Mchezaji James Mwasote Ambrose wa timu ya Tanzania Prisons FC amechaguliwa
kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa mwezi Machi 2015 kufuatia
kuwapiku wachezaji wengine waliokua wakiwania nafasi hiyo.
Jopo la maalum la
makocha ambao hutafuta wachezaji bora kwa kila mchezo na kisha kujumlisha alama
za mchezaji kwa kila mchezo na kumpata mchezji bora wa mwezi, ndio hufanya kazi
ya kuchagua mchezaji bora kwa kila mwezi.
Mshambuliaji wa Young
Africans Mrisho Ngasa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom
mwezi Aprili kufuatia kuwapiku Amos Edward, Frank Domayo na Emmanuel Okwi baada
ya kupata alama nyingi za jumla za mchezaji bora kwa kila mchezo.
Kwa kuibuka wachezaji
bora wa mwezi Machi na Aprili, James Ambrose na Mrisho Ngasa watazawadiwa fedha
taslimu sh. milioni moja kwa kila mmoja kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo
kampuni ya simu za mkononi ya Vodaom.
NB: Kesho jumamosi
tarehe 02 Mei 2015, kutakua na mkutano na waaandishi na habari saa 5 kamili
asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa TFF - Karume, waandishi wote wa habari
mnaombwa kuhudhuria bila kukosa.
No comments:
Post a Comment