Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii kwa
michezo sita kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini, huku michezo mitatu
ikichezwa siku ya Jumamosi na michezo mingine mitatu ikichezwa siu ya jumapili.
Jumamosi
katika Uwanja wa Sokoine wapinzani wa jiji la Mbeya, Prisons FC watakuwa wenyeji
wa wagonga nyundo Mbeya City mchezo utaochezwa majira ya saa 10 kamili kwa saa
za Afrika mashariki na Kati.
Katika
Uwanja wa Nangwanda Sijaona wenyeji timu ya Ndanda SC watawakaribisha wakata
miwa wa Kagera Sugar, huku jijini Tanga Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa
maafande wa JKT Ruvu mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Jumapili
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaa, Simba SC watawakaribisha Azam FC,
mchezo ambao unatabiriwa kuwa na upinzani mkali kusaka nafasi ya pili ili
mwakani kuweza kuwakilisha Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho
barani Afrika.
Jijini
Tanga wagosi wa kaya Coastal Union watawakaribisha timu ya Stand United kutoka
mjini Shinyanga, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, huku kwenye
Uwanja wa Manungu mjini Morogoro wenyeji Mtibwa Sugar wakiwakaribisha maafande
wa Ruvu Shooting.
No comments:
Post a Comment