KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, November 11, 2013

WAAMUZI 18 KUCHEZESHA KOMBE LA CHALENJI, WAMO WATANZANIA WATATU


BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), leo limetangaza majina ya waamuzi 18 watakaochezesha michuano ya mwaka huu ya Kombe la Chalenji itakayofanyika nchini Kenya.

Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amesema leo kuwa, kati ya waamuzi hao, tisa watakuwa wa kati na wengine tisa wasaidizi.

Musonye amesema waamuzi wote hao watalazimika kwenda Nairobi mapema kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya zao pamoja na uimara wa mwili.

Michuano hiyo imepangwa kuanza Novemba 27 mwaka huu, ikizishirikisha nchi zote wanachama wa baraza hilo kongwe barani Afrika.

Waamuzi wa kati ni :
1. Anthony Okwayo-Kenya
2. Denis Batte-Uganda
3. Wish Yabarow- Somalia
4. Israel Mujuni- Tanzania
5. Louis Hakizimana- Rwanda
6. ThieryNkurunziza- Burundi
7. WaziriSheha- Zanzibar
8. GebremichaelLuleseged- Eritrea
9. KheiralaMurtaz - Sudan
Waamuzi wasaidizi ni
1. Gilbert Cheruiyot- Kenya
2. TonnyKidiya- Kenya
3. Mark sonko- Uganda
4. FedinardChacha- Tanzania
5. Suleiman Bashir- Somalia
6. Fraser Zakara-South Sudan
7. SimbaHonore-Rwanda
8. Hamid Idam- Sudan
9. KinfeYimla-Ethiopia

No comments:

Post a Comment