KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 2, 2010

Manchester Band yatimua wanne, yaajiri wapya watano

BENDI ya muziki wa dansi ya Manchester imewatimua wanamuziki wake wanne wa zamani na kuajiri wengine wapya wanne kutoka bendi mbalimbali.
Mkurugenzi wa bendi hiyo, Jerome Mponda alisema mjini Dar es Salaam juzi kuwa, wameamua kuajiri wanamuziki wapya kwa lengo la kujiimarisha zaidi.
Aliwataja wanamuziki waliotimuliwa kuwa ni pamoja na mwimbaji, Amina Renny, wapiga magita Peter Kanuti na Juma Yegela na mpiga drums, Riziki Salehe ‘Chocholi’.
Jerome alisema wamefikia uamuzi wa kuwatimua wanamuziki hao wanne kwa makosa mbalimbali ya utovu wa nidhamu, ikiwa ni pamoja na ulevi wa kupindukia na kuchelewa mazoezini.
Kwa mujibu wa Jerome, wanamuziki wapya walioajiriwa na bendi hiyo hivi karibuni ni wacheza shoo Mariam Hussein kutoka Akudo, Monalisa Saidi, Judith Dalu na Merisa Joseph kutoka kundi la Nyamwela.
Katika orodha hiyo, pia yumo mwimbaji Hija Kimodo, ambaye amerejea tena kwenye bendi hiyo baada ya kurejea kutoka kwao Songea, alikokwenda kushughulikia matatizo ya familia yake.
Jerome alisema wameamua kuajiri wacheza shoo wengi ili kuipa bendi hiyo mvuto zaidi kwa mashabiki na pia kuifanya iende na wakati.
“Kwa kawaida wacheza shoo wana mvuto wa aina yake bendi inapokuwa jukwaani ikitumbuiza, hivyo tumewaajiri hawa wanne kwa lengo la kuongeza mvuto stejini,”alisema.
Mkurugenzi huyo alisema kwa sasa bendi yake ipo kwenye mapumziko ya mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na inatarajia kuanza maonyesho siku ya Idd el Fitr.
Alisema watalitumia onyesho la sikukuu ya Idi Mosi kutambulisha albamu yao mpya inayojulikana kwa jina la ‘Kijuba wa mtaa’, yenye nyimbo sita.

No comments:

Post a Comment