KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, November 5, 2013

THE TANZANITES KWENDA MSUMBIJI KESHO


Kikosi cha timu ya SOKA YA Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (The Tanzanites), kinaagwa kesho (Novemba 6 mwaka huu) saa chache kabla ya kuanza safari ya kwenda Maputo, Msumbiji.

Hafla fupi ya kuikabidhi bendera Tanzanites itafanyika kesho saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF wakati kikosi hicho kinatarajiwa kupaa saa 11 jioni kwa ndege ya LAM na kuwasili Maputo saa 3.45 usiku.

Msafara wa Tanzanite ambayo ilishinda mechi ya kwanza mabao 10-0 karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Kidao Wilfred.

Mechi hiyo ya marudiano itachezwa Novemba 9 mwaka huu Uwanja wa Taifa wa Zimpeto, na timu itarejea nyumbani Novemba 10 mwaka huu saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.

Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments:

Post a Comment