klabu za Simba na Yanga, hivyo imezitaka ziache mara moja mipango ya kutaka kuleta mageuzi ya mfumo wa uendeshaji.

Agizo hilo la serikali limekuja huku mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Yanga, Yussuf Manji, akitangaza kuikodisha klabu hiyo kwa miaka 10 huku mwenzake, Mohammed Dewji wa Simba, maarufu kwa jina la Mo, akitangaza kununua hisa zaidi ya asilimia 50.

Katika agizo hilo lililotangazwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja, serikali imewataka Manji na Mo kuanzisha klabu zao kama alivyofanya mmiliki wa Azam, Said Salim Bakhressa badala ya kuzing'ang'ania Simba na Yanga.

Kiganja amezitaka klabu hizo kusitisha mara moja michakato yote inayoendelea ya kubadilisha umiliki wa timu kutoka kwa wanachama kwenda katika umiliki wa hisa na ukodishwaji hadi kutakapofanyika marekebisho ya katiba za Simba na Yanga.

Amesema klabu hizo zinapaswa kurekebisha katiba zao kwanza kabla ya kufanya mabadiliko hayo kwa mujibu wa Sheria ya Baraza hilo na Kanuni za Msajili namba 442 Kanuni 11 kifungu kidogo cha (1-9) .

Kiganja alisema kuwa mabadiliko hayo yanayoendelea kwenye klabu hizo tayari yameingia dosari baada ya baadhi ya wanachama kwenda mahakamani kupinga michakato hiyo kitu ambacho sio kizuri na pia sio ishara nzuri endapo yataachwa yaendelee.

"Tumesitisha michakato yote ya kubadili umiliki kutoka kwa wanachama kwenda kwa uwekezaji kwa timu za Simba na Yanga mpaka watakapofanya mabadiliko kwa mujibu wa katiba za klabu zao," alisema Kiganja.

 BMT imemtaka mdau au mwanachama yoyote anayetaka kufanya uwekezaji kwenye klabu hizo, ni vema angeanzisha timu yake kama  Bakhressa alivyoanzisha Azam FC ili kupunguza malalamiko kwa vile timu hizo zina wanachama wengi.
Kiganja alisema kuwa michakato hiyo ilitakiwa ianzie kwenye matawi nchi nzima ili maamuzi yawe ya wote kwani mabadiliko yoyote ndani ya klabu hizo lazima yafuate katiba zao.

YANGA YAIGAGADUA JKT RUVU 4-0




YANGA jana iliendelea kung'ara katika michuano ya soka ya ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibugiza JKT Ruvu mabao 4-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Yanga ilijipatia mabao hayo manne kupitia kwa washambuliaji wake, Amis Tambwe, aliyefunga mawili, Obrey Chirwa na Simon Msuva.

Yanga ilicheza mechi hiyo ikiwa chini ya kocha wake msaidizi, Juma Mwambusi, baada ya Kocha Mkuu, Hans van der Pluijm kutangaza kujiuzulu.

Kutokana na ushindi huo, Yanga imeendelea kujichimbia nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa nyuma ya watani wao Simba kwa tofauti ya pointi moja.

Monday, October 24, 2016

ULIMWENGU ASEPA TP MAZEMBE, ATAKA KUTAFUTA TIMU ULAYA



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, ameripotiwa kuachana na klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.



Habari za uhakika kutoka DRC zimeeleza kuwa, mkataba wa Ulimwengu kuichezea TP Mazembe umeshamalizika na amekataa kuongeza mwingine.

Ulimwengu, ambaye ameitumikia TP Mazembe kwa miaka mitano, ameamua kufatilia ofa mbalimbali alizopata kutoka klabu za Ulaya.

Ulimwengu amekaririwa akiwaeleza viongozi wa TP Mazembe kuwa, kwa sasa anaelekeza akili yake katika kucheza soka ya kulipwa barani Ulaya.



HUYU NDIYE KOCHA MPYA YANGA ATAKAYEMRITHI PLUIJM



KOCHA mpya wa Yanga kutoka Zambia, George Lwandamina, amewasili nchini kwa ajili ya mazungumzo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji.

George aliwasili nchini jana usiku na iwapo mipango itakwenda vizuri, atarithi mikoba ya Kocha wa sasa, Hans van der Pluijm.
 
Habari zaidi zimeeleza kuwa, tayari kocha huyo ameshaingia mkataba wa miaka miwili wa kuinoa Yanga na taarifa rasmi zinatarajiwa kutolewa leo.


(Picha kwa hisani ya Mwananchi)

YALIYOJIRI KONGAMANO LA MABADILIKO YA UENDESHAJI WA KLABU ZA SOKA NCHINI


Kongamano la mabadiliko ya uendeshaji wa klabu za soka limefanyika Jumamosi Oktoba 22, 2016 kwenye ukumbi wa Uwanja Mkuu wa Taifa, Dar es Salaam.

Kongamano hilo lililoandaliwa na chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzani (TASWA) lilishirikisha wadau zaidi ya 60 nchini.

Kituo cha televisheni cha Azam kilionesha live (mubashara) kongamano hilo huku wajumbe wakikubaliana masuala kumi ya msingi.

Kwanza wajumbe walikubali kuwa kuna umuhimu wa kufanya mabadiliko sasa kwa sababu muundo unaotumika kuendesha klabu za soka una matatizo mengi.

Pili iliamuliwa klabu zijiandae vya kutosha kukaribisha mabadiliko hayo ikiwa ni pamoja na kuboresha utawala bora (governance) kwenye uendeshaji wa klabu.

Tatu mifumo yetu kama nchi inawezesha klabu kuwa na aina nyingi za mifumo ya kiuendeshaji hivyo wanachama waelimishwe kwa kina kuhusu mifumo hiyo ili wachague ulio bora zaidi kwa manufaa ya klabu zao.

Nne ili mabadiliko haya yafanyike kwa haki, inatakiwa wamiliki wa timu hizi (wanachama) waelimishwe  vya kutosha juu ya thamani yao ili wajitambue. Kwamba thamani ya klabu kubwa nchini haiwezi kulinganishwa na kiasi cha fedha kinachotolewa na wawekezaji hivyo wanachama wasiingie kwenye mabadiliko wakiwa wanyonge kwa sababu wao ndio wana mtaji mkubwa kuliko hela zinazoletwa kwa ajili ya uwekezaji.

Tano mabadiliko haya hayawezi kufanywa na wanachama na wawekezaji pekee bila kuishirikisha serikali. Hivyo klabu zinapojipanga kwa mabadiliko haya zihakikishe zinashirikisha serikali na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Sita mabadiliko haya yasifanywe kishabiki bali yafanywe kitaalamu ili  kutengeneza msingi Imara utakaoepusha migogoro hapo baadaye.

Saba kuelekea mabadiliko haya, hasa katika kipindi hiki ambacho uelewa wa wanachama ni mdogo, serikali inatakiwa kulinda maslahi ya walio wengi kwa kuingilia kati pale inapoona kuna mwelekeo wa kuwa na mabadiliko yanayominya maslahi ya walio wengi.

Nane mpira ni biashara ya kipekee ambayo mafanikio yake yanategemea jinsi washindani wanavyoshirikiana. Hivyo kuelekea mabadiliko haya wanatakiwa watumike wataalamu wa biashara ya mpira ili klabu zinapobadilika ziweke misingi itakayokubaliana na biashara ya soka.

Tisa  klabu zinao wajibu wa kulinda hadhi zake (brand) kwa sababu eneo hilo ndio msingi wa biashara ya mpira. Hivyo klabu zinapoelekea kwenye mabadiliko, lazima zizingatie hadhi zao zinalindwaje.

Kumi Chama cha Waandishi wa Habari na Michezo kiliombwa kufanya makongamao zaidi hasa kuhusiana na aina ya mabadiliko ambayo klabu zinaweza kuingia kwa sababu inaonekana wanachama ambao ndio wamiliki wa klabu hizi hawana uelewa wa kutosha hivyo inawapunguzia wigo wa kuchagua aina ya mabadiliko.

SHIJA RICHARD
KATIBU WA SEKRETARIETI

KONGAMANO LA MABADILIKO YA UENDESHAJI WA KLABU ZA SOKA

Oktoba 24, 2016.
…………………………………………..

TAARIFA KAMILI

UFUNGUZI

Kongamano lilifunguliwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohammed Kiganja kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Prof. Elisante  Ole Gabriel.

Kiganja aliwataka wajumbe kujadili hoja badala ya watu au timu. Alisisitiza wajumbe wajadili mifumo na aina ya mabadiliko ambayo klabu hizi zinaweza kuelekea.

Pia aliwataka TASWA kuhakikisha Waandishi wake wanaripoti taarifa zenye weledi na zenye manufaa kwa familia ya wana michezo.

Aliongeza TASWA iunde kamati ya maadili kwa ajili ya kuwawajibisha wanachama ambao wanaenda kinyume cha maadili.

WACHANGIAJI

PROFESA PROSPER NGOWI- Chuo Kikuu cha Mzumbe

Katika mada yake, Profesa anasema wanachama na wadau kwa ujumla hawatakiwi kuogopa kufanya mabadiliko au kubadilisha namna ya kuendesha vitu kwa sababu hilo ni jambo la kawaida.

Hata hivyo akadokeza kuwa wanachama wa Simba na Yanga hawapaswi kuwa wanyonge kuelekea kwenye mabadiliko hayo kwa sababu mtaji wao ni mkubwa kuliko pesa zinazoletwa na wafadhili.

“….(Wanachama) Mtaji wao mkubwa pengine sio pesa. Mtaji wao mkubwa ni majina yaani brand ya timu hizi. Mtaji mwingine ni historia ndefu ya timu hizi ya zaidi ya miaka 80 na ‘fan base’ kubwa sana. Pia vikombe ambazo timu hizi zimeshida ni mtaji mkubwa sana katka meza ya majadiliano. Hii ni mitaji ambayo thamani yake ni kubwa kuliko pesa. Kwa hiyo wenye timu hizi hawapaswi kuwa wanyonge kifedha mbele ya wawekezaji. Thamani ya mitaji hii hasa brand ni kubwa kuliko pesa.”

Aliendelea kueleza, “Lazima waelewe kama wanakodisha timu hizi, wanatoa na kupokea masharti gani? Hawapaswi kupokea tuu bali nao watoe masharti. Waamue wanawakilishwa vipi katika uendeshaji wa timu hizi katika nyanja zote? Brand ya timu hizi zinalindwa vipi? Ni muhimu pia kujua kuwa kama mwekezaji atataka muda mrefu wa mkataba, Lazima wenye timu wawe na muda na nafasi ya kufanya marekebisho ktk makubaliano baada ya muda fulani, mfano miaka miwili au mitatu badala ya kusubiri hadi mwisho wa mkataba, mfano miaka 10”, anasema Profesa Ngowi ambaye ni mtaalamu wa masuala ya uchumi na biashara.

Profesa Ngowi anasisitiza kuwa kwa mtazamo wa kiuchumi na kibiashara mabadiliko ni jambo la kawaida na halipaswi kuonekana la ajabu.

“Jambo hilo linapaswa kuwa la kawaida kwa yeyote anayependa. Hakuna sababu ya kuogopa kufanya mabadiliko au namna ya kufanya mambo” anasema Profesa Ngowi.

Anaendelea kueleza jambo la msingi katika mabadiliko hayo ni pande zinazohusika hasa wanachama ambao ni wamiliki wa klabu kujua ni kipi wanachokitaka.

“Inavyoonekana wanachotaka ni hali nzuri ya kiuchumi ya timu zao. Sio jambo baya. Wawekezaji nao wanataka maslahi ya kiuchumi nalo sio jambo baya hata kidogo,” anasema Profesa Ngowi.

PATRIC MUSUSA – MENEJA WA MASOKO NA MIRADI KUTOKA SOKO LA HISA DSM (DSE)

Mususa anasema  klabu zinapotaka kuelekea kwenye mabadiliko hasa kwa matarajio ya kuingia kwenye soko la hisa, kwanza zihakikishe zinabadilisha mifumo yao iliyopo sasa ili iendane na mahitaji ya soko la hisa.

Anasema lazima zisajiliwe kuwa kampuni na Wakala wa Usajili wa Makampuni (BRELA) na pia ziandae taarifa za fedha.

Lazima zitatakiwa kuwa na Bodi ya Wakurugenzi (BOD) watakaochaguliwa na wanahisa ambao ni wanachama  wamiliki wa klabu hizo.

Kila mwanahisa atastahili kupata gawio la faida pale kampuni (klabu) yao itakapotengeneza faida na atakuwa huru kuuza hisa yake kama anataka  kuachanana na umiliki katika klabu hiyo.

ANGETILE OSIAH, KATIBU MKUU WA ZAMANI WA TFF

Angetile anasema klabu zikihitaji kubadilisha mifumo yao zinatakiwa kuzingatia utawala bora kwa kutofautisha majukumu sekretarieti na taasisi nyingine zilizopo ndani ya klabu.

Anasema ulimwengu wa sasa mchezaji ni rasilimali(asset) inayothaminishwa kwa fedha kwenye vitabu vya hesabu hivyo klabu lazima iwe na wataalamu watakaoweza kukabiliana na changamoto hizo za utaalamu na nyinginezo.

Anasema klabu lazima ziwe na kurugenzi za uendeshaji, habari, biashara, sheria, fedha na masoko na ziajiri wataalamu kwa ajili ya kuendesha shughuli hizi. Kurugenzi hizo zinahitaji wataalamu kama waliopo kwenye taasisi nyingine za serikali na makampuni binafsi.

Anaongeza kuwa uendeshaji wa klabu lazima uzingatie utawala bora kwa kuzipa Uhuru na mipaka ya kazi taasisi au idara zote zilizopo ndani ya klabu.

Anawakumbusha wadau kurejea azimio la Bagamoyo ambapo Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lilileta utaratibu wa kutoa leseni kwa klabu zilizotimiza mashari.

Anasema masharti yanayotajwa yakiwemo kuwa na utawala bora, timu za vijana n.k kama yatazingatiwa, klabu nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuchagua mfumo wa kujiendesha kama ni wa wanachama au wanahisa.

CHARLES NDAKI, Mtaalam wa Masuala ya Masoko

Ndaki anasema jina la timu (brand) ni rasilimali muhimu inayitakiwa kutunzwa na kuendelezwa kwa sababu ndio msingi wa biashara iliyopo katika soka.

Anasema klabu zinatakiwa kuweka mikakati ya kujipa upekee ili kujitofautisha na wengine kwa lengo la kutumia vizuri jina lake kibiashara.

Anasema kwa kufanya hivyo klabu itakuwa na wigo mpana wa wanachama na mashabiki (fun base) NA hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kufanya biashara kupitia jina la klabu.

MICHAEL WAMBURA – KATIBU WA ZAMANI WA TFF

Wambura anasema serikali ndio inayoweza kulinda maslahi ya wengi katika mabadiliko haya hivyo watumie vyombo vyake kuhakikisha yanafanyika mabadiliko yenye maslahi kwa walio wengi.

Anasema ni vyema mabadiliko yakafanyika kwa kuzingatia Sheria za nchi, TFF, CAF na FIFA hivyo aliviomba vyombo vinavyohusika, TFF, BMT na Wizara kuhakikisha zinawezesha mabadiliko haya kwa manufaa ya klabu, wanachama, wawekezaji na sekta ya michezo kwa ujumla.

HENRY TANDAU
MKUFUNZI WA FIFA

Anasema wadau katika mabadiliko haya lazima wajifunze mifumo minne ya kuendesha soka kablaya kuelekea mabadiliko

Anaongeza tatizo kubwa la wadau wa michezo hawapendo kujifunza wanaendesha klabu kwa mazoea.

Anasema biashara ya mpira ni ya aina yake kwa sababu ili ufanikiwe inahitaji ushirikoane na mshindani wako. Kutokana na upekee huo, biashara hii inatakiwa kuendeshwa na wataalamu wenye weledi nayo.

Anasema Azimio la Bagamoyo ndio lilitakiwa kuwa msingi mkubwa wa mabadiliko kwa sababu limeanisha vitu vingi vizuri ambavyo havijafanyiwa kazi.

Anaongeza kuwa japo tumechelewa lakini tulipofika tungeanza na Azimio la Bagamoyo kuelekea kwenye mabadiliko ya kweli.

JAMAL RWAMBOW, MJUMBE WA BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA BMT

Anasema mabadiliko haya hawawezi kufanyika bila kuishirikisha serikali. “Itakuwa ni kujidanganya kuamini kwamba wawekezaji na wanachama wanaweza kufanya mabadiliko haya bila kuishirikosha serikali kwa sababu serikali ndio baba” anasema Rwambol.

Alitoa mwito kwa wadau kuishirikisha serikali na hasa kufuata maelekezo yaliyotolewa na BMT kuhusiana na utaratibu wa kufanya mabadiliko hayo kama klabu zi nataka kuelekea huko.

Mwishowe Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliahidi kwamba chama chake kitashirkiana wadau mbali mbali kuhakikisha makongamano kama hayo yanafanyika Mara kwa mara ili kutoa fursa kwa wadau ya kujifunza.

SIMBA YAIBUGIZA TOTO AFRICAN 3-0




SIMBA jana iliendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya soka ya ligi kuu ya Tanzania Bara, baada ya kuibugiza Toto African mabao 3-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Simba ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kutokana na ushindi huo, Simba sasa inazo pointi 29 baada ya kucheza mechi 11, ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 21 baada ya kucheza mechi 10.

Mshambuliaji Muzamil Yassin aliifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 42 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Frederick Blagnon.

Mrundi Laudit Mavugo aliiongezea Simba bao la pili dakika ya 51 baada ya kutengenezewa chumba safi na Muzamil.

Zikiwa zimesalia dakika 16 pambano hilo kumalizika, Muzamil aliiongezea Simba bao la tatu baada ya kumalizia kona iliyochongwa na Shiza Kichuya.

Sunday, October 23, 2016

MREMBO WA SINGIDA ASHINDA TAJI LA MISS TALENT 2016

MWENYEKITI wa Kamati ya Mashindano ya Miss Tanzania 2016, Hashim Lundenga (kulia) akimtangaza mshindi wa shindano la Miss Talent, lililofanyika juzi kwenye hoteli ya Jembe Beach, mjini Mwanza.
MSHINDI wa shindano la Miss Talent, Lisa Mdoro kutoka Singida, akipongezwa na washiriki wenzake baada ya kuibuka mshindi.

WASHIRIKI wa shindano la Miss Tanzania 2016, wakionyesha umahiri wao wa kucheza muziki wakati wa shindano la Miss Talent.
LISA Mdoro kutoka Singida, akionyesha manjonjo ya kucheza ngoma za asili na hatimaye kuibuka mshindi.
WASHIRIKI wa Miss Tanzania, wakicheza muziki wa kizazi kipya
WASHINDI watano wa mwanzo wa shindano la Miss Talent.

YANGA YATOA DOZI KALI KWA KAGERA SUGAR, YAIKUNG'UTA MABAO 6-2







YANGA sasa imeanza kuonyesha cheche zake katika michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuibugiza Kagera Sugar mabao 6-2 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Ushindi huo, ambao ni wa kwanza mkubwa kwa Yanga tangu ligi hiyo ilipoanza, umeiwezesha Yanga kuchupa hadi nafasi ya pili, ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza mechi 10, nyuma ya Simba inayoongoza kwa kuwa na pointi 26.

Katika mechi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali kipindi cha kwanza, hadi kilipomalizika Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 3-1.

Kagera Sugar ilikuwa ya kwanza kufunga bao dakika ya tatu lililopachikwa wavuni na Mbaraka Yussuf kabla ya Donald Ngoma kuisawazishia Yanga dakika ya nne.

Simon Msuva aliiongezea Yanga bao la pili dakika ya 21 kabla ya Obrey Chirwa kufunga la tatu dakika ya 26.

Kagera ilikianza kipindi cha pili kwa kasi na kuongeza bao la pili dakika ya 49 lililofungwa tena na Mbaraka kabla ya Yanga kuongeza mabao mengine matatu kupitia kwa Deus Kaseke, Chirwa na Ngoma.

Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa jana, Azam ilizinduka toka usingizini baada ya kuichaa JKTRuvu bao 1-0 kwenye Uwanja wa Chamazi Complex, Dar es Salaam.

Bao pekee na la ushindi la Azam lilifungwa na nahodha wake, John Bocco kwa njia ya penalti dakika ya 57.

MKUTANO MKUU WA DHARULA YANGA WAOTA MBAWA



MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Manji ametii agizo la Mahakama kwa kuufuta Mkutano Mkuu wa dharula wa klabu ya Yanga uliopangwa kufanyika kesho makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana ilitoa katazo la kufanyika Mkutano wa kesho kufutia kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama wa klabu hiyo.
Manji ametangaza kuufuta Mkutano huo mchana wa leo akizungumza na Waandishi wa Habari Jangwani.
Na amesema taratibu za kisheria zinafanyika juu ya kupambana na pingamizi hilo ili liondolewe na tarehe nyingine ya Mkutano itatajawa mara mpango huo utakapofanikiwa.
Kwa mujibu wa hati ya agizo halali la Mahakama, uongozi wa Yanga umezuiwa kufanya Mkutano huo baada ya kesi iliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi ya Mwenyekiti wa klabu, Yussuf Manji na Kampuni ya Yanga Yetu.
Ajenda kuu ya Mkutano huo ilikuwa ni kupitisha Baraza la Wadhamini la klabu hiyo pamoja na kuondoa Mjumbe mmoja na kuweka mpya.
Na hayo yanafuatia Baraza la Wadhamini kuikodisha timu kwa kampuni ya Yanga Yetu kwa miaka 10, baada ya wanachama kuafiki ombi la Mwenyekiti wao, Yussuf Manji katika Mkutano wa Agosti 6, mwaka huu.

MANJI: AHADI YA UWANJA KAUNDA IKO PALEPALE


MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Manji amesema kwamba bado ana matumaini ya kuijengea klabu Uwanja wa kisasa eneo la Jangwani, Dar ea Salaam.
Aidha, Manji amesema kwamba eneo la Geza Ulole, Kigamboni anataka kuijengea timu Uwanja wa mazoezi tu mdogo na kwamba Uwanja mkubwa na wa kisasa utakuwa Jangwani.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam kuhusu Mkutano Mkuu wa dharula Jumapili, Manji aligusia pia baadhi ya mambo mengine ya maendeleo ya klabu
Kule Geza Ulole tutajenga Uwanja wa mazoezi na gym. Lakini Uwanja mkubwa na wa kisasa tutajenga hapa hapa Jangwani. Kama klabu za Ulaya, Uwanja wa mazoezi unakuwa tofauti na Uwanja wa mechi,”alisema.
Yanga inatarajiwa kuwa na Mkutano wa dharula Jumapili wiki hii Uwanja wa Kaunda, uliopo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam na Manji amewataka wanachama kujitokeza kwa wingi kujadili mustakabali wa klabu yao.
Ajenda kuu ya Mkutano huo ni kupitisha Baraza la Wadhamini la klabu hiyo pamoja na kuondoa Mjumbe mmoja na kuweka mpya.
Na hayo yanafuatia Baraza la Wadhamini kuikodisha timu kwa kampuni ya Yanga Yetu kwa miaka 10, baada ya wanachama kuafiki ombi la Mwenyekiti wao, Yussuf Manji katika Mkutano wa Agosti 6, mwaka huu.
Pamoja na hayo, Manji amesema mzee Ibrahim Akilimali amepoteza haki ya uanachama wa klabu hiyo kwa kuwa hajalipia kadi yake kwa miezi sita iliyopita.
“Akilimali kama anataka kuja kwenye mkutano Jumapili kwanza aende kwenye tawi lake akaomba uanachama upya,” amesema Manji.
Mwenyekiti huyo amewakaribisha wale wote wanaopinga wazo lake la kuikodisha timu katika mkutano wa Jumapili, kwani kuishia kuzungumza kwenye vyombo vya Habari haitasaidia.

Thursday, October 20, 2016

KAMATI YARIDHISHWA NA MAANDALIZI YA MISS TANZANIA


Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano mfululizo.

Amesema washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini Marekani.

Viingilio katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja na Christian Bella ikiwa wataafiki makubaliano watadondosha burudani katika shindano hilo huku washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kujishindia gari.

Washiriki wa shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.

YANGA YAIBUGIZA TOTO AFRICAN MABAO 2-0, AZAM YALAZIMISHWA SARE NA MTIBWA SUGAR



MABINGWA watetezi Yanga jana waliwapa ahueni mashabiki  wao baada ya kuichapa Toto African mabao 2-0 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Kutokana na ushindi huo, Yanga sasa inazo pointi 18 baada ya kucheza mechi tisa huku ikiwa inaendelea kushika nafasi ya tatu, nyuma ya Simba na Stand United.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa na Simon Msuva, ndio walioiwezesha Yanga kutoka uwanjani na pointi zote tatu  baada ya kuifungia mabao hayo mawili.

Chirwa alifunga bao la kwanza dakika ya 29 alipounganisha wavuni kwa kichwa krosi kutoka kwa Simon Msuva. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Bao la pili lilifungwa na Msuva dakika ya 56 baada ya  Deus Kaseke kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Wakati huo huo, Jahazi la Azam jana liliendelea kudidimia baada ya kulazimishwa kutoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezwa usiku, Mtibwa ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya pili lililofungwa na Rashid Mandawa kabla ya Himid Mao kuisawazishia Azam dakika ya 11 kwa njia ya penalti.

Kwa matokeo hayo, Azam sasa inazo pointi 13 baada ya kucheza mechi 10 wakati Mtibwa imefikisha pointi 16 kutokana na kucheza mechi 11.

Katika mechi zingine za ligi hiyo zilizochezwa jana, Ruvu Shooting ilitoka sare ya bao 1-1 na Mwadui, Ndanda ilitoka sare ya bao 1-1 na Mbeya City, Prisons iliichapa Stand United mabao  2-1 wakati Majimaji iliona mwezi kwa kuifunga African Lyobn mabao 2-0.

TASWA YAANDAA KONGAMANO LA MABADILIKO YA UENDESHAJI SOKA


KONGAMANO kuhusu mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia litafanyika Jumamosi Oktoba 22 mwaka huu ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na litarushwa live (mubashara) na kituo cha televisheni cha Azam.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), likiwa na lengo la kupata maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo hiyo, ambapo Simba ipo mbioni kuingia mambo ya hisa, wakati Yanga utaratibu wa kukodishwa. 

Katika taarifa yake, Katibu wa TASWA, Amir Mhando amesema leo kwamba Kongamano halina nia ya kuzuia mabadiliko au kuharakisha mabadiliko katika klabu hizo, badala yake inataka litumike kutoa elimu ya kutosha kwa wadau wa mpira wa miguu kuhusu mifumo hiyo na aina nyingine ya mifumo ya uendeshaji wa klabu duniani, hivyo kusaidia kujibu maswali mbalimbali  ambayo pengine hayajibiwi ipasavyo.
Amesema baadhi ya mambo yatakayozungumziwa ni umuhimu wa mabadiliko katika klabu hizo, pia harakati za kuzibadili zilivyoanza miaka ya nyuma na matokeo yake na itazungumziwa pia mifumo ya uendeshaji ya klabu mbalimbali duniani.
"Lengo ni kujadili kitaalamu bila ushabiki wa namna yoyote kwani nia ni kujenga na kuimarisha soka na michezo kwa ujumla hapa nchini na ndiyo sababu tumealika wataalamu wa kada mbalimbali, viongozi wa zamani wa soka kwa tofauti na baadhi ya wadau wa soka," amesema.
Tunaomba mashabiki na wadau wengine mbao hawakualikwa watambue tunathamini mawazo yao, lakini nafasi ya wanaotakiwa kuhudhuria ni chache hivyo wafuatilie kupitia vyombo vya habari.


Wednesday, October 19, 2016

YANGA HAIWEZI KUKODISHWA KAMA SUFURIA-AKILIMALI










Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotoa msimamo wa kamati hiyo na baadhi ya wanachama wa Yanga  kuhusu ukodishwaji wa Nembo ya timu hiyo.


Katibu wa Kamati ya Muafaka ya Yanga Mzee Ibrahim Akilimali akionyesha baadhi ya vipengele vilivyokosewa katika kukodisha timu ya Yanga kwa  na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo wakati alipotoa msimamo wa kamati hiyo na baadhi ya wanachama wa Yanga  kuhusu ukodishwaji wa Nembo ya timu hiyo.

Kabla ya kufanyika mkutano Mkuu wa dharura wa klabu ya Yanga,siku ya Leo kamati ya Mwafaka wa wazee wa timu hiyo imezungumza na waandishi wa habari kuhusu maamuzi ya mwenyekiti Yusuf Manji kutaka kuitumia nembo ya Yanga kwa miaka 10 ili awe mmiliki halali.
Akizungumza katibu wa kamati hiyo Ibrahim Akilimali ,amesema kuwa kitu ambacho anataka kukifanya Manji kinapelekea kwenye vurugu kubwa kuzidi hata ile ambayo ilishawahi kutokea kipindi cha nyuma kwani atawagawa wanachama pamoja na mashabiki wanaotaka mfumo huo na wale wanaokataa mfumo huo pia.
“Sisi hatutaki kabisa kurudi kule ambapo tulipokuwepo katika migogoro ya miaka nane na mwaka 2002 ndipo tulipata mwafaka wa suluhisho na kukubaliana kuwa tutumie jina ambalo lilidhiwa na waasisi wetu na kuwa na Yanga sport club na Yanga Cooperation”alisema Akilimali
Aidha amesema kuwa Yanga kampuni ilikufa na tukaweka utaratibu wa kuwa na hisa ambazo ni 51 asilimia ni ya Yanga pamoja na asilimia 49 ni ya wanachama na tulizunguka mikoa mingi mno kwa ajili ya kuondoa migogoro,kesi na kuomba radhi wanachama wa klabu hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa tulukuwa na mwanasheria ambaye alikuwa mwenyekiti mpaka anamaliza muda wake aliiachia Yanga Mil 200 na hapo hapo tukampata tena mwanasheria mzuri bahati mbaya Nchunga alijiuzulu baada ya kukaa miaka miwili na hatimaye tukampta bwana Manji naye akaongoza miaka miwili kwa sababu ya mahaba yetu ikabidi tuikanyange katiba kwa kumuongezea muda tena na tulimchagua tena.
“Sasa tunashangaa haijapita hata miezi nane linakuja deni la billioni 11 na laki 6 kitu ambacho kimetushutusha mno wanayanga na pia limekuja swala la kuleta hoja kuwa akodishwe Yanga na nembo ya klabu kwa muda wa mika 10 ila sisi tunasema kuwa Yanga ni kubwa sana na haiwezi kukodishwa kama masufuri ya kwenda msibani na mimi na wazee wa kamati kwa pamoja tunasema hatukubaliani na jambo hilo kwa asilimia mia”alisema Akilimali
Kwa upande wa aliyekuwa mwenyekiti wa matawi ya jiji la Dar es salaam ya Yanga,Mohammed Msumi amesema kuwa kutokana na Manji kuwa na mahitaji makubwa na timu hiyo ni vyema akakaa pembeni au kuanzisha timu yake mwenyewe na kuiacha Yanga ili iweze kujiendesha kwa mfumo wa kisasa.
“Tujiulize maswali ivi ni kwanini anataka mchakato huu ufanyike haraka huku alishawahi kusema kuwa Yanga inajiendesha kwa hasara ni mtu gani huyu anakaa sehemu ya aina hiyo na kama hawezi kufuata utaratibu wa klabu na kushindwa kufuata katiba kama anauwezo aanzishe timu yake na kuacha kutumia pesa zake kwa mabavu iili aichukue Yanga”alisema Msumari
 

TFF YAMPIGA MARUFUKU KHALFAN NGASSA KUIFUNDISHA TOTO AFRICAN



Kocha Khalfan Ngassa amekuwa kwenye benchi la timu ya mpira wa miguu ya Toto Africans ya Mwanza akiwa kocha msaidizi kwa mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inayoendelea kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Khalfan Ngassa aliongoza timu kwenye mchezo Na. 62 dhidi ya Kagera Sugar Oktoba 7, 2016; mchezo Na. 67 dhidi ya Mbao FC uliofanyika Oktoba 12, 2016 na Mchezo Na. 79 dhidi ya Majimaji ya Songea uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 72 (3) (5) ya Ligi Kuu, Kocha Mkuu anatakiwa kuwa na Leseni ya chini kuanzia Daraja B ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) na Daraja C kwa Kocha Msaidizi pia kutoka CAF.

Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa Kocha Khalfan Ngassa  hana leseni yoyote kati ya hizo, hivyo hastahili kukaa kwenye benchi la timu ya Toto Africans kama kocha mkuu au kocha msaidizi.

Kitendo kinachofanywa na Toto Africans ni ukiukwaji wa kanuni na ni vema uongozi wa Toto ukamwondoa Khalfan Ngassa kwenye benchi ili kuepuka adhabu. Kipendele cha (7) cha kanuni hiyo ya 72, inaelekeza adhabu kuwa inaweza kutozwa si chini ya Sh 500,000 (shilingi laki tano).

Pia tunazikumbusha klabu zote kuwa kuanzia msimu ujao wa 2017/18 wa Ligi Kuu ya Vodacom, kocha anayestahili kukaa kwenye benchi ni yule mwenye leseni Daraja A kwa nafasi ya Kocha Mkuu na angalau Leseni Daraja B kwa kocha msaidizi.

YANGA, TOTO AFRICAN DIMBANI LEO MWANZA, SIMBA NA MBAO FC KESHO DAR



Michezo sita ya ligi kuu ya Tanzania Bara, inatarajiwa kufanyika leo Jumatano, Oktoba 19, mwaka huu, likiwemo pambano kati ya Yanga na Toto African.

Vodacom – Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza nchini kwa kutoa huduma za kisasa za mawasiliano ndiyo mdhamini mkuu ligi hiyo ikisaidiana kwa karibu sana Kampuni ya kisasa ya vyombo vya habari yenye kurusha vipindi vyake kwa weledi na ubora wa hali ya juu ya Azam Televisheni (Azam Tv) na DTB- Benki ya kuaminika nchini kwa usalama wa fedha zako.

Kampuni hizo zinazong’arisha VPL, kesho zitakuwa sambamba kwenye kuchagiza michezo ya Ruvu Shooting ya Pwani ambayo itaikaribisha Mwadui ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Mabatini uliuoko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo Na. 81 wa VPL utakaoanza saa 10.00 jioni.

Mchezo Na. 82 utakaozikutanisha Azam FC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Morogoro utafanyika saa 1.00 usiku (19h00). Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi – maskani ya Azam yalioko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati mchezo Na. 83 utazikutanisha timu za Ndanda FC na Mbeya City ya Mbeya kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mchezo Na. 85 utazikutanisha timu za Tanzania Prisons ya Mbeya na Stand United itakayokuwa mgeni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya huku mechi Na. 87 itazikutanisha Toto African ya Mwanza itakayocheza na Young Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati African Lyon itakuwa mwenyeji wa Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kwenye mchezo Na. 88.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho Alhamisi Oktoba 20, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambako vinara wa ligi hiyo kwenye msimamo hadi sasa, Simba itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza katika mchezo Na. 84.

LIGI DARAJA LA PILI KUANZA OKTOBA 29




Timu 24, zinatarajiwa kupambana katika michuano ya Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 kuanzia Oktoba 29, mwaka huu, imefahamika.

Timu hizo zimepangwa katika makundi manne yenye timu sita kwa kuangalia zaidi jiografia au kanda ambako timu imetoka – lengo likiwa kupunguza gharama kwa timu shiriki hasa ikizingatiwa kuwa michuano hiyo haijapata mdhamini hadi sasa.

Kundi A lina timu za Mashujaa ya Kigoma, Mirambo ya Tabora, Mji Mkuu ya Dodoma, Green Warriors ya Pwani, Bulyanhulu na Transit Camp za Shinyanga.

Mechi za kwanza zitakuwa ni kati ya Mashujaa dhidi ya Green kwenye Uwanja wa Tanganyika mjini Kigoma wakati Mirambo itaikaribisha Mji Mkuu kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi. Timu za Transit Camp na Bulyanhulu zitacheza Oktoba 30, mwaka huu.

Kundi B; African Wanderers ya Iringa itaikaribisha AFC ya Arusha kwenye Uwanja wa Kichangani mjini Iringa siku ya Oktoba 29, 2016 wakati Kitayosa itakuwa mgeni wa Madini kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha. Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Pepsi ambayo itacheza na JKT Oljoro Oktoba 30, mwaka huu.

Kundi C; Villa Squad itafungua dimba na Kariakoo ya Lindi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam wakati Burkinafaso ya itaikaribisha Abajalo kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Timu nyingine kwenye kundi hilo ni Cchanganyikeni na Cosmopolitan za Dar es Salaam.

Kundi D; Namungo ya Lindi itafungua dimba na Sabasaba kwenye Uwanja wa Sokoine ulioko Nachingwea mkoani Lindi wakati Mkamba Rangers itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkamba kuikaribisha Mawenzi Market kwenye Uwanja wa Mkamba ulioko Morogoro.

KICHUYA MCHEZAJI BORA WA LIGI KUU SEPTEMBA



Mshambuliaji Shiza Kichuya wa Simba SC amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa Septemba msimu wa 2016/2017.

Kichuya ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.

Mchezaji aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza Ligi hiyo inayoshirikisha timu 16. Pia alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne ilizocheza timu yake.

Kwa kushinda tuzo hizo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.

Monday, October 17, 2016

YANGA, AZAM HAKUNA MBABE


YANGA na Azam jana zilizidi kutoa mwanya kwa Simba kujikita kileleni mwa ligi kuu, baada ya kutoka suluhu katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kutokana na sare hiyo, Yanga sasa inazo pointi 15 baada ya kucheza mechi nane, ikitoka sare mechi tatu, imefungwa moja na kushinda nne.

Kwa upande wa Azam, sare hiyo imeifanya iwe na pointi 12 baada ya kucheza mechi tisa, ambapo imetoka sare mechitatu, imefungwa tatu na kushinda tatu.

Licha ya timu zote mbili kushambuliana kwa zamu, pambano hilo halikuwa na mvuto uliotarajiwa, kutokana na wachezaji wa timu hizo kuonyeshana ubabe zaidi.

SAMATTA ATEULIWA KUWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA



NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ni kati ya wachezaji 30 walioingia kwenye orodha ya awali ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika.
Samatta anayechezea KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, ameingia na wachezaji wawili wa Afrika Mashariki kipa Mganda, Dennis Onyango anayechezea Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na kiungo Mkenya, Victor Wanyama anayechezea Tottenham Hotspur ya England.
Orodha hiyo inaongozwa na Waalgeria watatu; mshambuliaji wa mabingwa wa England, Riyad Mahrez, Islam Slimani wa Leicester City na El Arabi Hillel Soudani wa Dinamo Zagreb.
Mkongwe Samuel Eto’o anayechezea Antalyaspor ya Uturuki naye yumo kwenye orodha, pamoja na Mcameroon mwenzake, Benjamin Mounkandjo wa Lorient.
Wengine ni Serge Aurier (Ivory Coast na PSG), Eric Bailly (Ivory Coast na Manchester City), Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Ivory Coast na Hebei Fortune), Mohamed Salah (Misri na Roma), Mohamed El Neny (Misri na Arsenal).
Wamo pia Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon na Dortmund), Andre Ayew (Ghana na West Ham), William Jebor (Liberia na Wydad Athletic Club), Mehdi Benatia (Morocco na Juventus), Hakim Ziyech (Morocco na Ajax), John Mikel Obi (Nigeria na Chelsea), Kelechi Iheanacho (Nigeria na Manchester City).
Wengine ni Ahmed Musa (Nigeria na Leicester City), Cedric Bakambu (DR Congo na Villareal), Yannick Bolasie (DRC na Everton), Sadio Mane (Senegal na Liverpool), Kalidou Koulibaly (Senegal na Napoli), Keegan Dolly (Afrika Kusini na Mamelodi Sundowns), Itumeleng Khune (Afrika Kusini na Kaizer Chiefs, Aymen Abdennour wa Tunisia na Valencia, Wahbi Khazri (Tunisia na Sunderland)  na Khama Billiat (Zimbabwe na Mamelodi Sundowns).
Ikumbukwe Samatta ndiye anashikilia tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika aliyotwaa Januari mwaka huu kufuatia kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe ya DRC mwaka jana na kuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.
Ni mafanikio hayo yalimfanya anunuliwe na klabu ya Genk iliyoizidi kete Lyon ya Ufaransa na klabu nyingine ziliokuwa zinataka huduma ya mchezaji huyo wa zamani wa Simba SC.

SIMBA YAZIDI KUCHANJA MBUGA, YAIBANJUA KAGERA SUGAR 2-0


SIMBA juzi iliendelea kujidhatiti kileleni mwa ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-0.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Simba ilipata mabao hayo mawili, moja katika kila kipindi, wafungaji wakiwa Muzamil Yassin na Shiza Kichuya.

Kutokana na ushindi huo, Simba inaendelea kuongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa, ikifuatiwa na Stand United yenye pointi 20 baada ya kucheza mechi 10.

Iliwachukua Simba dakika 43 kuhesabu bao la kwanza lililofungwa na Muzamil, aliyeunganisha wavuni kwa kichwa kona maridhawa kutoka kwa Kichuya.

Kichuya aliiongezea Simba bao la pili dakika ya 75 baada ya kuukwamisha mpira wavuni kwa njia ya penalti, iliyotokana na beki Juma Ramadhani wa Kagera Sugar kumwangusa Mo Ibrahim ndani ya eneo la hatari.

Katika mechi hiyo, wanasoka wa kulipwa wa Simba, Frederick Blagnon na Laudit Mavugo walishindwa kuonyesha uwezo wao, hali iliyosababisha malalamiko kutoka kwa mashabiki.

Friday, October 14, 2016

SIMBA KUIKARIBISHA KAGERA SUGAR UWANJA WA TAIFA KESHO



Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Oktoba 15, 2016 kwa michezo mitatu ambako Simba inayoongoza katika msimamo wa kuwania taji hilo katika timu 16 itaikaribisha Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo Na.73, mwamuzi atakuwa Hussein Athuman kutoka mkoani Katavi ambako pembeni atasaidiwa na Joseph Bulali wa Tanga na Silvester Mwanga wa mkoani Kilimanjaro wakati Soud Lila wa Dar es Salaam atakuwa mwamuzi wa akiba huku Kamishna wa mchezo akiwa Pius Mashera wa Dodoma.

Mchezo mwingine utakuwa ni kati ya JKT Ruvu na Mwadui ya Shinyanga. Ni mchezo Na. 74 utakaofayika Uwanja wa Mabatini ulioko Mlandizi mkoani Pwani ambako utachezeshwa na Mwanamama mwamzi mwenye beji la FIFA, Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam, akisaidiwa na Shafii Mohamed pia wa Dar es Salaam na Gesper Ketto wa Arusha.

Mwamuzi wa akiba atakuwa Abdallah Rashid wa Pwani wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Charles Mchau wa Kilimanjaro.

Pia Stand United ya Shinyanya itaikaribisha African Lyon kwenye Uwanja wa CCM Kambarage katika mchezo Na. 75 ambao utachezeshwa na Eric Onoka wa Arusha akisaidiwa na Agnes Pantaleo pia wa Arusha na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Joseph Pombe wa Shinyanga. Kamishna wa mchezo atakuwa Hamisi Kitila wa Singida.

Ligi hiyo itaendelea keshokutwa Jumapili kwa mchezo utakaozikutanisha timu za Azam na Young Africans; zote za Dar es Salaam. Mwamuzi wa mchezo huo Na. 76 atakuwa Israel Nkongo wa Dar es Salaam. Nkongo atasaidiwa na Soud Lila       na Frank Komba na mwamuzi wa akiba atakuwa Helen Mduma; wote wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Michael Wambura pia wa Dar es Salaam.

Mchezo Na. 77 utazikutanisha timu za Ruvu Shooting na Mbeya City Jumapili Oktoba 16, 2016 kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani. Mwamuzi wa mchezo huo atakuwa Rudovic Charles wa Tabora akisaidiwa na Samwel Mpenzu wa Arusha na Jeremina Simon    wa Dar es Salaam. Kamisha wa mchezo huo atakuwa Idelfonce Magali wa Morogoro.

Mtibwa Sugar ya Morogoro na Tanzania Prisons ya Mbeya nazo zitacheza Jumapili Oktoba 16 kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro. Mchezo huo Na. 78 utachezeshwa na Elly Sasii wa Dar es Salaam. Waamuzi wasaidizi ni Ferdinand Chacha wa Mwanza Lulu Mushi wa Dar s Salaam wakati mwamuzi wa akiba Nicolaus Makalanga wa Morogoro. Kamishna ni George Komba wa Dodoma.

Kwa siku ya Jumapili mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Toto African ya Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Mchezo huo Na. 79 utachezeshwa na mwamuzi Shomary Lawi wa Kagera akisaidiwa na Abdallah Uhako wa Arusha na Julius Kasitu wa Shinyanga huku mwamuzi wa akiba akiwa Mathew Akrama wa Mwanza. Kamishna atakuwa Michael Bundala wa Dar es Salaam.

SMART KUTOA BURE HUDUMA YA WIFI WAKATI WA TAMASHA LA KNDANDA DAY


Mratibu wa Tamasha la Kandanda Day (Katikati), Fatma Dahir, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya mwisho ya kandanda day ambayo itafanyika katika viwanja vya Jakaya M. Kikwete Youth Park, Oktoba 15 Mwaka Huu.

KAMPUNI ya simu za mikononi ya Smart,inatarajia kutoa huduma ya bure ya mtandao  wa  Wifi  katika tamasha  la Kandanda  Day,litakalofanyika leo,katika Uwanja wa Jakaya M Kikwete Youth Park,Kidogo Chekundu.

Mratibu wa tamasha hilo,Fatma Dahir,alisema kwamba maandalizi kuelekea tamasha hilo yamekamilika na wanaishukuru kampuni ya  Smart kwa kuwawekea wanakandanda huduma ya kuperuzi mtandao wa intaneti bure wakiwa uwanjani.


“Tunapenda kuwatangazia wanakandanda wote kuwa maandalizi yamekamilika kila kitu,halikadhalika tunapenda pia kuishukuru kampuni ya Smart,kwa kuamua kusherehesha tamasha letu kwa kuwawekea huduma ya ‘free wifi’ kwa watakaohudhuria,”alisema Fatma na kuongeza:

“Halikadhalika,napenda pia kusisitiza timu  shiriki ambazo ni Akiba Commercial bank,Taswa Fc,Coca Cola,Smart,Dar City Fc,Team Dizo Moja na Team Ismail,zijitahidi kuwahi mapema,ili tuweze kufanikisha lengo letu katika muda tuliopanga.”


Tamasha hilo ambalo lengo lake kuu ni kuchangia madawati kwa shule teule ya  msingi ya  Msumi,linapambwa na kampuni ya matairi ya Bin Slum Tyres Ltd,Smart,Coca Cola,Galacha na kituo cha House of Blue Hope.  
 
Imeandaliwa na Mratibu
Mohamed Mkangara

TFF YATANGAZA TENDA YA JEZI MPYA ZA TAIFA STARS



 Shirikisho Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linaalika umma kuwania zabuni ya kubuni mwonekano mpya wa jezi mpya za timu ya taifa zitakazotumika kwa msimu wa 2017/18 na msimu wa 2018/19.

Kwa taarifa hii, TFF imefungua milango kwa umma ambako mtu mmoja mmoja anaweza kuwasilisha ubunifu wa mwonekano wa jezi hizo katika ofisi zake zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume ulioko kwenye makutano ya barabara za Uhuru na Shaurimoyo, Ilala jijini Dar es Salaam.

Wakati mwisho wa kupokea zabuni hizo ni Novemba 30, 2016, sharti kwa mbunifu ni kutoiga ubunifu kutoka makampuni makubwa ya vifaa vya michezo. Na Mbunifu Bora au Mshindi wa jezi ambazo zitakuwa lazima ziwe na nembo ya TFF na Bendera ya Taifa, atazawadiwa shilingi milioni mbili (Sh milioni 2).

Jezi za sasa za Timu ya Taifa ni rangi ya bluu kwa michezo nyumbani na nyeupe mechi za ugenini.