JOCELYNE Maro (22) mwezi uliopita aliweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kushinda taji la mrembo wa Afrika Mashariki baada ya kuwabwaga washiriki wenzake 12 kutoka katika nchi mbalimbali za ukanda huu wa Afrika. Katika makala hii ya ana kwa ana iliyoandikwa na Mwandishi Wetu, mrembo huyo anaelezea ushiriki wake katika shindano hilo na matarajio yake ya baadaye.
SWALI: Wewe ni Mtanzania wa kwanza kushinda taji la mrembo wa Afrika Mashariki tangu mashindano hayo yalipoanzishwa miaka mitano iliyopita. Ulijisikiaje ulipotangazwa kuwa mshindi?
JIBU: Nilifurahi sana. Kwanza nilipatwa na mshtuko kwa sababu sikutegemea kama nitashinda. Sio kwamba nasema mimi mbaya au nini, lakini wenzangu niliokuwa nashindana nao, wote walikuwa wazuri na tulikaa kambini kwa muda mrefu, tulizoeana kwa hiyo nilifurahi sana kwa sababu kushinda shindano hili ni kitu kikubwa sana.
SWALI: Unadhani ni kitu gani kilichokuwezesha kushinda taji hili?
JIBU: Kwa kweli siwezi kujua, majaji ndio wanaojua.
SWALI: Wazazi na ndugu zako waliupokeaje ushindi wako?
JIBU: Walifurahi sana. Mwanzoni Renna Callist (Mratibu wa mashindano haya) aliponiomba na kunishawishi nishiriki kwenye shindano hili, nilikuwa naogopa kumweleza baba na mama. Ni kwa sababu mashindano ya aina hii yamekuwa yakitawaliwa na skendo nyingi. Lakini siku nilipowaeleza, hawakuwa na kinyongo waliniruhusu. Kwa hiyo walifurahi sana baada ya mimi kushinda.
SWALI: Hii ni mara yako ya ngapi kushiriki katika mashindano ya urembo?
JIBU: Ilikuwa mara yangu ya kwanza. Nilikuwa sijawahi kushiriki kwenye mashindano ya aina hii. Hata Renna alipokuwa akinishawishi nishiriki, nilikuwa sijiamini.
SWALI: Kuna dhana iliyojengeka katika jamii kwamba mashindano ya urembo ni ya kihuni. Nini mtazamo wako kuhusu dhana hii?
JIBU: Mashindano ya urembo si ya kihuni. Tatizo lipo kwa baadhi ya washiriki wa mashindano hayo kuyatumia vibaya na hivyo kutoa mwanya kwa vyombo vya habari kuyafanya yaonekane kuwa ya kihuni. Nadhani uhuni ni tabia ya mtu. Lakini wapo wengi walioshiriki kwenye mashindano haya na ambao kwa sasa wamepata nafasi nzuri za kazi katika kampuni mbalimbali.
SWALI: Umejifunza nini kutokana na kushiriki kwenye mashindano haya?
JIBU: Nimejifunza vitu vingi sana kwa sababu wakati tulipokuwa kambini, tulitembelea sehemu nyingi. Tulikwenda Ngorongoro, ambako nilikuwa sijawahi kufika. Nimejifunza vitu vingi kuhusu Tanzania na pia kukutana na washiriki wenzangu kutoka nchi mbalimbali na hivyo kujifunza mengi kutoka kwao, hasa masuala ya kiutamaduni na kimaendeleo. Nilikuwa nafurahia kuzungumza nao kwa sababu ilikuwa nafasi nzuri kwangu kujua mengi kuhusu nchi zao.
SWALI: Nini majukumu yako baada ya kushinda taji la mrembo wa Afrika Mashariki?
JIBU: Moja ya majukumu yangu ni kusaidia kampeni za kupambana na magonjwa ya ukimwi, malaria na kutoa elimu ya magonjwa hayo na mambo mengineyo. Vilevile nitakuwa nikifanyakazi za kuwasaidia wanawake kuwapa moyo na kuinua maisha yao. Inawezekana pia nikaongezewa majukumu mengine, lakini kikubwa kwa sasa ni kutoa elimu ya kupambana na ukimwi na malaria.
SWALI: Kabla ya kushiriki kwenye shindano hili, ulikuwa ukijishughulisha na nini?
JIBU: Nilikuwa chuoni Uingereza. Nilikuwa nachukua shahada ya kwanza katika masuala ya uchumi na biashara. Nilimaliza mwezi Julai ndipo nikaja Tanzania kutafuta kibarua kwa muda ili baadaye nikaendelee na masomo. Lengo langu ni kurudi tena Uingereza kuchukua shahada ya uzamili.
SWALI: Masomo yako ya elimu ya msingi na sekondari ulichukulia wapi?
JIBU: Yote nilisoma Kenya.
SWALI: Kwa maana hiyo hujaishi sana Tanzania?
JIBU: Ni kweli, nilikuwa nakuja na kuondoka, lakini wazazi wangu wote wanaishi hapa Tanzania.
SWALI: Wazazi wako wanajishughulisha na nini kwa sasa?
JIBU: Mama yangu anafanyakazi Agha Khan na baba yangi anafanyakazi TIB (Tanzania Investement Bank).
SWALI: Ni matukio gani ya bahati uliyowahi kukutana nayo katika maisha yako?
JIBU: Kushinda taji la mrembo wa Afrika Mashariki. Ni kitu ambacho sikukitarajia. Kimenifurahisha sana na mpaka hapa nilipo, bado siamini. Ni kama vile bado nipo kwenye mshtuko.
SWALI: Ni tukio gani lililowahi kukuhuzunisha sana katika maisha yako?
JIBU: Kusema ukweli, huwa natokewa na vitu vingi sana, lakini mara nyingi huwa naviacha vipite, sina kawaida ya kuweka kitu rohoni kwangu. Huwa siyapi uzito mambo ya aina hiyi katika maisha yangu. Na yakishapita, nasahau.
SWALI: Unapendelea michezo ya aina gani?
JIBU: Soka na mpira wa kikapu. Nilipokuwa sekondari, nilikuwa nacheza mpira wa kikapu. Nilikuwepo kwenye timu ya shule, lakini nilipokwenda chuo, sijui ikawaje, kazi zilizidi ikabidi niache. Mchezo wa soka napenda kuutazama. Katika ligi ya England, mimi ni shabiki wa Arsenal. Katika ligi ya nyumbani, nafuatilia kidogo lakini sio sana.
SWALI: Unapenda kupika na kula chakula cha aina gani?
JIBU: Napenda sana kula chips na mayai. Pia napenda vyakula vya kiasili kama vile mtori na ndizi. Si unajua sisi wachaga. Pia napenda kula chapati na pilau.
SWALI: Katika siku zijazo, unaweza kufikiria kushiriki kwenye mashindano ya Miss Tanzania? Au unahisi utakuwa umejishusha?
JIBU: Hapana. Sio kwamba nitakuwa nimejishusha, bali hata kushiriki kwenye shindano hili niliamua iwe ni mara moja tu. Kuna vitu vingi ambavyo nimepanga kuvifanya, hivyo sidhani kama nitakuwa na muda tena wa kufanya hivyo.
SWALI: Unapenda kutoa mwito gani kwa wasichana, ambao wangependa kushiriki kwenye mashindano haya, lakini wanaogopa?
JIBU: Napenda kuwaambia kwamba, kushiriki kwenye mashindano haya sio kitu kibaya. Inategemea na mtu mwenyewe alivyo. Kama unajiamini na kujiona unaweza kufanya vizuri, huna sababu ya kuogoa. Kushiriki kwenye mashindano haya kamwe sio uhuni. Wapo warembo wengi walionufaika kutokana na mashindano haya. Huwezi kuonekana mtu tofauti kwa kushiriki kwenye mashindano haya. kama unataka kufanya kitu, fanya.
'
Tuesday, January 15, 2013
Saturday, January 12, 2013
YANGA YAPIGWA MBILI KAVU NA WAHOLANZI
Yanga jana ilipoteza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi baada ya kufungwa kwa mabo 2-0 katika mchezo uliofanyika katika mji wa Bereke kwenye viwanja vya Arcuda foootball Antalya.
Yanga ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za kufunga lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake Nizar Khalfani, George Banda na Saimon Msuva kuliinyima Yanga kupata bao katika dakika 15 za kwanza.
Dakika ya 23 Saimon Msuva alishindwa kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia pasi safi nzuri ya Nizar Khalfani ambapo Msuva aliupiga mpira na kuokukolewa na mlinda mlango wa timu ya Emmen FC.
George Banda ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati akisaidiana na Nizar Khalfani alishindwa pia kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima akitokea upande wa kushoto wa uwanja.
Mlinda mlango wa Yanga Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya hatari langoni mwake baada ya washambuliaji wa Emmen kugongeana vizuri na kuwatoka walinzi wa Yanga lakini mashuti yao walikuta yakiishia mikononi mwake.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zilipomalizika, hakuna timu iliyoweza kupata bao. Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kikosi chote ambapo waliingia, Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladslaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Godfrey Taita, Omgea Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na David Luhende.
Yanga ilianza tena mchezo kwa utulivu huku ikipanga mbinu za kuweza kupata bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Emmen Fc ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga kuweza kuipita ngome hiyo.
Emmen FC waliitawala zaidi sehemu ya kiungo hali iliyopelekea kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga, na katika dakika ya 73 waliweza kujipatia bao la kwanza baada ya mfungaji kumalizia krosi iliyowapita walinzi wa Yanga.
Dakika nne (4) baadae, Emmen FC walijiapati bao la pili ikiwa ni dakika ya 77 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa Emmen FC kumponyoka mlinda mlango Yusuph Abdul na kugonga mwamba wa juu kabla ya mshambuliaji wa Emmen FC haujaukwmishwa wavuni na kuhesabu bao la pili.
Jerson Tegete aliumia dakika ya 79 katika harakati za kfunga na nafasi yake kuchukuliwa na Rehani Kibingu laikini mabadiliko hayo hayakuisadia Yanga kubadilisha matokeo.
Mara baada ya mchezo kocha mkuu Ernest Brandts alisema amesikitishwa na matokeo hayo; "timu yangu ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kuwabana vizuri wapinzani wetu lakini kipindi cha pili umakini ulikosekana hali iliyopelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka,"alisema.
"Makosa yaliyojitokeza katika kipindi cha pili tumeyaona kwa pamoja na benchi zima la ufundi hivyo tutayafanyia kazi yasijitokeze tena katika michezo itakayofuata," alisema 'Brandts' .
Yanga kesho itafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kabla ya kuanza kujiandaa na safari ya nchini Tanzania siku ya Jumapili mchana ambapo itarajiwa kufika Dar es salaam majira ya saa 10 kasoro ikiwa ni siku ya Jumatatu alfajiri.
Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza: Said Mohamed, Juma Abdul, Stephano Mwasika, Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge Banda, Nizar Khalfani, Haruna Niyonzima
Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji, Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende.

AZAM, TUSKER KAZI IPO LEO
TUSKER ya Kenya juzi ilifuzu kucheza fainali ya michuano ya soka ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Miembeni ya Zanzibar mabao 2-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa.
Kwa ushindi huo, Tusker sasa itakutana na Azam katika mechi ya fainali itakayopigwa leo kwenye uwanja huo. Azam ilifuzu kucheza fainali baada ya kuichapa Simba kwa penalti 5-4.
Pamoja na timu zote mbili kucheza kwa kushambulia katika kipindi cha kwanza kwa lengo la kupata mabao, hadi mapumziko hakuna iliyoweza kupata bao.
Tusker ilibadili staili ya mchezo katika kipindi cha pili na kufanikiwa kufunga mabao mawili dakika ya 52 na 72 kupitia kwa Luke Ochieng na Jesse Were.
Wakati huo huo, Kocha Msaidizi wa Azam, Kalimagonga Ongara ametamba kuwa, wana kila sababu ya kuifunga Tusker leo na kutwaa Kombe la Mapinduzi.
Ongara alisema mjini hapa juzi kuwa, japokuwa Tusker ni timu iliyokamilika katika kila idara, vijana wake wana ari kubwa ya kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo.
Hata hivyo, Ongara alikiri kuwa pambano hilo litakuwa gumu kwa sababu wapinzani wao ni timu nzuri na wanacheza kwa ushirikiano mkubwa.
“Itakuwa mechi ngumu kwa sababu Tusker ni wazuri, lakini hata sisi timu yetu ni nzuri, hivyo tutapigana kiume kuhakikisha tunashinda na kutwaa ubingwa,"alisema.

URAIS TFF SH. 500,000, FOMU KUANZA KUTOLEWA J'TATU
SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limesema, fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu, zitaanza kutolewa Jumatatu.
Taarifa iliyotolewa na TFF kwa vyombo vya habari jana ilisema kuwa, fomu hizo zinapatikana kwenye ofisi ya katibu mkuu wa shirikisho hilo kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa10 jioni na mwisho wa kuzirejesha ni Januari 18 mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni ya rais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji, ambapo nafasi zitakazogombewa ni 13.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa, ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi ya urais ni sh. 500,000, wagombea wa nafasi ya makamu wa rais sh. 300,000 na wagombea wa nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji sh. 200,000.
Imezitaja sifa za wagombea kuwa ni wawe raia wa Tanzania, kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne, uzoefu wa uendeshaji wa soka, wasiwena hatia ya makosa ya jinai, umri uziopungua miaka 25,wawe wamewahi kucheza soka, makocha, waamuzi au kuendesha soka katika ngazi zozote.
Taarifa hiyo ilizitaja sifa za wagombea wa nafasiya rais na makamu wake kuwa ni kuwa na shahada ya chuo kikuu na uwezo wa kuwakilisha TFFndani na nje ya nje.
Wakati huo huo, fomu za kuwania uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopangwa kufanyika Februari 22 mwaka huu, zitaanza kutolewa Jumatatu.
Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni ya mwenyekiti wa bodi, makamu mwenyekiti, wajumbe wawili wa kuziwakilisha klabu za ligi daraja la kwanza kwenye kamatiya uongozi.
Ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti ni sh. 200,000 wakati wagombea wa nafasi za ujumbe watalipa sh. 100,000.

Friday, January 11, 2013
TRA YAIDAI YANGA MIL. 203 ZA PAYE, SIMBA MIL 50.7
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imesema inazidai klabu za Simba na Yanga jumla ya sh. milioni 253.7 kutokana na kukwepa kulipa kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE).
Kiasi hicho cha fedha ni makato ya PAYE kwa ajili ya wachezaji wa kigeni waliosajiliwa na klabu hizo mbili kwa nyakati tofauti, na ambao kwa muda mrefu walikuwa hawakatwi kodi kulingana na sheria za kodi nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Elimu kwa Walipakodi wa TRA, Hamis Lupenja alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, mamlaka hiyo inaidai Yanga sh. milioni 203 na tayari imekwishafunga akaunti yake ya benki ya CRDB.
Lupenja alisema Simba inadaiwa sh. milioni 50.7, lakini akaunti ya klabu hiyo bado haijafungwa na wametoa muda kwa viongozi wake kulipa deni hilo kabla ya hatua ya kufungiwa kuchukuliwa.
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema TRA imekuwa ikizikumbusha mara kwa mara klabu hizo kongwe nchini kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ikiwa ni pamoja na kutoa elimu.
Alisema hatua ya kuzifungia klabu inakuja baada ya klabu kushindwa kutekeleza wajibu wake na kuongeza kuwa, iwapo klabu hizo zitashindwa kulipa fedha hizo, hatua itakayofuata ni kukamata mali za klabu.
Lupenja alisema zoezi hilo halitaishia kwa klabu za Simba na Yanga, badala yake litafanyika kwa zote, ambazo zimewahi kusajili wachezaji wa kigeni.
"Unajua kwa muda mrefu klabu zetu zimekuwa zikileta wachezaji wa kigeni, lakini hawakatwi kodi na deni linakuwa kubwa, hivyo kwa sasa tumeamua kufuatilia kwa kina na tulianza na baba yao Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na sasa watoto ambao ni klabu," alisema Lupenja.
Alisema lengo la TRA siyo kudidimiza michezo, bali ni kutekeleza wajibu wa kukumbusha watu wote umuhimu wa kulipa kodi.
Mwishoni mwa mwaka jana, TRA ilifunga akaunti ya TFF baada ya shirikisho hilo kudaiwa sh. milioni 157,407.968 zilizotokana na malimbikizo ya PAYE za makocha wa kigeni wa timu za Taifa.
Hata hivyo, akaunti hiyo ilifunguliwa baada ya mazungumzo kati ya TRA, TFF na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa vile fedha hizo zimetolewa na wadhamini, Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom kwa ajili ya klabu za ligi kuu.
Alipoulizwa kuhusu hatua, ambazo Yanga imechukua baada ya akaunti yao kufungwa, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrence Mwalusako alikiri kuwa ni kweli akaunti hiyo imefungwa na wameathirika.
Mwalusako alisema akaunti hiyo ndiyo inayopokea fedha za malipo ya kadi za wanachama kabla ya kushiriki katika mkutano mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Januari 19 mwaka huu.
Hata hivyo, Mwalusako alisema uongozi wa klabu yake unaendelea kulishughulikia suala hilo na huenda likatatuliwa hivi karibuni. Hakuwa tayari kutaja hatua wanazotarajia kuchukua.
Viongozi wa Simba hawakuweza kupatikana jana kuzungumzia suala hilo kwa vile kila walipopigiwa simu, hawakuwa tayari kuzipikea.

Thursday, January 10, 2013
SAMATTA: NITAIFANYIA MAKUBWA TAIFA STARS
MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, amesema amepanga kuifanyia mambo makubwa timu ya taifa, Taifa Stars.
Samatta alisema hayo mjini Dar es Salaam juzi, muda mfupi kabla ya Taifa Stars kwenda Ethiopia kwa ziara ya mechi moja ya kirafiki.
Mshambuliaji huyo, ambaye amekuwa akishutumiwa kwa kucheza chini ya kiwango anapoichezea Taifa Stars, alisema si kweli kwamba hana uzalendo kwa timu yake ya taifa.
"Habari hizi zinanikera sana. Hivi mimi ningejulikana vipi na TP Mazembe kama sio Taifa Stars na Simba? Wangeniona wapi? Mimi nitaendelea kuichezea timu yangu ya Taifa kwa mapenzi yote ili niwazibe midomo wabaya wangu,"alisema mchezaji huyo.
Alisema yupo tayari kuichezea Taifa Stars wakati wowote atakapoitwa na Kocha Kim Poulsen kwa sababu moja ya sifa za mwanasoka wa kimataifa ni kufanya vizuri katika timu yake ya taifa.
Samatta alisema moja ya ndoto zake ni kuifungia Taifa Stars mabao mengi katika michuano ya kimataifa na pia kuiwezesha kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014 zitakazofanyika nchini Brazil.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za African Lyon na Simba alisema, kwa sasa yupo fiti baada ya kupona na kusisitiza kuwa, ataanza kuonyesha makali yake leo katika pambano kati ya Taifa Stars na Ethiopia litakalofanyika mjini Addis Ababa.
"Kwa kweli najisikia faraja kubwa leo hii kusafiri na wachezaji wenzangu wa nchi yangu,nina imani mwaka huu nitafanya mengi makubwa, ikiwa ni pamoja na kufunga mabao kwa kushirikiana na wenzangu. Na hilo nitalifanya hata kwa klabu yangu ya TP Mazembe,"alisema nyota huyo.
Samatta alikiri kuwa, kwa sasa anakabiliwa na kibarua kizito cha kupata namba ya kudumu kwenye klabu yake ya TP Mazembe kutokana na kuwepo kwa wachezaji wengi nyota kutoka katika nchi mbalimbali.

WENGINE TISA SIMBA KWENDA OMAN KESHO
KUNDI la pili la wachezaji tisa wa klabu ya Simba linatarajiwa kuondoka nchini leo kwenda Oman kwa ajili ya kambi ya wiki mbili.
Wachezaji hao wanaondoka leo baada ya wengine wanane kuondoka nchini juzi kwenda Oman kwa ajili ya kambi hiyo ya mazoezi.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kiwhelo 'Julio' alisema jana kuwa, kundi hilo la pili la wachezaji linatarajiwa kuondoka saa 10:00 jioni kwa ndege ya Shirika la Emirates.
Julio alisema wameamua kuondoka leo badala ya Jumapili baada ya timu hiyo kutolewa mapema katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kufungwa kwa penalti 5-4 na Azam.
Aliwataja wachezaji watakaoondoka leo kuwa ni William Mweta, Miraj Adam, Paul Ngalema, Hassan Isihaka, Komabil Keita, Jonas Mkude, Ramadhani Singano, Abdallah Seseme na Said Demla.
Julio alisema anaamini kuwa, kambi ya Oman itazidi kuiimarisha timu yake ili iweze kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara na mashindano ya klabu bingwa Afrika.
Kocha huyo alisema ushiriki wao katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi umewasaidia kujenga kikosi imara na pia kuwapa uzoefu zaidi wachezaji waliopandishwa kutoka kikosi cha pili.
"Tumepata mazoezi mazuri katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi na sasa tunaelekeza nguvu katika kambi ya Oman ili tuweze kujiimarisha na kuongeza viwango vya wachezaji wetu," alisema Julio.
Mshindi kati ya Simba na Azam ilibidi apatikane kwa njia ya penalti tano tano baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya bao 2-2. Katika mechi hiyo, Simba ilitumia wachezaji wa kikosi chake cha pili.

MWANARIADHA WA KENYA AFANYIWA KITU MBAYA BRAZIL
SAO PAULO, Brazil MWANARIADHA Edwin Rotich wa Kenya juzi alifanyiwa kitu mbaya baada ya kuvamiwa na mtu anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili wakati alipokuwa akishiriki katika mbio za kimataifa za kilometa 10 nchini Brazil.
Rotich alikumbwa na mkasa huo wakati alipokuwa akiongoza mbio hizo na kubakiza kilometa chache kabla ya kumaliza.
Mtu huyo, aliyetajwa kwa jina la Wallace de Sousa (33) alimvamia Rotich kwa lengo la kumwangusha, lakini mwanariadha huyo alipambana naye kiume na kufanikiwa kujinasua.
Wakati Wallace alipokuwa akitaka kumvamia Rotich kwa mara ya pili, polisi watatu waliokuwa kwenye pikipiki walifanikiwa kumuokoa na kumtia mbaroni mtu huyo.
Kwa mujibu wa polisi wa Brazil, tukio hilo lilitokea katika mtaa wa Cuiaba, ambapo Wallace alikuwa miongoni mwa watazamaji waliokuwa wakiwashuhudia washiriki wa mbio hizo wakichuana.
Pamoja na kukumbwa na mkasa huo, Rotich alifanikiwa kumaliza mbio hizo akiwa wa kwanza na kushangiliwa na umati mkubwa wa mashabiki.
Hii ni mara ya pili kwa Rotich kushinda mashindano ya riadha nchini Brazil. Wiki iliyopita, mwanariadha huyo wa kimataifa wa Kenya aliibuka mshindi katika mbio za kimataifa za Sao Silvestre Race zilizofanyika mjini Sao Paulo.
Katika mbio za juzi, Mark Korir wa Kenya alishika nafasi ya pili, akifuatiwa na Daniel da Silva wa Brazil. Polisi wamesema Wallace na historia ya matatizo ya akili na kwamba hiyo haikuwa mara ya kwanza kujihusisha na matukio ya aina hiyo.

MGOSI AANZA KIBARUA JKT RUVU
MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa klabu ya Simba na timu ya Taifa, Taifa Stars, Musa Hassan 'Mgosi' ameanza rasmi mazoezi na timu yake mpya ya JKT Ruvu.
Mgosi, ambaye alirejea nchini hivi karibuni akitokea China, alikokwenda kucheza soka ya kulipwa, alianza mazoezi hayo jana kwenye uwanja wa Mlalakuwa, Dar es Salaam.
Kocha Mkuu wa JKT Ruvu, Charles Kilinda alisema jana kuwa, wanatarajia kuanza rasmi kumtumia Mgosi katika mechi za mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara, unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Kilinda alisema Mgosi alikwenda China kwa ajili ya michuano maalumu, iliyowashirikisha wachezaji kutoka nchi za Afrika, ambapo aliongoza kwa kufunga mabao.
Mgosi alisajiliwa na JKT Ruvu kabla ya kuanza kwa ligi, lakini alishindwa kuichezea katika mzunguko wa kwanza kutokana na kukosa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) kutoka DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Kwa mujibu wa Kilinda, ujio wa Mgosi utazidi kukiimarisha kikosi chake kutokana na uzoefu wake wa michuano mbalimbali na pia umahiri wa kupachika mabao.
"Tumeshapata uhamisho wake kutoka DRC na sasa Mgosi ataanza kuvaa jezi za JKT Ruvu katika mzunguko wa pili,"alisema kocha huyo, ambaye aliwahi kuichezea Yanga miaka ya 1980.

SIMKOKO ATIMULIWA POLISI MORO
NA DEUSDEDIT UNDOLE
UONGOZI wa timu ya soka ya Polisi ya Morogoro umeamua kuvunja mkataba kati yake na Kocha John Simkoko.
Ofisa Habari wa Polisi Morogoro, Clement Bazo alisema kwa njia ya simu jana kutoka Morogoro kuwa, nafasi ya Simkoko sasa imechukuliwa na Kocha Mohammed Rishard Adolph.
Bazo alisema wameamua kuvunja mkataba na Simkoko kutokana na mwenendo mbaya wa timu hiyo katika mechi za mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Alisema wanaamini ujio wa Adolph, atakayekuwa akisaidiwa na Boniface Njohole, utakiimarisha zaidi kikosi hicho kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo, unaotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu.
Kwa mujibu wa Bazo, Adolph ambaye alikuwa kocha msaidizi wa timu za taifa za vijana na timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, imeingia mkataba wa kuifundisha Polisi Morogoro kwa miezi sita.
Polisi Morogoro ilimaliza mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ikiwa ya mwisho baada ya kuambulia pointi nne katika mechi 13. Ilipata pointi hizo kutokana na kutoka sare katika mechi nne.
Bazo alisema pia kuwa, katika kujiimarisha zaidi, timu hiyo imeamua kumsajili kwa mkopo mshambuliaji Salum Machaku kutoka Simba.
Pamoja na kukatisha mkataba wa Simkoko, Bazo alisema wamepanga kumpa kocha huyo kazi ya kuwa mshauri wa masuala ya kiufundi.
Wakati huo huo, Bazo amesema Polisi Morogoro inatarajia kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu.

TAIFA STARS KUIVAA ETHIOPIA KESHO
KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa, 'Taifa Stars' kinashuka dimbani leo kumenyana na Ethiopia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa, Ethiopia.
Taifa Stars itautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za 2014 dhidi ya Morocco, itakayopigwa Machi 22 mwaka huu.
Kwa upande wa Ethiopia, itautumia mchezo huo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya michuano ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, zinazotarajiwa kuanza Januari 19 mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika.
Wambura alisema Taifa Stars ilitarajia kufanya mazoezi yake ya mwisho jana jioni katika Uwanja wa Taifa wa Addis Ababa kwa saa moja kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo na kuongeza kuwa, wachezaji wote wapo katika hali nzuri.
Kwa mujibu wa Wambura, ripoti ya Kocha Mkuu wa timu hiyo, Kim Poulsen imeeleza kuwa, timu ipo katika hali nzuri na inatarajia kufanya vyema katika mchezo huo.
Wambura alimkariri Poulsen akisema kuwa, ushindi kwa timu yake utawafanya wachezaji wajiamini zaidi baada ya mwezi uliopita kuwafunga mabingwa wa Afrika, Zambia bao 1-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, Taifa Stars itawakosa Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva na Nadir Haroub ‘Canavaro’, ambao wapo na kikosi cha Yanga nchini Ututruki. Pia itamkosa kipa Mwadini Ally, aliyebaki na timu yake ya Azam visiwani Zanzibar na mshambuliaji, John Bocco aliyefanyiwa upasuaji wa goti nchini India.
Wachezaji waliokwenda na Taifa Stars nchini Ethiopia ni makipa Juma Kaseja (Simba), ambaye ndiye nahodha na Aishi Manula (Azam FC). Mabeki ni Aggrey Morris, Issa Rashid, Erasto Nyoni (Azam), Amir Maftah na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar, Khamis Mcha (Azam), Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar) wakati washambuliaji ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo- DRC) na Mrisho Ngasa (Simba).

MKUTANO YANGA SASA JAN 20
UONGOZI wa klabu ya Yanga umeamua kusogeza mbele kwa siku moja tarehe ya mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo, uliopangwa kufanyika Januari 19 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, mkutano huo sasa utafanyika Januari 20 mwaka huu.
Mwalusako alisema wameamua kusogeza mbele tarehe ya mkutano huo ili kutoa nafasi kwa wanachama kufanya maandalizi, ikiwa ni pamoja na kulipia kadi zao.
Alisema uamuzi huo umefanyika baada ya uongozi kubaini kuwa, baadhi ya wanachama watashindwa kuhudhuria mkutano huo iwapo utafanyika siku ya Jumamosi kwa vile watakuwa kazini.
Katibu Mkuu huyo wa Yanga alisema, siku ya Jumapili ni nzuri zaidi kwa wanachama kufika mkutanoni kwa vile ni siku ya mapumziko kikazi.
Amewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kulipia kadi zao za uanachama ili waweze kuwa na haki ya kushiriki katika mkutano huo, ambao alisema utajadili mambo mengi muhimu.

NYOTA MPYA AZAM WE ACHA TU-ONGARA
KLABU ya Azam imejigamba kuwa, nyota wake wapya waliosajiliwa kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara, wametoa mchango mkubwa kwa timu hiyo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Kalimagonga Ongara ameieleza tovuti ya Azam jana kuwa, huo ni mwanzo mzuri kwa wachezaji hao kutokana na kumudu vyema nafasi wanazocheza.
Wachezaji wapya waliosajiliwa na Azam wakati wa usajili wa dirisha dogo ni Brian Umony kutoka Uganda, Jockins Atudo na Humphrey Mieno kutoka Kenya, David Mwantika kutoka Prisons, Seif Abdallah kutoka JKT Oljoro na Uhuru Selemani kutoka Simba.
"Wachezaji hawa wameonyesha umahiri mkubwa wa kucheza soka na hii ni ishara nzuri kwa Azam kwamba itakuwa tishio zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu,"alisema.
Ongara alisema anaamini kadri siku zinavyokwenda mbele, wachezaji hao wapya watazidi kuelewana vyema na wenzao wa zamani na kuifanya Azam itimize malengo yake ya kutwaa ubingwa wa bara.

BRANDTS: YANGA SASA INATISHA
Na BARAKA KAZIGUTO, ANTALYA
KOCHA Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts ametamba kuwa, timu yake kwa sasa iko imara kutokana na wachezaji kuelewa na kufuata vyema mafundisho yake.
Brandts alitoa majigambo hayo juzi licha ya Yanga kuchapwa mabao 2-1 na timu ya Denizlispor FC ya Uturuki katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye viwanja vya Kamelya Complex mjini hapa.
"Timu yangu imecheza vizuri, nadhani wote tulikuwa mashuhuda jinsi vijana wangu walivyoonyesha soka ya kuvutia iliyowashangaza watazamaji,"alisema kocha huyo.
Brandts alikiri kuwa, hakupendezwa na matokeo ya mchezo huo na alimtupia lawama mwamuzi kwa madai kuwa alishindwa kulimudu vyema pambano hilo kutokana na kutoa maamuzi ya kutatanisha.
Mechi hiyo ilikuwa ya pili kwa Yanga tangu ilipowasili Uturuki na kuweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara.
Katika mechi yake ya kwanza, Yanga ilitoka sare ya bao 1-1 na timu ya daraja la nne ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani.
Katika mechi ya juzi, Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wake, Jerry Tegete aliyemalizia gonga safi kati ya Haruna Niyonzima na Athumani Iddi 'Chuji'.
Denizlispor ilisawazisha dakika ya 78 kabla ya kuongeza bao la pili dakika ya 88 kwa njia ya penalti baada ya beki Nadir Haroub 'Cannavaro' kumchezea rafu mshambuliaji mmoja wa timu hiyo.
Yanga iliwakilishwa na Ally Mustafa 'Barthez', Juma Abdul, Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani/Mbuyu Twite, Athumani Idd 'Chuji, Saimon Msuva/Oscar Joshua, Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Didier Kavumbagu,Jerson Tegete/Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima.

Tuesday, January 8, 2013
SIMBA YAENDA OMAN KWA MAFUNGU
TIMU ya soka ya Simba inatarajiwa kuondoka nchini leo jioni kwenda Oman kwa ajili ya kuweka kambi ya wiki mbili ya kujiandaa kwa mzunguko wa pili wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara.
Habari kutoka ndani ya klabu hiyo zilieleza jana kuwa, kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuondoka saa 10 jioni kwa ndege ya Shirika la Emirates.
Hata hivyo, habari hizo zimeeleza kuwa, Simba itakwenda Oman kwa mafungu, kufuatia baadhi ya wachezaji wake kuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars na wengine kwenye kikosi kinachoshiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Chanzo cha habari kimeeleza kuwa, kikosi kitakachoondoka leo kitaongozwa na Kocha Msaidizi, Jamhuri Kihwelu.
Hata hivyo, haikuweza kufahamika ni wachezaji wangapi watakaoondoka leo kwa vile uamuzi wa mwisho ulitarajiwa kutolewa jana jioni na Kocha Mkuu, Patrick Liewig.
Wachezaji wa Simba walioko kwenye kikosi cha Taifa Stars, kitakachoondoka leo kwenda Ethiopia ni Juma Kaseja, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Amri Kiemba,
Mwinyi Kazimoto na Mrisho Ngasa.
Wachezaji hao wanatarajiwa kwenda Oman wakitokea Ethiopia, ambako Taifa Stars itacheza na timu ya taifa ya nchi hiyo, katika mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayopigwa keshokutwa mjini Addis Ababa.
Mmoja wa viongozi wa Simba alisema wachezaji wengine wa timu hiyo walioko Zanzibar, wanatarajiwa kuondoka nchini Jumapili wakiongozana na Kocha Leiwig.
Simba inatarajiwa kushuka dimbani kesho kumenyana na Azam katika mechi ya pili ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Amaan. Kikosi kitakachocheza mechi hiyo kinaundwa na wachezaji wengi waliopandishwa daraja kutoka kikosi cha pili.
EL-MAAMRY AMTOLEA UVIVU ISSA HAYATOU
MJUMBE wa heshima wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), Said Hamad El-Maamry ameamua kumtolea uvivu rais wa sasa wa shirikisho hilo, Issa Hayatou kwa kusema kuwa wakati wake wa kuwa kiongozi wa taasisi hiyo umefikia kikomo.
El-Maamry, ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) amesema, Hayatou anapaswa kumuachia mtu mwingine kuliongoza shirikisho hilo.
Kauli hiyo ya El-Maamry imekuja baada ya Hayatou kupitishwa kuwa mgombea pekee wa urais wa CAF katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo uliopangwa kufanyika mwaka 2014 nchini Morocco.
Akizungumza katika kipindi cha Nyumba ya Jirani kilichorushwa hewani na kituo cha televisheni cha TBC 1 juzi, El- Maamry alisema uamuzi wa Hayatou kugombea tena nafasi hiyo unadhihirisha kwamba, ameamua kuigeuza taasisi hiyo kuwa ya kisultani.
Hayatou alichaguliwa kuwa rais wa CAF kwa mara ya kwanza mwaka 1988 na amekuwa rais wa shirikisho hilo kwa miaka 25 mfululizo. Iwapo atachaguliwa tena katika uchaguzi wa mwaka 2014, atakuwa ameweka rekodi ya kuliongoza shirikisho hilo kwa miaka 29.
El-Maamry alisema kutokana na marekebisho ya katiba ya CAF yaliyofanyika mwaka jana, ni vigumu kwa Hayatou kuondoka madarakani, vinginevyo lazima liwepo shirikisho la kumtaka afanye hivyo kutoka kwa nchi wanachama.
"Kwa mujibu wa marekebisho hayo ya katiba, mgombea urais wa CAF lazima awe mjumbe wa kamati ya utendaji. Na kwa wajumbe 12 wanaounda kamati hiyo hivi sasa, sioni mwenye uwezo wa kuwa rais wa CAF," alisema El-Maamry, ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa kilichokuwa Chama cha Soka nchini (FAT) na pia mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Hata hivyo, El-Maamry alikiri kuwa, Hayatou amefanya mambo mengi mazuri na makubwa katika kuendeleza soka barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa wadhamini wengi katika mashindano mbalimbali.
"Kusema kweli kwa hilo anastahili sifa, tumpe heko, lakini kwa sasa umri umemtupa mkono, aachie ngazi, amwachie nafasi mtu mwingine na kama anaweza, amwandae mtu wa kuchukua nafasi yake. Tunahitaji mtu mpya kama alivyokuwa yeye wakati alipochukua madaraka mwaka 1988,"alisema El-Maamry, ambaye kitaaluma ni mwanasheria.
El-Maamry alisema moja ya mambo anayotarajia kuyafanya iwapo atakutana na Hayatou, ni kumshauri asigombee tena urais wa CAF iwapo atashinda uchaguzi wa mwaka 2014 kwa vile kufanya hivyo ni kudumaza maendeleo ya soka barani Afrika.
Mjumbe huyo wa heshima wa CAF alisema moja ya sababu zinamfanya Hayatou asiwe na mpinzani katika nafasi hiyo ni kukosekana kwa umoja na mshikamano miongoni mwa nchi wanachama.
Alisema kwa sasa, nchi wanachama wa CAF zimejitenga kutokana na ukanda, lakini iwapo zitaamua kuungana, itakuwa rahisi kumuondoa Hayatou madarakani na kumweka kiongozi mpya kutoka nchi zingine.
"Kama CECAFA itaungana na COSAFA (Shirikisho la Soka Kusini mwa Afrika) na nchi zingine za magharibi zinazozungumza kiingereza kama vile Nigeria, Ghana, Sierra Leone na zinginezo, itakuwa rahisi kumaliza usultani wa Hayatou,"alisema kiongozi huyo wa zamani wa soka nchini.
Alimpigia chapuo Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kuwa ndiye pekee anayefaa kurithi mikoba ya Hayatou kwa sasa kwa vile anakubalika miongoni mwa nchi nyingi wanachama wa CAF.
Monday, January 7, 2013
TAFF YATOA ONYO KWA WASANII
Na Elizabeth John SHIRIKISHO la Filamu Tanzania (TAFF) limekemea baadhi ya wasanii walioonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa aliyekuwa msanii wa filamu nchini, Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
Pia limesisitiza kuwa msanii atakaYeripotiwa katika vyombo vya habari kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu atafungiwa kuigiza.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba alisema amesikitishwa na kitendo cha wasanii kuacha msiba na kwenda kunywa pombe wakati msiba huo ni wa dini.
Alisema baadhi ya wasanii kuonyesha utovu wa nidhamu katika msiba wa marehemu Kanumba na wengine katika msiba wa Sajuki.
“Nasikitika kuona msanii hajitambui hata kidogo, yaani anaacha msiba anakwenda kunywa pombe tena jirani na mahala pa msiba, jamani huu msiba ni wa dini, hivyo atakayeripotiwa vibaya katika misiba, TAFF tutamfungia” alisema Mwakifwamba.
Katika hatua nyingine, Mwakifwamba alisema msiba huo ulitawaliwa na utani hali ya kwamba umewakutanisha watani wa makabila.
Msiba huo ulitawaliwa na utani baada ya kuwepo kwa wasanii wachekeshaji kama vile, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya fedha, Lucas Mhuvile ‘Joti’ na wengineo wengi.
Wakati huo huo, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imewataka wasanii nchini kujitokeza kushiriki tamasha la sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambalo litafanyika nchini Rwanda mwezi ujao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, kwa Niaba ya Katibu Mkuu, Ofisa Utamaduni Mwandamizi wa Wizara hiyo makao makuu, Habibu Mohamed amesema tamasha hilo lijulikanalo kama JAMAFEST litafanyika kwa siku nane kuanzia Februari 9 hadi 16 mwaka huu.
“ Kwanza napenda kuwajulisha kuwa tumepata mwaliko wa kushiriki Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki, ‘JAMAFEST – 2013’ ambalo ni tamasha muhimu sana kwa wasanii wetu kushiriki katika hatua ya kutangaza na kuuza kazi zao katika soko la sanaa la Afrika Mashairiki,” amesema Habibu.
Amesema kutokana na mwaliko huo wa Jumuiya, Wizara inatoa mwaliko kwa wasanii, asasi, vikundi, wabunifu wa mavazi na kampuni kwa hapa nchini, ambao zitaweza kufanya maonesho na kuuza bidhaa na huduma za Sanaa na Utamaduni, katika mabanda ya Tanzania kutuma maombi yao wizarani ambapo mwisho wa kutuma maombi ni Januari 25. Amesema washiriki watajigharamia nauli ya kwenda na kurudi, chakula na malazi katika kushiriki tamasha hilo.

YANGA KUKIPIGA NA WATURUKI KESHO
TIMU ya soka ya Yanga kesho inashuka tena dimbani kukipiga na timu ya Denizlispor FC ya Uturuki, inayoshiriki michuano ya ligi daraja la kwanza katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika katika uwanja wa Selen Football -Kalimya Complex pembeni kidogo ya mji wa Antlaya.
Yanga, ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya, itautumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu hiyo, ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka jana na hivi sasa inapambana kurudi tena katika ligi kuu ya Uturuki.
Kocha Mkuu wa Yanga, Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC, ambayo inaundwa na wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakuwa mchezo safi na wa kuwavutia.
"Baada ya kuwa na wiki moja ya mazoezi na mechi moja ya kirafiki dhidi ya Armini Bielefeld ya Ujerumani mwishoni mwa wiki iliyopita, hii itakuwa fursa nyingine nzuri ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu nyingine, hii itanisadia kuona maendeleo ya kikosi changu kutokana na mazoezi ambayo tumekuwa tukiyafanya tangu tulipofika hapa," alisema Brandts.
Denizlispor FC ni miongoni mwa timu zaidi ya 200 kutoka sehemu tofauti duniani, ambazo zimeweka kambi katika mji wa Antlaya kwa ajili ya maandilizi ya mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza nchini Uturuki.
Mchezaji wa zamani wa Leicester City ya Uingereza, Dundee United ya Scotland na Ivernes ya Uholanzi, mtanzania mzaliwa wa Uingereza, Eric Odhiambo ni miongoni mwa washambuliaji wa kutegemewa wa timu ya Denizlispor FC.
Kikosi cha wachezaji 27 wa Yanga waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna majeruhi hata mmoja, hali itakayomfanya Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Athumani Idd 'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizuri kwani wanaendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini Antalya.
Kuhusu hali ya hewa ya leo, haijaonekana kuwa tatizo kwa wachezaji kwani wanaonekana kuimudu na muda mwingi kwa sasa kumekuwa na jua linalowaka kuanzia asubuhu wakati wa mazoezi mpaka mida ya jioni. Kwa leo hali ya hewa ni nyuzi joto 17 - 21, hivyoni nzuri na jua linawaka muda wote.
Sunday, January 6, 2013
YANGA YATOKA SARE NA WAJERUMANI
Timu ya Young Africans Sports Club imetoka sare ya bao 1-1 dhidi ya timu ya Arminia Bielefeld ya Ujerumani katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni katika uwanja wa Adora Football pemebni kidogo ya mji wa Antalya.
Armini Bielefeld ilianza soka kwa kasi kwa lengo la kujipatia bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Yanga na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' ilikuwa kikwazo kwao kwani mashambulizi yao yaliishia mikononi mwake.
Ikiwa ni mchezo wake wa kwanza wa kujipima nguvu Young African iliweza kuonyesha soka safi katika kipindi cha kwanza hali iliyowashangaza wajerumani hao na kipindi cha pili kuamua kufanya mabadiliko ya kikosi kizima.
Viungo wa Yanga Frank Domayo, Haruna Niyonzima na Kabange Twite waliweza kutawala mchezo kwa dakika 45 zote za kipindi cha kwanza huku baadhi ya wajerumani waliokuwa wakishuhudia mchezo huo kushangazwa na kiwango cha timu ya Yanga. Hadi mapumziko timu zote zilikuwa hazijafungana.
Kipindi cha pili Arminia Bielefeld iliamua kubadilisha kikosi chake chote cha wachezaji kwa lengo la kuingiza nguvu mpya ili waweze kuikabili kasi ya wachezaji wa Yanga ambao walionekana kuwa imara na bora zaidi.
Dakika ya 55 Yanga ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa Said Bahanuzi na David Luhende na nafasi zao kuchukuliwa na Jerson Tegete na Saimon Msuva.
Jerson Tegete aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 60 ya mchezo, akiunganisha pasi safi aliypewa na Saimon Msuva aliyewatoka walinzi wa Arminia Bielefeld na kumpa pasi Tegete ambaye aliukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la kwanza.
Kuona hivyo wajerumani walikuja juu kusaka bao la kusawazisha, lakini bado ukuta wa Yanga uliendelea kuonekana kuwa makini, lakini makosa ya mshika kibendera yaliipelekea Armini Bielefeld kupata bao la kusawazsiha dakika ya 81 kupitia kwa Eric Agyemang amabaye alikua ameotea.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Young Africans 1 - 1 Arminia Bielefeld.
Kocha Mkuu wa Young Africans, Ernest Brandts amesema amefurahishwa na kiwango walichokionyesha wachezaji wake na anaamini kadri siku zinavyokwenda wanazidi kuimarika na kuwa bora, hivyo katika michezo mingine wataendelea kuonyesha mabadiliko makubwa.
Young Africans: Ally Mustafa 'Barthez, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondani, Kabange Twite, Haruna Niyonzima/Nizar Khalfan, Frank Domayo/Nurdin Bakari, Said Bahanuzi/Jerson Tegete, Didier Kavumbagu, David Luhende/Saimon Msuva

Friday, January 4, 2013
SIMBA, TUSKER HAKUNA MBABE
TIMU ya soka ya Simba jana ilitoka sare ya bao 1-1 na Tusker ya Kenya katika mechi ya michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kuanzia saa moja usiku, Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 18 kupitia kwa Haruna Moshi 'Boban' aliyeunganisha wavuni krosi kutoka kwa Ramadhani Chombo 'Redondo'.
Tusker ilisawazisha dakika ya 39 kwa bao lililofungwa na Khalid Aucho na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Licha ya kila timu kufanya mabadiliko kipindi cha pili na pia kushambuliana kwa zamu, hakuna iliyoweza kuongeza bao na hivyo kuzifanya zigawane pointi moja kila moja.
Kwa matokeo hayo, Tusker inaongoza kundi hilo kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, kufuatia kila moja kuwa na pointi tatu baada ya kucheza mechi mbili.
Hii ni mara ya pili kwa Simba kukutana na Tusker katika muda wa wiki moja. Katika mechi ya kirafiki kati ya timu hizo iliyochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Simba ilichapwa mabao 3-0 na Tusker.
Katika mechi iliyochezwa jioni, Jamhuri ya Pemba iliichapa Bandari mabao 2-1.
JK ASHIRIKI MAZISHI YA SAJUKI
sj2: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki wakati wa mazishi ya msanii huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam

TAIFA STARS KUJIPIMA UBAVU NA ETHIOPIA JAN 11
Timu ya Taifa (Taifa Stars) itacheza mechi ya kujipima nguvu dhidi ya Ethiopia. Mechi hiyo itachezwa Januari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Stars chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen inatarajia kuingia kambini jijini Dar es Salaam keshokutwa (Januari 6 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
Mechi hiyo itakuwa kipimo cha mwisho kwa Ethiopia kabla ya kwenda Afrika Kusini kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazoanza Januari 19 mwaka huu.
Ethiopia iko kundi C pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso. Ethiopia itacheza mechi yake ya kwanza Januari 21 mwaka huu dhidi ya Zambia.
Katika mechi yake ya mwisho, Taifa Stars iliifunga Zambia bao 1-0 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Desemba 22 mwaka jana Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Ethiopia ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo dhidi ya Morocco kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014. Mechi hiyo itachezwa Machi mwaka huu.
Wachezaji wanaotakiwa kambini ni Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam.
Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Benchi la Ufundi linaundwa na Kim, Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
UCHAGUZI KWA WANACHAMA WA TFF
Kamati ya Uchaguzi ya TFF inatarajia kukutana leo mchana (Januari 4 mwaka huu) ambapo pamoja na mambo mengine itapitia maendeleo ya uchaguzi kwa wanachama wa TFF ikiwemo Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board).
Wanachama wa TFF (vyama vya mikoa) wote wameshafanya uchaguzi ukiondoa mikoa ya Rukwa na Katavi inayotarajiwa kufanya uchaguzi baadaye mwezi huu.
Kwa upande wa vyama shiriki ambavyo bado havijafanya uchaguzi ni Makocha (TAFCA), Wachezaji (SPUTANZA), Waamuzi (FRAT) na Tiba ya Michezo (TASMA).
Vilevile Kamati ya Uchaguzi ya TFF baada ya kikao hicho huenda ikatangaza rasmi mchakato wa uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

YANGA KUKIPIGA NA WAJERUMANI KESHO
Timu ya Young Africans Sports Club yenye makao makuu yake jijini Dar es salaam nchini Tanzania kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Arminia Bielefeld ya kutoka nchini Ujerumani, mchezo utakaofanyika katika mji wa Antalya.
Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa pekee ya kuweza kujipima uwezo dhidi ya timu hiyo ya Ujerumani ambayo pia imekuja kambi y amafunzo kujiandaa na mzunguko wa ligi daraja la pili nchini Ujerumani.
Kocha Mkuu wa Young Africans, Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kwa kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Armini Bielefeld ambayo inawachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
"Unajua tuna siku tano (5) tangu tufike hapa mjini Antalya Uturuki na tumeshafanya mazoezi kwa siku nne (4) hivyo fursa ya kupata mchezo wa kirafiki ni nzuri sana kwetu kwani itanipa nafasi ya kuona wachezaji wangu wameshayashika kwa kiasi gani mafunzo yangu," alisema Brandts.
Arminia Bielefeld imeshawasili mjini Antalya kwa ajili ya kambi yake ya mafunzo na hivyo kwao pia ni fursa nzuri ya kuweza kujipima uwezo na timu ya Young Africans ambao ni mabingwa mara 23 katika ligi kuu ya Tanzania.
Jana asubuhi Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa siku ya Jumamosi mjini Antalya.
Kikosi cha wachezaji 27 waliopo mjini Antalya wote wako katika hali nzuri na hakuna maheruhi hata mmoja hali itakayompa kocha Brandts kuamua kumtumia mchezaji yoyote katika mchezo huo.
Kuhusu hali ya hewa leo jua linawaka toka asubuhi mpaka hivi sasa na kwa leo ni sentigred 23 mpaka 25, hivyo hali ya hewa ni nzuri kabis ana jua linawaka.

Thursday, January 3, 2013
SIMBA YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI
SIMBA jana ilianza vyema michuano ya soka ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba mabao 4-2 katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Pambano hilo halikuwa na mvuto sana kwa mashabiki kutokana na kuathiriwa na mvua iliyoanza kunyesha kabla ya timu kuingia uwanjani na hivyo kuwafanya wachezaji wateleze.
Jamhuri ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Mfanyeje Mussa Yussuf kabla ya Haruna Chanongo kuisawazishia Simba dakika ya 27.
Dakika mbili baadaye Simba iliongeza bao la pili kupitia kwa Chanongo kabla ya Mfanyeje kuisawazishia Jamhuri na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya mabao 2-2.
Simba iliongeza makali ya mchezo katika kipindi cha pili na kufanikiwa kuongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Felix Sunzu na Shomari Kapombe.
SAJUKI KUZIKWA KESHO DAR
MAZISHI ya msanii mahiri wa tasnia ya filamu Juma Issa Kilowoko ‘Sajuki’ yanatarajiwa kufanyika kesho (Ijumaa) mchana katika makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba amesema leo kuwa mazishi hayo yatasimamiwa na shirikisho hilo na wadau wa tasnia ya filamu
“Tumeamua kulichukua jukumu la kumzika msanii mwenzetu Sajuki na familia wabaki na shughuli nyingine kwa sababu amemwacha mke na mtoto, ambao kwa vyovyote watahitaji kuishi kwa hiyo kama kuna kidogo basi kiwasaidie, kwa hiyo tayari kuna kamati inayoshughulikia hilo,”amesema Mwakifwamba.
Rais wa TAFF alimedai kuwa bajeti ya awali kuanzia leo hadi siku ya mazishi gharama au fedha inayohitajika ni milioni saba, ambazo wadau mbalimbali na wasanii bado michango inahitajika hivyo amewaomba wanaoguswa na msanii huyo hata kama si wasanii, wafike msibani na kuwakilisha michango hiyo.
Wednesday, January 2, 2013
JK ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KIFO CHA SAJUKI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara kufuatia kifo cha msanii maarufu wa kujitegemea hapa nchini, Juma Kilowoko maarufu kwa jina la kisanii la Sajuki, kilichotokea usiku wa kuamkia tarehe 2 Januari, 2013 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Enzi za uhai wake, Marehemu Juma Kilowoko alianza kujishughulisha na Tasnia ya Sanaa kwa kujiunga na kundi maarufu la sanaa la Kaole kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa msanii wa kujitegemea ambapo aliendelea kupata umaarufu katika tasnia ya michezo ya kuigiza na filamu na kufanikiwa kutengeneza filamu nyingi.
Baada ya kuanza kuugua mwaka 2010, Marehemu Kilowoko aliwahi kupatiwa matibabu nchini India mwaka 2011 na kurejea akiwa amepata nafuu kubwa kiasi cha kumwezesha kutengeneza filamu nyingine, lakini alianza kuugua tena hadi mauti yalipomkuta.
“Nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na kifo cha Msanii Juma Kilowoko ambaye ametoa mchango mkubwa katika kuinua kiwango cha sanaa hususan michezo ya kuigiza na filamu hapa nchini. Kwa hakika kifo cha msanii huyu ni pigo kubwa kwa Tasnia ya Michezo ya Kuigiza na Filamu ambayo inaendelea kujizolea umaarufu mkubwa miongoni mwa Watanzania”, amesema Rais Kikwete katika Salamu zake za Rambirambi.
“Kutokana na msiba huu mkubwa, nakuomba wewe Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara unifikishie salamu zangu za rambirambi na pole nyingi kwa Familia ya Marehemu Juma Kilowoko kwa kuondokewa na Kiongozi na Baba wa Familia.
“Natambua uchungu ilio nao Familia ya Marehemu Kilowoko, lakini nawahakikishia kwamba binafsi niko pamoja nao katika kuomboleza kifo cha mpendwa wao. Nawaomba wawe na moyo wa uvumilivu, ujasiri na subira katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Namuomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aipokee na kuilaza mahala pema peponi roho ya marehemu Juma Kilowoko, Amina”.
Aidha Rais Kikwete ametoa pole kwa wasanii wote nchini hususan wanaojishughulisha na masuala ya michezo ya kuigiza na filamu kwa kumpoteza mwenzao na hivyo kuleta simanzi na huzuni kubwa miongoni mwao. Hata hivyo amewataka kuwa wavumilivu na kuchukulia kifo hiki kama changamoto kwao katika kuendeleza tasnia ya michezo ya kuigiza na filamu hapa nchini.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
2 Januari, 2013
Tuesday, January 1, 2013
BREAKING NEWSSSSSS! SAJUKI AFARIKI DUNIA
MSANII nyota wa filamu nchini, Juma Kilowoko, almaarufu kwa jina la Sajuki, amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam.
Sajuki alikuwa amelazwa kwenye hospitali hiyo wiki iliyopita kutokana na matatizo ya tumbo na pumuna hadi mauti yalipomfika, alikuwa amewekewa mashine ya kumsaidia kupumua.
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Sajuki alifariki dunia saa moja asubuhi na alifikishwa kwenye hospitali hiyo kutokana na kusumbuliwa zaidi na maumivu ya tumbo.
Mdogo huyo wa marehemu alisema madaktari walishauri Sajuki awekewe mashine ya kumsaidia kupumua kwa saa 10 ili itakapoondolewa aweze kuwa katika hali nzuri.
Alisema baada ya kuondolewa kwa mashine hiyo, iwapo Sajuki angeweza kukaa kwa saa 10 bila kutumia kifaa hicho, angeweza kupelekwa India kwa ajili ya matibabu zaidi.
Sajuki alipelekwa India mapema mwaka jana kwa ajili ya kupatiwa matibabu ya tumbo na baada ya kurejea nchini, hali yake ilikuwa nzuri, lakini alipaswa kurejea huko kwa matibabu zaidi.
Hivi karibuni, Sajuki aliandaa maonyesho kwa ajili ya kuwashukuru Watanzania kwa kumsaidia kupata matibabu ya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua. Alifanya maonyesho hayo katika miji ya Iringa na
Arusha.
Akiwa katika onyesho la mjini Arusha, msanii huyo alijikuta akiishiwa nguvu na kudondoka stejini kabla ya kusaidiwa na wasanii wenzake na kupelekwa hospitali.
Jumatatu iliyopita, Sajuki alihojiwa na mtangazaji Salama Jabir katika kipindi cha Mkasi kilichorushwa hewani na kituo cha televisheni cha East Africa, ambapo alielezea kwa kirefu kuhusu maisha yake, ugonjwa unaomsumbua na matarajio yake ya baadaye.
WACHEZAJI YANGA WAFURAHIA KAMBI UTURUKI
Wachezaji na bechi la ufundi la timu ya Young Africans wamefurahishwa na hali ya kambi hapa katika mji wa Antalya kwamba hali ya hewa ni nzuri, vyakula aina zote vinapatiikana na huduma za mazoezi kwa ajili ya kambi ni za kiwango cha juu sana.
Wakiongea na www.youngafricans.co.tz Kocha wa makipa Razaki Siwa amesema kw akeli hali ya hewa sio mbaya kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali, hali ya hewa ni nzuri, mazingira ya kambi ni ya kuridhisha vifaa vya kwa ajili ya mazoezi vipo kwa wingi hivyo inakuwa nio rahisi kwetu walimu kuwaelekeza wachezaji wafanye nini.
Kocha Siwa amesema pia wanaushukuru uongozi wa Young Africans kwa kuamua kuileta timu kambini nchini Uturuki kwani wachezaji wanapata nafasi nzuri ya kujifunza kwa pamoja, mafunzo ambayo hayana bughuza kwani kambi ipo katika hadhi ya kimataifa ndio maana timu nyingi za Ulaya
zinapenda kuja kuweka kambi eneo tulivu kama hili la Antalya.
Fred Felix Minizro kocha msaidizi kwa upande wake amesema hali ya kambi kwa ujumla ni nzuri, na kuhusu hali ya hewa ni baridi ya kisai tu kama Mbeya na Arusha hivyo haoni kama hali ya hewa inaweza kuwa ni kikwazo katika kambi hii ya mafunzo.
Naye kiungo mshambuliaji Saimon Msuva amesema wanafurahia kupata nafasi hii ya kuja kuweka kambi nchini Uturuki, kwani anaamin mazingira na huduma z akambi ni nzuri kabisa hivyo wanayapokea vizuri mafunzo ya kocha mkuu Brandts na pindi watakaporudi Tanzania wataweza kuwapa raha wapenzi wa soka kwa kuwaonyesha ni nini hasa wamekipata kwa kipindi cha wiki mbili
KOCHA MPYA SIMBA AMWAGA WINO MIEZI MINANE
KOCHA Mkuu mpya wa Simba, Patrick Leiwig kutoka Ufaransa, leo amemwaga wino wa kuifundisha timu hiyo kwa mkataba wa miezi minane. hafla ya kutia saini mkataba huo ilifanyika kwenye hoteli ya Spice iliyopo mtaa wa Lumumba na kusuhudiwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba,Geofrey Nyange 'Kaburu' na Katibu Mkuu, Evod Mtawala.
KITIME AUCHAMBUA MUZIKI 2012
Mwaka 2012 ndio huoo umetokomea, ni vizuri kuangalia yaliyopita ili kujitayarisha na yajayo. Muziki wa nchi yetu ulitawaliwa na muziki wa Bongoflava, Taarab, muziki wa bendi, matarumbeta, muziki wa Enjili, na muziki wa kiasili. Si siri kuwa muziki wa Bongoflava ndio uliokuwa ukitawala katika vyombo vya habari na sehemu nyingi za maonyesho ukifuatiliwa na muziki wa Taarab na muziki wa enjili. Katika muziki wote huu jambo lililokuwa wazi ni kuwa waimbaji ndio waliokuwa wakipewa kipaumbele katika tasnia hii. Waimbaji katika aina zote za muziki uliotajwa hapo juu ndio waliotajwa na kupewa sifa kwa ubora wa muziki. Kumekuweko na mashindano kadhaa ambayo yote yamejikita katika kutafuta vipawa vya waimbaji japo mara nyingi yamejitambulisha kama mashindano ya kusaka vipaji mbalimbali. Hakuna ubishi muziki wa dansi na muziki wa asili ndio muziki uliopewa muda mchache sana katika vyombo vya habari. Na hata katika muziki huo, bendi ambazo zimejikita kufuata mipigo ya Kikongo vilipewa nafasi zaidi ya bendi ambazo zimejichagulia njia nyingine za muziki wao.
Kuna sababu kadhaa ambazo zimefanya muziki wa bongoflava kuchukua nafasi zaidi katika vyombo vya habari, la kwanza ni uwingi wa kazi za bongoflava zinazorekodiwa. Karibu kila mji una studio ya aina moja au nyingine, na katika studio hizo kazi nyingi zaidi zinazorekodiwa ni aina hiyo ya muziki, hivyo kutokana na uwingi wa kazi hizo ni wazi kabisa ndizo ambazo zitaendelea kutawala anga la vyombo vya habari, na pia ni kutokana na mfumo wa vyombo vyetu vyote kujikita katika mfumo wa aina fulani tu za muziki.
Kwa mtizamo wangu heka heka za muziki wa Enjili zilipungua 2012. Yale matamasha makubwa ya muziki huo yalipungua sana, na hata nyimbo za kushtua jamii hazikuwa nyingi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Muziki wa Taarab haujaleta mabadiliko kimuziki, mengi yaliyofanywa katika 2012 ni marudio tu ya ubunifu uliofanyika nyuma. Kama vile uanzishwaji wa kucheza show katika taarab, upigaji wa gitaa na kuliachia pekee yake kama ilivyokuwa kwa bendi kuachia gitaa la rhythm miaka kabla ya tisini na zile video za kucheza mbele za viwanja vya hoteli. Kumekuweko tu ubunifu wa misemo na mipasho, jambo tena ambalo limesababisha kuenziwa zaidi kwa waimbaji tu katika fani hiyo pia.
Bendi ziko katika wakati mgumu, wakati wanamuziki wengi wa bendi wakilalamika kuwa muziki wa bendi haupigwi, kumekuweko na jitihada ndogo za bendi kurekodi nyimbo mpya, maelezo mengi yamekuwa ni kuhadithia enzi ambapo muziki wa bendi ulitawala na kuona kama hiyo ni sababu tosha ya muziki huo kurushwa hewani. Bendi chache zilizorekodi hazijaja na nyimbo zilizoweza kuteka umma wa wa Tanzania na hivyo kusababisha muziki huu kukosekana katika anga za muziki. Matangazo mengi ya muziki wa dansi yamekuwa ni kutangaza rap mpya au kupatikana kwa msanii mpya, lakini kiujumla hakujakuwa na kitu kipya katika muziki wa bendi.
Muziki asili pia umekosekana kwenye vyombo vya habari kwa kuwa si vikundi vingi vya muziki huu vyenye uwezo wa kulipia gharama za studio ambao muziki huu unastahili kurekodiwa. Studio nyingi zimejengwa kwa ajili ya muziki wa aina ya Bongoflava tu, zile studio za kuweza kuruhusu kundi la muziki wa asili kurekodi gharama yake huwa ni kubwa sana.
Kundi la Makirikiri lilitakiwa kuwa elimu tosha kwa wasanii wa muziki wa Kiasili, kuwa na muziki huo ukifuata taratibu nzuri ya kurekodiwa unauza vizuri sana, bahati mbaya kuna vikundi sasa vimeacha muziki na ngoma zao, vinaiga uchezaji wa Makirikiri.
Pengine watu watasema nimesahau muziki wa kwaya, sijausahau, kwa kweli muziki huu umebaki hasa kwenye muziki wa Enjili. Hapo zamani ulikuwa ukitumika sana kwenye siasa na kampeni , lakini kwa mwaka 2012 hali imekuwa mbaya kwa muziki huu.
Pamoja na kuwa wengine wangeweza kusema tunasonga mbele katika muziki, kwangu mimi naona tunarudi nyuma kitaaluma. Tasnia inaingiza pesa nyingi zaidi, na hata kuna wasanii walioingiza pesa nyingi sana, lakini kwangu hilo si kipimo cha maendeleo katika tasnia hii.
Kama nilivyoanza kusema washika maikrofon wamekuwa ndio alama ya muziki wa Tanzania. Muziki ni zaidi ya kuimba. Katika kuimba sauti nzuri ya muimbaji ni muhimu, na ninashukuru kwa hilo tunao waimbaji wazuri wengi sana, lakini ule muziki unaomsindikiza muimbaji ni muhimu sana kwani ule hauna mipaka wala lugha, na ndio unaoweza kutufungulia mlango wa soko la kimataifa. Wengi tunapenda sana muziki wa kutoka Kongo, Nigeria, South Africa, pamoja na kuwa hatujui hata moja wanaloliongelea tunaupenda muziki huo kutokana na mpangilio wa vyombo vyao. Kutokujali wapigaji katika mfumo wa nchi yetu ndio unatupelekea kuwa watu wa ‘copy and paste’ wa upigaji wa muziki wa nchi nyingine. Ukiorodhesha nyimbo zote zilizotikisa nchi hii kwa mwaka 2012 utagundua asilimia kubwa ya muziki uliotumika ulikuwa ni wa kunakili kutoka muziki wa nchi nyingine, Nigeria, Congo na Afrika Kusini ndio wamekuwa waalimu wetu wakuu. Ushauri kwa maproducer wa Bongoflava, kuangalia pia muziki wetu wa asili humu ndani ya nchi ili tuje tumalize 2013 na kitu chetu ambacho Wanaigeria, Wakongo nao pia waige toka kwetu. Inawezekana sana maana wimbo wa Weekend wa Afro70 uliwahi kuweko katika kumi bora 1972, Nigeria.
Muziki wa Enjili pamoja na kuwa ndio unaotegemewa kutufundisha maadili, ulikuwa na kasoro moja kubwa nayo ni kukosa maadili kwa kucopy na kupaste. Nyimbo nyingi zilizokuwa maarufu na kuteka hisia za maelfu ya watu zilikuwa ni kuiga moja kwamoja kutoka Afrika ya kusini. Najiuliza je ndio kilichopunguza moto wa muziki huu 2012? Kulikuwa hakuna za kukopi? Wanamuziki wa Enjili kama ilivyo kwa ushauri kuhusu Bongoflava, ni muda wa kurudi nyuma na kutumia raslimali ya utamaduni iliyoko kuleta mabadiliko na kukuza soko la muziki huo.
Tasnia ya muuziki wa Tanzania katika tafiti moja wapo umeitwa ‘the radio-driven contemporary music industry’. Kwa maneno rahisi, tasnia ambayo imekuwa inaendeshwa na radio. Radio zimekuwa na uwezo wa kumpandisha na kumshusha mwanamuziki, kumtafutia soko, kumzibia soko na kadhalika. Hali hii ikisindikizwa na rushwa ambayo imetapakaa katika jamii yetu, unapata picha kuwa kungeweza kukawa na sura bora au tofauti ya muziki hali isingekuwa ilivyo. Kuna ripoti za watu kutoa hongo nyimbo za wenzao zisipigwe, hongo ili nyimbo zipigwe, visasi vya kuzuia nyimbo zisipigwe na kadhalika. Na katika jamii ambayo imekuwa na kawaida ya kutegemea vyombo vya habari kujua muziki gani mpya na mzuri, uwanja huu si uwanja ulio tambarare hata kidogo. Bahati mbaya inaonekana wenye vyombo hivi wako mbali na ukweli unaoendelea katika vyombo vyao au kwa kutokujua au kupuuza. Janga hili limevikumba hata vyombo ambavyo vinaendeshwa na taasisi za dini. Wanamuziki wa muziki wa Enjili nao pia wanalia kudaiwa rushwa na watangazaji wa radio za Enjili!. Nakumbuka siku niliyopata nafasi kuongea na kiongozi mmoja wa dini ambaye Kanisa lake linaendesha kituo cha radio, nilipata mshangao baada mkuu huyo, kuanza kutetea watangazaji wake badala ya kuamua kufanya uchunguzi wa tuhuma.
Umefika muda wa radio kuanza kujigawa kimuziki. Ni kichekesho mji kuwa na vituo vya radio 30 halafu vyote vinapiga aina hiyohiyo ya muziki, wakati kuna aina mbalimbali za watu. Ajabu ni kuwa wenye radio wanajua kuwa katika nchi nyingine unaweza kukuta radio iliyoamua kupiga aina fulani tu ya muziki, Jazz Radio, Country music Radio, Classic Music Radio, lakini hilo limekuwa gumu kwao kutekeleza hapa. Kuwe na utofauti, Wasikilizaji tuko wa aina tofauti.
Vyombo vya habari viijitahidi kupata wataalamu husika wa aina tofauti za muziki, muziki unaviingizia vyombo hivyo mabilioni ya fedha, vyombo vya habari viupe heshima yake. Bila muziki hakuna radio.
Magazeti yamekuwa mstari wa mbele katika kutangaza aina mbalimbali za wasanii na sanaa. Pamoja na hongera kwa kazi nzuri lakini bado kuna nafasi kubwa ipo tupu, hakuna wataalamu wa uandishi wa habari za muziki. Hivyo habari nyingi za muziki zinaandikwa na waandishi kama wapenzi wa muziki na si wataalam wa uandishi wa muziki, jambo ambalo liko tofauti na uandishi wa michezo kwa mfano soka. Unaweza ukasoma habari ya soka ambapo mwandish atakueleza nafasi za wachezaji, kama ni faulo, ni nini kilisababisha, na kama ni goli lilikuwa ni la kichwa au kona au penalty, hili haliko katika muziki. Utaambiwa tu bendi ilipagawisha, au msanii fulani ateka nyoyo za wapenzi, na maelezo ya juu juu kama yale, kunahitajika kuanzishwa mafunzo ya elimu ya uandishi wa kazi za sanaa. Hili litapunguza hata vurugu kama zilizotawala mwaka huu ya wapiga picha kufikia hata kulala chini ili tu wapate picha ya nguo za ndani za msanii na hayo ndio kuwa maelezo makuu ya onyesho zima la muziki.
Ikiwa kulikuwa na mchango wa serikali katika muziki, basi ulikuwa mdogo au ulikuwa ni kwa shughuli maalumu lakini si kwa kutengeneza mazingira ya kuwezesha unafuu kwa wanamuziki kwa ujumla. Idara ya Utamaduni imeendelea kupata bajeti ndogo ambayo imefanya Baraza La Sanaa La Taifa kuendelea kubaki Dar es Salaam tu, likibangaiza kuweko kwa kutegemea kutoa vibali mbalimbali kwa wasanii, na nguvu zake kuonekana Dar es Salaam tu. Na kwa kuwa hakuna Maafisa Utamaduni Mkoa, na Maafisa Utamaduni Wilaya na Manispaa wako chini ya serikali za mitaa hivyo kuwa wizara tofauti na Waziri wa Utamaduni, nguvu za serikali katika utamaduni ni 0. COSOTA chombo ambacho shughuli yake ilikuwa ni kulinda hakimiliki za wasanii na ambacho kilikuwa chini ya wasanii, kwa kinyemela kabisa kimerudishwa katika mikono ya serikali, lakini bado kinakusanya mirabaha 'kwa niaba ya wasanii' huku kukiwa na bodi isiyo na uwakilishi wa wasanii kuanzia 2007. Swali utakusanyaje pesa kwa iaba yangu lakini huniruhusu kujua ni kiasi gani umekusanya, unazitumiaje na ukiulizwa unakuwa mkali!!!!!!? Kuna wasanii wamekuwa wakidai kurudishiwa COSOTA, ushauri wangu wasanii wakae wajipange na kuelewa vizuri sheria ya Hakimiliki kabla ya kujitwishwa zigo hilo la miba.
Katika miezi 6 ya mwisho ya 2012 kumejitokeza spidi kali ya Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato kutengeneza mazingira ya kukusanya mapato kutokana na mauzo ya kazi za muziki na filamu. Kimsingi kulipa kodi ni wajibu wa kila mwananchi na wasanii ni wananchi pia, lakini taratibu zake ndio zinanipa utata, hasa pale ambapo kwa muda mrefu imekuwa ikitangazwa kuwa njia hii itasaidia wasanii kwa kupunguza kuibiwa. Sentensi hii inaonyesha wazi anaeiongelea aidha hajui mfumo wa biashara ya kazi muziki, au kwa makusudi anapotosha ili kuficha kitu. Wasanii wengi huwa wamekwishalipwa kwa kazi ambazo zimesambaa na ziko barabarani zinaibiwa, wanaoibiwa ni wasambazaji. Hivyo kulinda kazi hizo unamlinda msambazaji si msanii. Pia kuanza kukusanya kodi kwa kazi hizi kumepewa jina ‘kurasmishwa kwa kazi ya usanii’, kuna mabilioni wasanii wanatakiwa walipwe na watumiaji wa kazi za sanaa, kama radio na TV, mapromota, waajiri na kadhalika hakuna anaeliongelea hilo wala hakuna anaetamka takwimu hizo. Kuna kazi ya kurudisha mitaala ya masomo ya sanaa mashuleni, kurudisha vyuo vya walimu wa sanaa, kurudisha maafisa utamaduni kuwa chini ya Wizara ya Utamaduni kuwawezesha kufanya kazi zao kadri ya sera ya Utamaduni, na mengine mengi ya aina hiyo ndio ningeona kurasimisha kazi za sanaa, lakini kukusanya kodi tu kwa kazi ambazo hata hivyo mikataba yake mingi inautata na kuita urasimishaji si sahihi.
Katika nchi nyingi critics au watu ninaoweza kuwaita kiswahili wakosoaji, huwa ni muhimu katika maendeleo ya sanaa, watu hawa hupata heshima kutokana na kuweza kuangalia mapungufu katika kazi za sanaa na kuyasema, jambo ambalo hupelekea wasanii kujirekibisha na kutengeneza kazi bora zaidi. Hapa kwetu kutoa ushauri ni kutafuta matusi, toka kwa wasanii wenye kazi husika, vyombo vya habari na hata sehemu ya jamii, umefika muda wahusika kuchukua uchambuzi kama changa moto za kuboresha kazi.
Niliyoyataja hapa yote yako wazi ninachotegemea ni kuona 2013, hatua zinaanza kupigwa kurekibisha, ili wanamuziki wa nchi hii nao wapate nafasi sawa na wengine wa nchi nyingine.
John Kitime
31.12.2012
Sinza, Dar es Salaam
WACHEZAJI 22 WAITWA KAMBINI TAIFA STARS
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ametaja wachezaji 22 watakaoingia kambini Januari 6 mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mashindano dhidi ya Morocco itakayochezwa Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa Kocha Kim, wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini katika hoteli ya Tansoma saa 11.30 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza Januari 7 mwaka huu.
Wachezaji walioitwa ni makipa Juma Kaseja kutoka Simba ambaye pia ndiye nahodha wa Stars, Aishi Manula na Mwadini Ally wote kutoka Azam. Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Issa Rashid (Mtibwa Sugar), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).
Viungo ni Salum Abubakar (Azam), Athuman Idd (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Khamis Mcha (Azam), Frank Domayo (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho Ngasa (Simba), Simon Msuva (Yanga), na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Mbali ya Kim, benchi la ufundi la Taifa Stars linaundwa na Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Tasso (Meneja), Dk. Mwanandi Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Mtaalamu wa tibamaungo) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).
CAF YAMTUMA LIUNDA KUKAGUA VIWANJA ETHIOPIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua ofisa wake Leslie Liunda wa Tanzania kwenda Ethiopia kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa utoaji leseni kwa klabu zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.
Ofisa huyo atawasili nchini Ethiopia kesho (Januari 2 mwaka huu) ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 6 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.
Utekelezaji wa kazi yake hiyo nchini Ethiopia utahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF), Wizara ya Michezo ya nchi hiyo, viongozi wa klabu na mameneja wa viwanja husika.

YANGA WAANZA MAZOEZI UTURUKI
Wachezaji wa Young Africans wakiwa nje ya hotel ya Fame Residence tayari kwa kuelekea kuanza mazoezi
Wachezaji wa Young Africans wakifanya mazoezi leo katika Uwanja wa Fame Residence Football - Antalya Uturuki
Kocha wa Magolikipa Razaki Siwa akiwawapa maelekezo magolikipa Said Mohamed, Yusuph Abdul na Ally Mustafa 'Barthez'
Young Africans Sports Club imeanza mazoezi jana asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.
Mji wa Antalya ni maarufu katiak medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameanda sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja.

KOCHA MPYA WA SIMBA ATUA DAR
Katibu wa Simba, Evodius Mtawala (kushoto) akiongozana na kocha mpya wa klabu hiyo, Patrcik Liewig na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba, Manembe baada ya kocha huyo kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam jana.
Subscribe to:
Posts (Atom)