KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, September 22, 2010

Wachezaji Twiga Stars wajigamba


WACHEZAJI wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, 'Twiga Stars' wametamba kufanya vizuri katika michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika itakayofanyika mwezi ujao nchini Afrika Kusini.
Majigambo ya wachezaji hao yamekuja siku moja baada ya timu hiyo kupangwa kundi A katika michuano hiyo, pamoja na wenyeji Afrika Kusini, mabingwa wa zamani, Nigeria na Mali.
Upangaji wa makundi ya michuano hiyo ulifanyika juzi nchini Afrika Kusini na kundi hilo limebatizwa jina la kifo kutokana na kuundwa na vigogo vya soka ya wanawake barani Afrika.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, nahodha wa Twiga Stars, Sophia Mwasikili alisema, wanatambua vyema kwamba kundi walilopangwa ni gumu, lakini maandalizi waliyoyafanya yanawapa matumaini ya kufanya vizuri.
"Tupo kambini muda mrefu na kila siku tunafanya mazoezi ya nguvu na kujituma kwa pamoja, kitu ambacho kimetujengea hali ya kuelewana vyema uwanjani, hivyo nadhani tutafanya vizuri," alisema
Michuano hiyo, inayotarajiwa kuanza Octoba 29 hadi Novemba 14 mwaka huu, itashirikisha timu nane, ambapo Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza baada ya kuzitoa Ethiopia na Eritrea.
Nchi zingine zitakazoshiriki kwenye fainali hizo, ambazo zimepangwa kundi B ni bingwa mtetezi Equatorial Guinea, Ghana, Cameroon na Algeria.

No comments:

Post a Comment