KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 3, 2017

SIMBA YATOKA SARE YA BAO 1-1 NA MABINGWA WA AFRIKA KUSINI


SIMBA SC imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na mabingwa wa Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini, Bidvest Wits katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Sturrock Park, Chuo Kikuu cha Afrika Kusini asubuhi ya leo.


Katika mchezo huo wa kujipima nguvu kujiandaa na msimu mpya, Simba SC walikuwa wa kwanza kupata bao, lililofungwa na beki anayeweza kucheza kama kiungo pia, Erasto Edward Nyoni dakika ya 33 kabla ya wenyeji kusawazisha.


Huo ulikuwa mchezo wa pili wa kirafiki wa Simba katika kambi yake Afrika Kusini kujiandaa na msimu, baada ya Jumamosi kufungwa 1-0 Orlando Pirates.


Baada ya mchezo huo, Simba SC inatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania kwa ajili ya mchezo mwingine wa kujipima nguvu dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda Agosti 8, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar  es Salaam.

No comments:

Post a Comment