KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, March 18, 2015

BEACH SOCCER KUONDOKA ALHAMISI


Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Cairo, Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika kwa soka la ufukweni utakaofanyika Jumapili.

Tanzania inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Misri  ili kufuzu kwa fainali za soka la ufukweni barani Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli, kufuatia kupoteza mchezo wake awali uliofanyika Escape 1 jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Msafara wa timu ya Beach Soccer utakaoondoka na Shirika la Ndege la Ethiopia, utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri Mgoyi, Kocha Mkuu John Mwansasu, Kocha Msaidizi Ali Sheikh Alhashby, Meneja Deogratius Baltazar na Daktari wa timu, Dr Leonidas Rugambwa.

Wachezaji ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed Rajab Juma, Roland Revocatus Kessy, Samwel Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi, Mohamed Makame Silima, Mwalimu Akida Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum Said na Ally Rabby Abdallah.

No comments:

Post a Comment