SIMBA WATAKIWA KUMLIPA CHANONGO MIL 11
Klabu ya Simba SC inatakiwa kumlipa
mchezaji Haruni Chanongo sh. 11,400,000, kufikia Aprili 30, 2015
vinginevyo Sekretarieti ya TFF itaanza kukata mapato ya Simba ili kumlipa
mchezaji huyo.
Iwapo Simba itakuwa na vielelezo
vingine katika kikao kinachofuata cha Kamati kitakachofanyika Mei 3, 2015
itafanywa hesabu na Simba kurejeshewa fedha itakayokuwa imezidi.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji
ya TFF imeagiza kwa klabu ya Simba na klabu nyingine zote kuwa kwa wachezaji wa
mkopo, maslahi yao (mishahara na posho) yote yailipwe na klabu husika kwa klabu
ambayo mchezaji anakwenda kwa mkopo ili malipo yake yawe yanafanyika kutoka
kwenye klabu moja badala ya kufuatilia malipo yake katika klabu mbili tofauti,
hali hii inaweza msabababishia usumbufu mchezaji aliye kwenye mkopo.
Amissi Tambwe vs Simba Sports Club
Mchezaji Amissi Tambwe aliwasilisha
malalamiko dhidi ya Simba ya kutolipwa dola 7,000 za Marekani zilizotokana na
klabu hiyo kuvunja mkataba wake Desemba 15, 2014. Uamuzi wa kuvunja mkataba
ulikuwa ni wa makubaliano ya pande zote ambapo Simba ilitakiwa iwe imemlipa
fedha hizo mlalamikaji kufikia Desemba 17, 2014.
Katibu Mkuu wa Simba SC , Steven Ally
alikiri klabu yake kudaiwa na mchezaji huyo na kuwa wameshafanya mawasiliano na
wakili wake aliyepo Ureno, Felix Majani na kupanga utaratibu wa kulipa
isipokuwa kinachosubiriwa ni kusaini hati ya makubaliano ya malipo (Deed of
Settlement).
Kamati imesikitishwa na klabu ya Simba
kushindwa kumlipa mchezaji huyo kama ilivyokuwa katika makubaliano ya kuvunja
mkataba yaliyofikiwa na pande zote mbili Desemba 15, 2014.
Klabu ya Simba inatakiwa kumlipa
Amissi Tambwe fedha hizo kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ya dola 5,000 malipo
yawe yamefanyika kufikia Aprili 30, 2015. Salio la dola 2,000 ili kukamilisha
jumla ya dola 7,000 liwe limelipwa kufikia Mei 10, 2015, uamuzi ambao upande wa
Simba ulikubaliana nao.
Amiri S.
Msumi vs Ndanda SC
Klabu ya
Ndanda SC imeamuriwa kumlipa mchezaji Amiri S. Msumi kiasi cha fedha sh.
2,600,000. Pia Kamati ilihoji mkataba kutokuwa na kipengele cha mshahara, na
kusema ni lazima mkataba uonyeshe Kaiser ambacho mwajiriwa analipwa.
Pia Kamati
imeagiza kuwa vilabu vifahamishwe kuwa fedha ya kusaini mkataba (sign on fee) hazitakiwi
kulipwa kwa mafungu. Tafsiri ya fedha ya kusaini, ni mchezaji kulipwa fedha
yote baada ya kusaini, na si kwa mafungu. Pamoja na uamuzi huo, Katibu Mkuu wa
Ndanda SC ametakiwa kuwepo kwenye kikao cha Mei 3, 2015.
Malalamiko mengine yataendelea kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za
Wachezaji Mei 3, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment