KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, November 5, 2013

KIGOGO ANG'OLEWA TFF

 
 
KAMATI mpya ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko ya wasimamizi wa mikoa katika michuano ya ligi.
 
Katika mabadiliko hayo, kamati hiyo imemtosa msimamizi wa kituo cha Dar es Salaam, Msafiri Mgoyi, ambaye alikiongoza kwa kipindi cha miaka minane iliyopita.
 
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura imesema kituo hicho sasa kitakuwa chini ya mjumbe mpya wa kamati ya utendaji, Wilfred Kidau.
 
Kwa kawaida, wajumbe wa kamati ya utendaji ndio huteuliwa kusimamia vituo vya ligi.
 
Mgoyi amekuwa mjumbe wa kamati ya utendaji kwa miaka minane, akitokea mkoa wa Kigoma. Ni mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF kutoka mkoa huo.
 
Mgoyi amechaguliwa tena kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji kutoka mkoa huo na kuweka rekodi ya kushika wadhifa huo kwa kipindi kingine cha miaka mine ijayo.
 

No comments:

Post a Comment