KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, May 15, 2017

SERENGETI BOYS KUIVAA MALI LEO AFCON U-17 GABON


Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa Miaka 17, Serengeti Boys, leo Jumatatu  inafungua pazia lake katika mashindano ya Kombe la Afrika kwa Vijana, kwa kumenyana na Mali katika michuano hiyo inayofanyika nchini Gabon.
Serengeti Boys ipo Kundi B, pamoja na timu nyingine za Angola na Niger ambazo nazo zitakuwa kibaruani leo.
Akizungumza  kwa njia ya simu jana, kocha mkuu wa kikosi hicho, Bakari Shime, alisema kuwa kikosi chake kipo vizuri na kimejiandaa vya kutosha kuwakabili vijana wa Mali kwenye mchezo huo wa kwanza.
 “Kikosi kipo vizuri na tumejipanga kuikabili vilivyo timu ya Mali kwani tunataka kuwafurahisha Watanzania kwa kutowaangusha na naomba wazidi kutuombea,” alisema Bakari Shime.

timu hiyo imepata pigo baada ya Nahodha Abas Makamba, kuvunjika mguu kwa hiyo hataweza kucheza michuano yote.

No comments:

Post a Comment