KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, May 6, 2014

AZAM YAVUNJA MKATABA NA KONE WA IVORY COAST


UONGOZI wa klabu ya Azam FC umefikia makubaliano ya kuvunja Mkataba na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Ismail Kone ambaye alikuwa anamaliza Novemba mwaka huu.

Pande zote mbili zimefikia makubaliano na mchezaji huyo amepewa haki zake na kurejea nchini mwao. Aidha, Azam FC inawashukuru kwa mchango wao, wachezaji wake wanne, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Malika Ndeule na Omar Mtaki kwa kipindi chao chote walichoitumikia klabu hiyo.

Wanne hao wamemaliza mikataba yao na hawataongezewa- klabu inawashukuru kwa mchango wao kwa kipindi chote tangu wajiunge nayo. Azam FC pia imepokea na kuyakubali maombi ya wachezaji wake wawili, Samih Haji Nuhu na Luckson Kakolaki kustaafu kwa sababu mbalimbali.

Nuhu anasumbuliwa na maumivu ya goti ambalo hana matumaini ya kupona karibuni, wakati Kakolaki ameamua kustaafu ili achukue mafunzo ya ukocha. Klabu imempa ajira ya kudumu Nuhu katika moja ya viwanda vyake, wakati Kakolaki ameingizwa kwenye benchi la Ufundi la akademi ya klabu.

Tayari klabu imekamilisha usajili wa wachezaji wapya watatu, ambao ni washambuliaji Didier Kavumbangu wa Burundi, Ismaila Diarra kutoka Mali na mzalendo Frank Domayo.

Usajili wa Kavumbangu na Diarra unafanya Azam iwe na wachezaji watano wa kigeni, wengine wakiwa ni Kipre Herman Tchetche na Kipre Michael Balou, ndugu wawili na pacha kutoka Ivory Coast na Mganda Brian Umony.

Azam chini ya kocha wake, Mcameroon Joseph Marius Omog imepanga kuboresha zaidi kikosi ili msimu ujao iweze kupata mafanikio zaidi katika Ligi ya Mabingwa Afrika na kutetea ubingwa wa Bara.

No comments:

Post a Comment