KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, August 4, 2017

TFF YAPANGUA MAKUNDI YA LIGI DARAJA LA KWANZA


Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko kidogo ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.

Timu ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi mechi zake katika Kundi ‘A’.

Kwa msingi huo, makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kund, zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19 yatakuwa hivi:-

Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.

Kundi ‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na Mawezi Market ya Morogoro.

Kundi ‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

No comments:

Post a Comment