'
Wednesday, May 6, 2015
COASTAL UNION YAAGIZWA KUITISHA MKUTANO WA DHARULA
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ameiandikia barua Klabu ya Coastal Union akiiagiza klabu hiyo kuitisha mkutano mkuu wa dharura wa wanachama tarehe 17 Mei mwaka 2015.
Matokeo ya maamuzi haya yamepatikana baada ya kikao cha usuluhishi cha amani kilichoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ahmed Iddi Mgoi aliyekuwa ameongozana na Makamu Mkurugenzi wa Sheria na Uanachama shirikisho la soka nchini (TFF) Eliud Peter Mvella kilichofanyika April 13 mwaka huu katika hotel ya Tanga Beach Resort Tanga mjini.
TFF imeahidi kutuma orodha tatu za majina
(A) Wanachama stahiki.
(B) Wanachama waliobainika kuwa wanadosari na inabidi wathibitishwe na wanachama stahiki naa.
(C) Waombaji wapya wa wanachama watakaohakikiwa na wanachama stahiki.
Orodha hizi zinapaswa kubandikwa kwenye ubao wa Matangazo wa Klabu, katika kikao cha ufunguzi cha kuleta usuluhisho huo, mbali na kuhudhuriwa na kamati ya Utendaji ya Coastal Union chini ya Makamu wake Mwenyekiti Steven Mguto pia kilihudhuria na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF,Khalid Abdallah, Mwenyekiti wa Chama cha soka Mkoa wa Tanga,Said Soud.
Wengine waliohudhuria kikao hicho walikuwa ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Tanga, Digna Tesha, Katibu wa Chama cha soka Mkoa wa Tanga, Beatrice Mgaya, Afisa Utamaduni Jiji la Tanga, Peter Semfuko na Katibu wa Chama cha soka wilaya ya Tanga (TDFA) Salim Carlos.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment