KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, January 8, 2016

MAFUNZO YAIFUNGASHA VIRAGO AZAM KOMBE LA MAPINDUZI



KWA mara ya kwanza katika historia ya Kombe la Mapinduzi, Azam FC imetolewa katika hatua ya makundi, baada ya kufungwa mabao 2-1 jioni ya leo na Mafunzo FC Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Azam FC pia inaondoka bila ya ushindi katika mashindano hayo, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia yake ya ushiriki wa michuano hiyo ikimaliza na pointi mbili, za sare dhidi ya Yanga na Mtibwa Sugar, zote 1-1 pamoja na kipigo cha leo.
Aliyewarudisha mapema Azam FC Dar es Salaam leo ni Habib Sadik aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Haji Abdi dakika ya 90 na ushei kuipatia Mafunzo bao la pili.
Azam FC walitangulia kupata bao kupitia kwa mshambuliaji Kipre Herman Tchetche dakika ya 20 akimalizia kona iliyochongwa na beki wa kulia, Shomary Kapombe
Mafunzo ambao leo walicheza bila kocha wao Mkuu, Hemed Morocco, aliyefiwa na mama yake mzazi, ilipata bao la kusawazisha dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wake, Rashid Abdallah  aliyemalizia pasi ya Ali Hassan.
Matokeo haya yanazifanya Yanga SC na Mtibwa Sugar zenye pointi nne kila moja zifuzu moja kwa moja hatua ya nusu fainali na zitamenyana katika mechi ya mwisho ya kundi A usiku wa leo kusaka mshindi wa kwanza na wa pili.

CHANZO CHA HABARI: BINZUBEIRY BLOG

No comments:

Post a Comment