KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, March 18, 2015

SPIKA ANNE MAKINDA AMKUMBUKA MAREHEMU KOMBA


 SPIKA wa Bunge, Anne Makinda, jana alitoa taarifa ya Spika kuhusu kifo cha aliyekuwa mbunge  wa Mbinga Magharibi (CCM),marehemu Kaptein John Komba, aliyefariki  dunia Februari 28, mwaka huu, kutokana na shinikizo la damu.

Makinda alitoa taarifa hiyo bungeni mjini hapa jana kabla ya kuanza kwa kipindi cha maswali na majibu.

Katika taarifa yake, Spika alisema huo ulikuwa ni msiba mkubwa na wao kama bunge, wamepoteza mtu ambaye ni mpiganaji na atakumbukwa daima.

“Kwa kweli ni msiba mkubwa. Mnamo Febuari 28, mwaka huu, tulimpoteza mbunge mwenzetu Kapteni Komba na kumzika Machi 3, mwaka huu, nyumbani kwao Lituhi mkoani Ruvuma,”alisema.

Spika Anne alisema, marehemu Komba, alifariki kwa ugonjwa wa shinikizo la damu akiwa katika majukumu yake ya kikazi kama mbunge.

Aidha, alisema kabla ya kukutwa na mauti, Komba alikuwa katika maandalizi ya safari ya kwenda nchini Ethiopia kwa shughuli za kibunge.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wabunge kusimama kwa dakika moja kwa ajili ya kumkumbuka marehemu Komba.

No comments:

Post a Comment