KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, March 25, 2015

BEACH SOCCER WAREJEA


Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni (Beach Soccer) imerejea nchini juzi mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia ikitokea nchini Misri,ambako mwishoni mwa wiki ilipoteza mchezo wake wa marudiano kwa kufungwa 9-4 na wenyeji.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema timu ya soka la ufukweni haikupata matokeo mazuri katika mchezo wake kutokana na ugeni wa michuano hiyo.

Malinzi alisema uzoefu ndio ulikuwa kikwazo kwa timu ya Tanzania, kwani ndio mara ya kwanza kushiriki michuano hiyo ikiwa ni miezi sita tangu kutambulishwa kwa mchezo huo nchini Tanzania.

Ili kuwa na timu bora ya Taifa na wachezaji wengi wa mchezo huo, TFF imepanga kuutangaza na kuufundisha mpira wa ufukweni katika mikoa mbali mbali nchini , tofauti na sasa ambapo mchezo huo unachezwa  Dar es Salaam na Zanzibar.

Katika mchezo huo, mabao ya Tanzania yalifungwa na Ally Rabbi (3) Kashiru Salum (1). Tanzania imetolewa kuwania kufuzu kwa fainali za Soka la Ufukweni barani Afrika na Misri kwa jumla ya mabao 15-6.
Misri imefanikiwa kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa Soka la Ufukweni Visiwa vya Shelisheli, zitakazofanyika mwezi Aprili, mwaka huu, kwa mara ya saba mfululizo tangu kuanzishwa kwa mchezo huo mwaka 2006 nchini humo.

No comments:

Post a Comment