KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 10, 2013

KOMBE LA UHAI NOVEMBA 17


Michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye umri chini ya miaka 20
wa klabu za Ligi Kuu inaanza kutimua vumbi Novemba 17 mwaka huu katika viwanja
vya Karume na Azam Complex, Dar es Salaam.

Droo ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Maji Uhai imefanyika leo (Novemba 8
mwaka huu) mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) ambapo timu zimepangwa katika makundi matatu.

Kundi A linaundwa na timu za Azam, Coastal Union, JKT Ruvu Stars, Mbeya City na
Yanga, wakati kundi B ni Ashanti United, Mgambo Shooting, Oljoro JKT na Ruvu
Shooting. Kagera Sugar, Mtibwa Sugar, Rhino Rangers na Tanzania Prisons ndizo
zinazounda kundi C.

Mechi za ufunguzi kundi A Novemba 17 mwaka huu ni kati ya Azam na Coastal
Union (saa 2 asubuhi- Karume), Yanga na Mbeya City (saa 8 mchana- Karume).
Kundi B ni Ruvu Shooting na Ashanti United (saa 4 asubuhi- Karume), Oljoro JKT na
Simba (saa 10 jioni- Karume).

Kagera Sugar na Mtibwa Sugar (saa 2 asubuhi- Azam) na Rhino Rangers na
Tanzania Prisons (saa 10 jioni- Azam) ndizo zitakazocheza mechi za ufunguzi
Novemba 17 mwaka huu katika kundi C.

Robo fainali ya michuano hiyo itachezwa Novemba 24 na 25 mwaka huu wakati
nusu fainali itapigwa Novemba 26 na 27 mwaka huu. Mechi ya kutafuta mshindi wa
tatu na ile ya fainali zitachezwa Novemba 30 mwaka.

No comments:

Post a Comment