KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 2, 2010

K-Sher apigwa stop Tip Top Connection


MSANII pekee wa kike katika kundi la muziki wa kizazi kipya la Tip Top Connection, Khadija Shaaban amesimamishwa kufanya maonyesho ndani ya kundi hilo kwa muda usiojulikana.
Khadija, maarufu kwa jina la K-Sher, amesimamishwa ndani ya kundi hilo kwa tuhuma za makosa ya utovu wa nidhamu.
Meneja wa kundi hilo lenye maskani yake Manzese, Dar es Salaam, Khamis Tale alithibitisha wiki hii kuhusu kusimamishwa kwa msanii huyo.
Tale alisema wamefikia uamuzi huo baada ya msanii huyo kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu kwa muda mrefu na kukataa kubadilika kila alipoonywa na viongozi.
“Mara nyingi K-Sher amekuwa akifanya vitu, ambavyo vinaleta usumbufu kwa wenzake,”alisema Tale.
“Kwa mfano, hivi karibuni tulikuwa na onyesho Mwanza, lakini yeye alishindwa kufika kwa sababu tulishindwa kupata tiketi ya ndege ya kumsafirisha kwa muda huo, wenzake walikuja kwa basi na kufanya onyesho kisha wakarudi Dar,”aliongeza.
“Tulipofika Dar, akawa anadai alipwe pesa za onyesho hilo huku akitishia kujitoa kundini iwapo hatalipwa. Yapo mambo mengine mengi, ambayo msanii huyo amekuwa akiyafanya na kusababisha usumbufu kwa wenzake, kitu ambacho kimetusukuma sisi viongozi kuchukua uamuzi wa kumsimamisha mpaka hapo baadaye,” alisema Tale.

No comments:

Post a Comment