KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 7, 2013

YANGA YAKWEA KILELE, AZAM NA MBEYA CITY HAKUNA MBABE



MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Bara, jana walimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo wakiwa wa kwanza, baada ya kuicharaza JKT Oljoro mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo uliiwezesha Yanga kuwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 13, na kuzipiku Azam na Mbeya City, ambazo zimetoka sare ya mabao 3-3 na kumaliza mzunguko huo zikiwa na pointi 27 kila moja.

Yanga ilihesabu bao lake la kwanza dakika ya 21 kupitia kwa kiungo wake, Haruna Niyonzima kabla ya Mrisho Ngasa kufunga bao la pili dakika ya 30. Bao la tatu lilifungwa na Jerry Tegete dakika ya 52.

Wakati huo huo, Azam na Mbeya City zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika mechi iliyopigwa kwenye uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment