KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 3, 2013

YANGA RAHA TUPU



JANGWANI wanacheka! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kuendelea kutoa dozi kwa timu za majeshi baada ya jioni hii kuivurumusha JKT Ruvu kwa mabao 4-0 na kukalia kiti cha uongozi wa ligi hiyo.


Mabao mawili ya mapema ya Mrisho Ngassa 'Uncle' na mengine ya kipindi cha pili yaliyofungwa na beki wa kushoto, Oscar Joshua na jingine la Jerry Tegete yameifanya Yanga kufikisha pointi 25 kutokana na kucheza mechi 12, huku Ngassa akifikisha jumla ya mabao matano katika orodha ya wafungaji na Tegete kufikisha manne.

Ushindi huo wa Yanga ni wa tatu mfululizo kwa maafande wa Jeshi baada ya awali kuitafuna Mgambo mabao 3-0 kisha kuisulubu Rhino Rangers kwa idadi hiyo kabla ya leo kuisasambua JKT Ruvu.

No comments:

Post a Comment