KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 3, 2017

NIYONZIMA RASMI MALI YA SIMBA,KUTAMBULISHWA SIMBA DAY


Mabingwa wa Kombe la FA Cup timu ya Simba imetangaza rasmi kuwa imeingia mkataba wa miaka miwili kiungo hodari Haruna Niyonzima ambaye amemaliza mkataba wake na Mabingwa wa Vodacom Yanga.

Leo au kesho, kiungo Haruna Niyonzima anaweza kuungana na wenzake Afrika Kusini Sasa una sababu ya kuwa na hofu kwa kuwa Simba wenyewe wameshasema Niyonzima ni mchezaji wao.

Awali kulikuwa na uficho wa mambo, lakini sasa kila kitu kiko hadharani kuwa Niyonzima atavaa jezi nyekundu na nyeupe msimu wa 2017-18.

Simba waliendelea kufanya siri usajili wa Niyonzima kwa kuwa mkataba wake na Yanga wakati wakimalizana naye haukuwa umekamilika.

Lakini sasa Simba wamevunja ukimya na wanaweza kulizungumzia suala hilo hadharani kwa kuwa mkataba wa Yanga na kiungo huyo Mnyarwanda umekamilika.

No comments:

Post a Comment