KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, January 4, 2016

AZAM, MTIBWA ZATOKA SARE KOMBE LA MAPINDUZI


TIMU za Mtibwa Sugar na Azam FC zimegawana pointi katika mchezo wa Kundi B wa Kombe la Mapinduzi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 usiku wa Jumapili, kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Matokeo hayo yanazifanya timu hizo za Tanzania Bara zifungane kwa kila kitu, nyuma ya Yanga SC yenye pointi tatu na mabao matatu, wakati Mafunzo inashika mkia ikiwa haina pointi.

Mtibwa Sugar walianza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Hussein Javu anayecheza kwa mkopo kutoka Yanga SC.

Azam FC walisawazisha kupitia kwa nahodha wake, John Bocco kwa penalti, ambaye yeye mwenyewe alichezewa rafu ndani ya boksi.

No comments:

Post a Comment