KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 12, 2010

Mwakalebela afikishwa mahakamani



KATIBU Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Fredrick Mwakalebela amefikishwa mahakamani na kusomewa shtaka la tuhuma za kutoa rushwa wakati wa mchakato wa upigaji kura za maoni kwa wagombea wa Chama cha Mapinduzi.
Mwakalebela alisomewa shtaka hilo jana na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Prisca Mpela mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Iringa, Festo Lwila.
Hata hivyo, Mwakalebela hakuwepo mahakamani kutokana na kuomba udhuru na kesi yake imepangwa kutajwa Agosti 17 mwaka huu.
Kiongozi huyo wa zamani wa TFF, aliyekuwa akiwania kuteuliwa kuwa mgombea wa Jimbo la Iringa Mjini, anatuhumiwa kutoa rushwa ya pesa taslimu sh. 100,000 kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Mkoga, Hassan Luhanga, ambazo alitakiwa kuzigawa kwa wanachama wa CCM 30 ili wamchague katika kura za maoni.
Lwila aliieleza mahakama kuwa, kutoa rushwa ni kinyume cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15 (1) (b), kinachokwenda sambamba na sheria ya gharama za uchaguzi namba 16 ya mwaka 2010 kifungu namba 21 (1) (a) na kifungu cha 24 (8).

No comments:

Post a Comment