KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 21, 2013

YANGA B HOI KWA AZAM B



AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi katika michuano ya Kombe la Uhai baada ya kuilaza Yanga mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mabao ya Azam yalifungwa na Adam Omar dakika ya saba na Gadiel Michael dakika ya 39.

Katika mchezo mwingine uliofanyika Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam, Mtibwa Sugar iliichapa Rhino Rangers ya Tabora bao 1-0.

Bao hilo la pekee na la ushindi la Mtibwa lilifungwa na Patrick Mdidi dakika ya 38.

Katika mechi zilizochezwa asubuhi, Ashanti United iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Oljoro ya Arusha kwenye uwanja wa Azam Complex.

Mabao yote mawili ya Ashanti yalifungwa na mtoto wa beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Yanga, Salum Kabunda ‘Ninja Msudan’ (marehemu), aitwaye Ally Salum Kabunda anayecheza na mdogo wake, Hassan Salum Kabunda.

Katika mechi nyingine, Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Prisons ya Mbeya.
Mabao ya Kagera yalifungwa na Mohammed Mohammed na Hassan Rajab.

Kwenye uwanja wa DUCE, Mbeya City iliifunga JKT Ruvu bao 1-0 wakati Ruvu Shooting ikatoka sare ya 1-1 na Mgambo JKT.

No comments:

Post a Comment