KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 28, 2013

CANNAVARO AMPA TANO KASEJA


NAHODHA wa timu ya soka ya Yanga, Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema, amefurahia kusajiliwa kwa kipa nyota nchini, Juma Kaseja, aliyeachwa na klabu ya Simba.
Cannavaro amesema, ujio wa Kaseja utakuwa na msaada mkubwa kwa Yanga kwa sababu ni kipa mwenye uzoefu wa michuano ya ligi na kimataifa.
Kaseja alijiunga na Yanga hivi karibuni, akiwa mchezaji huru baada ya kulipwa kitita cha sh. milioni 40.
Kipa huyo wa zamani wa Simba, alitarajiwa kuanza mazoezi na Yanga juzi, lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu.
Kwa mujibu wa Cannavaro, Kaseja ataleta changamoto kubwa kwa timu hiyo, yenye makipa wengine wawili nyota, Ally Mustapha 'Bartez' na Deogratius Munishi 'Dida'.
"Nampenda sana Kaseja kwa sababu ni kipa mzuri na anayependa mazoezi. Naamini uzoefu wake utatusaidia sana katika ligi na michuano ya kimataifa,"alisisitiza beki huyo.
Aliitaja sifa nyingine ya Kaseja ni kuwa kiongozi mzuri wa wachezaji wenzake, kwa kuwaeleza jinsi ya kujipanga na pia kuwakumbusha majukumu yao wanapokuwa uwanjani.
"Nimeshawahi kucheza naye nikiwa Yanga na timu ya Taifa, hivyo namjua vizuri na ninavutiwa na uwezo wake,"alisema Cannavaro.

No comments:

Post a Comment