KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, August 5, 2015

TWIGA STARS KUWEKA KAMBI ZANZIBAR KESHO



Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) inatarajiwa kuingia kambini kesho kisiwani Zanzibar kujiandaa na Fainali za Michezo ya Afrika (All Africa Games) zitakazofayika mwezi Septemba mwaka huu nchini Congo Brazzavile.

Kikosi hicho cha wachezaji 25 chini ya Kocha Mkuu Rogasian Kaijage, tayari kimeanza mazoezi kujiandaa na michuano hiyo ambapo Tanzania ilikata tiketi ya kushiriki fainali hizo baada ya kuiondoa Zambia kwa jumla ya mabao 6-5.

Twiga Stars inaingia kambini  kwa gharama za TFF, huku jitihada za TFF kuwasiliana na Kamati ya Olimpiki nchini (TOC) zikiendelea kuona ni jinsi gani kamati hiyo inaihudumia timu hiyo ya Taifa kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ya Michezo Afrika.

TFF inatambua TOC ndio wana jukumu la kuhudumia timu za Taifa kuelekea kwenye michuano hiyo ya Michezo ya Afrika ikiwemo Twiga Stars.

Twiga Stars ambayo imefuzu kwa Fainali za Michezo ya Afrika itakayoanza kutimua vumbi Septemba 04 – 17 imepangwa kundi A na wenyeji Congo Brazaville na Nigeria pamoja na Ivory Coast.

No comments:

Post a Comment