KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 10, 2013

WATATU WAOMBEWA ITC UJERUMANI



Watanzania watatu wameombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) na Chama
cha Mpira wa Miguu Ujerumani (DFB) ili wacheze mpira wa miguu nchini humo.

Wachezaji hao ni Charles Mishetto na David Sondo wanaombewa hati hiyo ili waweze
kujiunga na timu ya SpVgg 1914 Selbitz, wakati Eric Magesa ameombewa kibali
hicho ili achezee timu ya klabu ya SC Morslingen.

Hata hivyo, katika maombi hayo DFB haikuleza hapa nchini walikuwa wakicheza
katika klabu zipi. Wachezaji wote wameombewa hati hiyo kama wachezaji wa ridhaa.

No comments:

Post a Comment