KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 10, 2013

DIRISHA DOGO KUFUNGULIWA NOVEMBA 15


Usajili wa wachezaji kwa dirisha dogo kwa msimu wa 2013/2014 Tanzania Bara
unafunguliwa Novemba 15 mwaka huu na utafungwa rasmi Desemba 15 mwaka
huu.

Kwa mujibu wa kanuni, klabu zenye fursa ya kusajili wachezaji katika dirisha dogo ni
zile ambazo hazijatumia nafasi zote 30 za wachezaji.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zimemaliza duru la
kwanza msimu huu. Duru za pili litaanza kutimua vumbi Januari mwakani.

Kwa mujibu wa Kalenda ya Matukio ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
matukio ya Novemba na Desemba ni dirisha dogo la usajili na mechi za kirafiki za
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)- FIFA Date.

Matukio mengine ni michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha wachezaji wenye
umri chini ya miaka 20 wa klabu za VPL na michuano ya Kombe la Chalenji
itakayofanyika Nairobi, Kenya.

No comments:

Post a Comment