KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, March 30, 2015

STARS, MALAWI ZAINGIZA MIL 72/-


Mchezo wa kirafiki wa Kimataifa uliofanyika jana jumapili jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kati ya wenyeji timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) umengiza jumla ya tsh 72.839,000 kutokana na idadi ya washabiki 15,762 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.

Mgawanyo wa mapato kwa mchezo hu ni VAT 18% sh. 11,111,103, gharama za tiketi sh. 3,203,700, gharama za mchezo (15%)sh. 8,778,639, Uwanja (15%) 8,778,639, CAF (10%) sh. 5,852,426 na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF (35%) sh. 35,114,560.

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini inatoa shukrani kwa chama cha soka mkoa wa Mwanza  (MZFA) kwa ushirikiano wao katika kufanikisha maandalizi ya mchezo huo, waandishi na vyombo vya habari mbalimbali kwa sapoti waliyoitoa kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)

Aidha TFF iinawashukru wapenzi, wadau na washabiki wa soka nchini, na hususani wa kanda ya ziwa waliojitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo, kwani waliishangilia Taifa Stars tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho kwa ustaarabu wa hali juu.

Katika mchezo huo Taifa Star ilitoka sare ya bao 1- 1 dhidi ya The Flames, bao la wageni lilifungwa na Mecium Mhone kabla ya na Mbwana Samatta kuisawazishia Tanzania.

No comments:

Post a Comment