KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, September 22, 2010

SIKINDE YAMKABIDHI MAUFI GITA LA SOLO

MWANAMUZIKI Kaingilila Maufi (wa tatu kulia) akikabidhiwa gita la solo na kiongozi wa bendi ya Mlimani Park Orchestra, Habibu Abbas ‘Jeff’ (wa tatu kushoto) wakati wa onyesho lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, Dar es Salaam.


UONGOZI wa bendi ya muziki wa dansi ya Mlimani Park Orchestra umemkabidhi rasmi mwanamuziki Kaingilila Maufi jukumu la kuwa mpiga gita la solo.
Hafla ya kumkabidhi jukumu hilo Maufi, ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita wakati wa onyesho la bendi hiyo lililofanyika kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, Dar es Salaam.
Maufi alikabidhiwa gita hilo na kiongozi wa bendi hiyo, Habibu Abbas Jeff na kushuhudiwa na wanamuziki wenzake pamoja na baadhi ya wanachama wa Sikinde Family.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, mwanamuziki Hassan Kunyata alisema, Maufi amekabidhiwa gita hilo kutokana na uhodari wake wa kujifunza kupiga ala nyingi za muziki.
Kabla ya kuanza kupiga solo, Maufi alikuwa gita la rythim na ni mmoja kati ya watunzi hodari wa nyimbo.
Onyesho hilo, lililohudhuriwa na mashabiki lukuki, lilikuwa la kwanza kwa Mlimani Park mjini Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Bendi hiyo ilialikwa kwenda kufanya maonyesho katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Kagera wakati wa sikukuu ya Idd El Fitri.
Wakati huo huo, msemaji mkuu wa bendi hiyo, Jimmy Chika alisema Mlimani Park inajiandaa kupakua vibao vipya vitatu vilivyotungwa wakati wa mwezi wa Ramadhani.

No comments:

Post a Comment