KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 10, 2013

KASEJA SASA RASMI YANGA, ALIPWA MIL 40/-


HATIMAYE ile minong'ono na mustakabali wa kipa wa kimataifa wa Tanzania, Juma Kaseja sasa imemalizika baada ya kuamua kumwaga wino Yanga.

Kaseja, ambaye msimu uliopita aliichezea Simba, amemwaga wino Yanga kwa mkataba wa miaka miwili, ulioanza Jumamosi iliyopita.

Kwa mujibu wa mkataba huo, Kaseja amemwaga wino Yanga kwa malipo ya sh. milioni 40.

Mkataba huo ulitiwa saini na Kaseja mbele ya wajumbe wa kamati ya usajili ya Yanga, Abdalla Bin Kleb na Ahmed Seif 'Magari'. Pia alikuwepo wakala wa Kaseja, Abdulfatah Saleh.

Kusajili kwa Kaseja kunaifanya Yanga sasa iwe na makipa watatu. Wengine ni Ally Mustapha 'Barthez' na Deogratius Munishi 'Dida'.

Barthez alikuwa kipa namba moja wa Yanga mwanzoni mwa msimu huu, lakini alipoteza namba kwa Dida mwishoni mwa mechi za mzunguko wa ligi.

Hii ni mara ya pili kwa Kaseja kusajiliwa na Yanga. Mara ya kwanza ilikuwa msimu wa 2009/2010.

Sababu kubwa ya kuachwa kwa Kaseja katika kikosi cha Simba ni madai kuwa kiwango chake kimeshuka. Nafasi yake ilichukuliwa na Abel Dhaira kutoka Uganda.

Baada ya kutupiwa virago, Kaseja hakuichezea timu yoyote katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi uliomalizika wiki iliyopita.

Kaseja amewahi kuzichezea timu za Moro United kuanzia 2001, timu ya Taifa ya vijana wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys kabla ya kuhamia Simba 2003.

No comments:

Post a Comment