KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, May 1, 2014

YANGA YAZIDI KUMEGUKA, DOMAYO AFUATA NYAYO ZA KAVUMBAGU, AMWAGA WINO AZAM



KIUNGO mkabaji wa Yanga SC, Frank Domayo amesaini mkataba wa miaka miwili kujiunga na mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Azam FC jana mjini Mbeya.

Domayo amesaini Azam FC baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na Yanga SC, ambayo alijiunga nayo akitokea JKT Ruvu miaka miwi iliyopita.

Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa Mohamed ‘Father’ amesema katika kuendelea kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao, wamepiga hatua nyingine kwa kumsaini Domayo.

Father alisema wamemsajili Domayo kutokana na ushauri na mapendekezo ya Kocha Mkuu wa timu hiyo,
Joseph Marius Omog.

Domayo anakuwa mchezaji wa wa pili ndani ya siku mbili kusajiliwa na Azam FC kutoka Yanga. Siku mbili zilizopita, Azam ilifanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Didier Kavumbagu baada ya mkataba wake na Yanga kumalizika.

No comments:

Post a Comment