KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, March 23, 2015

SIMBA YAFUFUA MATUMAINI


SIMBA jana iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mechi ya ligi kuu ya soka ya Tanzania Bara, iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo  umeleta ahueni kubwa kwa mashabiki wa Simba, kufuatia timu hiyo kuchapwa mabao 2-0 na Mgambo Shooting wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mshambuliaji machachari Ibrahim Ajibu aliwainua vitini mashabiki wa Simba dakika ya 60 baada ya kuifungia bao kwa njia ya penalti baada ya Awadh Juma kuchezewa rafu ndani ya eneo la hatari.

Dakika moja baadaye, Awadhi aliiongezea Simba bao la pili baada ya kuwatoka mabeki wa Ruvu Shooting na kufumua shuti lililotinga moja kwa moja wavuni.

Elias Maguri alihitimisha furaha ya mashabiki wa Simba dakika ya 75 baada ya kuifungia bao la tatu, baada ya kipa Abdalla wa Ruvu Shooting kutema shuti la Saidi Ndemla na mpira kumkuta mfungaji.

No comments:

Post a Comment