KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, May 2, 2015

YANGA FUNGA HAO WAARABU





Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini - TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri Wawakilishi pekee wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CC) timuYoung Africans katika mchezo wake wa marudiano dhidi ya timu ya Etoile du Sahel utakaochezwa kesho nchini Tunisia.

Katika salamu zake Malinzi amesema ,Young Africans wakiwa ndio timu wawakilishi pekee wa Tanzania na Afrika Mashariki katika michuano ya kimataifa barani Afrika wanapaswa kupambana kuhakikisha wanasonga mbele katia hatua inayofuata.

Katika mchezo wa awali uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es salaam, Young Africans ilitoka sare ya bao 1- 1 na Etoile du Sahel, na mshindi wa jumla kwa mchezo wa huo, atacheza hatua ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu zitakazokuwa zimetolewa kwenye Ligi ya Mabingwa (CL) kuwania kufuzu kwa hatua ya makundi.

Mchezo huo wa marudiano utapigwa kesho jumamosi katika dimba la Olympique de Sousse katika mji wa Sousse kuanzia majra ya saa 3 kamili usiku kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

No comments:

Post a Comment