KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, May 18, 2014

MWANAMUZIKI AMINA NGALUMA 'JAPANESE GIRL' AFARIKI THAILAND



Aliyewahi kuwa mwanamuziki wa dansi wa bendi za African Revolution 'Wana tam tam' na Double M, enzi hizo chini ya uongozi wa Muumin Mwinjuma, Amina Ngalum A.K.A Japanese (pichani enzi za uhai wake) amefariki dunia nchini Thailand, ambako alikuwa akifanya shughuli zake za kimuziki.

Akizungumza na mtandao huu, mtoaji wa habari hizi, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wake katika bendi ya Tam Tam, Asha Baraka, amesema kuwa Amina amefariki dunia wakati akifanyiwa upasuaji.

''Imeelezwa kuwa Amina alianza kuugua ghafla, huku akilalamika kuwa kichwa kinamuuna na tumbo, na ndipo alipokwenda hospitali kwa ajili ya kupima na kuambiwa kuwa alikuwa na uvimbe kichwani na hivyo kutakiwa kufanyiwa upasuaji,"alisema.

Aidha ilielezwa kuwa uvimbe huo ulikuwa ukitoa damu na baada ya kuanza kufanyiwa upasuaji hakuweza kuamka tena na ndipo umauti ulipomfika'.

Mpaka mauti yanamfika, Amina alikuwa mwanamuziki wa bendi ya Jambo Survivors. Msiba upo Kipunguni B, Machimbo jijini Dar es Salaam.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU AMINA MAHALI PEMA. AMEN.

No comments:

Post a Comment