KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, May 1, 2017

YANGA YAVULIWA UBINGWA KOMBE LA FA, YACHAPWA 1-0 NA MBAO FC




MABINGWA watetezi wa michuano ya Kombe la FA, Yanga jana walivuliwa ubingwa baada ya kupigwa mweleka wa bao 1-0 na Mbao FC katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Hili ni taji la pili kuvuliwa kwa Yanga msimu huu. Mapema kabla ya kuanza kwa ligi kuu, Yanga ilivuliwa taji la Ngao ya Jamii kwa penalti 4-1 na Azam, baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya bao 1-1.

Kutokana na ushindi huo, Mbao FC sasa itacheza fainali ya kombe hilo kwa kumenyana na Simba, katika mechi itakayopangiwa tarehe hapo baadaye.

Bao pekee na la ushindi la Mbao lilitokana na uzembe wa beki Andrew Vicent 'Dante' baada ya kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Pius Buswita.

No comments:

Post a Comment