KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 10, 2013

TANZANITES YAIUA TENA MSUMBIJI


Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi
ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada
ya  kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.

Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini
Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati
mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia Minja.

Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred uliwasili Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jana Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa
8.30 mchana kwa ndege ya LAM.

Tanzanite inayofundishwa na Rogasian Kaijage, itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi
ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6
na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba
20-22 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment