KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, January 8, 2016

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA JUMA ALI DAVID



Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambirambi kwa chama cha soka cha Zanzibar (ZFA) kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu wa FIFA Juma Ally Khamis kilichotokea jana kisiwani Pemba.

Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wadau wa mpira wa miguu na kusema TFF ipo pamoja na wafiwa katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.

Wakati wa uhai wake marehemu Juma Ally Khamis alikuwa mwamuzi mwenye beji ya FIFA, mkufunzi wa waamuzi Tanzania, Meneja wa uwanja wa Amani – uliopo Zanzibar na mratibu wa michezo Wizara ya Habari na Utamaduni na Michezo kisiwani Zanzibar.

Mazishi yalifanyika juzi  nyumbani kwake Pemba.

Wakati huo huo, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), limetuma salamu za rambirambi kwa kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Suleiman “Morocco” kufutia kifo cha baba yake mzazi Suleiman Ally Hemed kilichotokea juzi kisiwani Zanzibar.

Katika salamu hizo za rambirambi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wapo pamoja na familia ya marheemu katika kipindi hiki kigumu cha maombeloezo.

Aidha pia TFF imetuma rambirambi (ubani) wa shilingi laki mbili (200,000) kwa familia ya kocha Hemed Moroco kufuatia kifo cha baba yake Suleiman Ally.

Mazishi ya marehmu Suleiman Ally Hemed mefanyika jana jioni mjini Zanzibar

No comments:

Post a Comment