KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 16, 2010

KOPA: Mtasema sana, sijafulia, nazidi kupeta


BAADA ya ukimya wa muda mrefu, mwimbaji machachari wa muziki wa taarab nchini, Khadija Omar Kopa ameibuka na kusema kuwa hajafilisika kiusanii.
Badala yake, Khadija amesema bado anaendelea kuteza katika muziki huo na kwamba ataendelea hivyo kwa kipindi kirefu kijacho.
Khadija amesema kauli zinazotolewa na baadhi ya wadau wa muziki huo kwamba ukimya wake unaonyesha amefilisika, hazina ukweli wowote.
“Mimi sijafulia, wanaosema hivyo watasema sana, bado nipo juu na ninazidi kupeta, wanaofikiria nimefulia, wanajidanganya nafsi zao,”alisema.
Khadija alisema hayo wiki iliyopita wakati wa mkutano wa kampeni wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Jakaya Kikwete uliofanyika katika mji wa Kilosa.
Katika mkutano huo uliohudhuriwa na watu lukuki, Khadija alitoa burudani kali alipoimba kibao chake kipya, kinachokwenda kwa jina la Wanaume magumegume.
Khadija alijigamba kuwa, yeye bado ni malkia wa muziki wa mipasho nchini na kwamba hana mpinzani. Aliisifu CCM kwa namba inavyotekeleza ilani yake ya uchaguzi.
Khadija alianza kupata umaarufu alipokuwa katika kikundi cha taarab cha Culture cha Zanzibar, ambako alitamba kwa vibao vyake vya Daktari, Kadandie na Wahoi.
Baadaye aliibukia kwenye kundi la Tanzania One Theatre (TOT-Plus) kabla ya kuhamia kundi la Muungano na kisha East African Melody.

No comments:

Post a Comment