KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 7, 2012

WEMA ATUMIA MIL 29/- KUTENGENEZA FILAMU







MSANII nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amesema ametumia zaidi ya sh. milioni 29 kwa ajili ya kuandaa na kukamilisha filamu yake mpya inayojulikana kwa jina la Super Star.
Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Wema alisema filamu hiyo imewashirikisha wasanii mbalimbali nyota nchini, wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
Aliwataja baadhi ya wasanii hao kuwa ni Hemed Mlela, Barnaba, Khaleed Mohamed (TID), Mr. Blue, Judith Wambura (Lady JayDee) na Jacob Steven (JB).
Kwa mujibu wa Wema, hii ni filamu yake ya kwanza baada ya kuamua kuwa mtayarishaji na muongozaji wa filamu.
Alisema amelazimika kutumia kiasi kikubwa cha pesa kutengeneza filamu hiyo kutokana na kuwashirikisha wasanii wengi nyota na pia kutumia maeneo mengi ya bei mbaya.
“Unajua hadi sasa nimeshacheza movi nyingi sana, nikaona kwa nini na mimi nisianze kutengeneza filamu zangu mwenyewe. Niliona kama wengine wameweza, kwa nini mimi nisiweze,”alisema Wema, ambaye aliwahi kuwa mrembo wa Tanzania wa mwaka 2006.
Katika filamu hiyo, awali Wema ameigiza kama mwanamke wa hali duni kimaisha, anayeishi kijijini. Akiwa huko, anashawishiana na rafiki yake na kuamua kwenda mjini kutafuta maisha.
Wakiwa mjini, rafiki yake ndiye anayeanza kufanikiwa kimaisha na kujiita Super Star. Kila Wema anapomuomba msaada rafiki yake huyo, anamtolea nje.
Hatimaye, Wema naye anafanikiwa kimaisha na kuwa msanii maarufu, kiasi kwamba kila anapokwenda, anafuatwa na lundo la waandishi wa habari.
Kutokana na kufanikiwa huko kimaisha, Wema anaamua kumshiti mpenzi wake, Hemed aliyemsaidia wakati anatoka kijijini kwao. Naye akaanza kujiona ni Super Star.
Je, ni kwa nini Wema amekuwa akitawala vyombo mbalimbali vya habari kila kukicha?
Akijibu swali hilo, Wema alisema nyota yake inang’ara ndio sababu kila anachokifanya ama kukisema, kimekuwa kikipewa uzito na vyombo vya habari.
“Sifanyi yote hayo kwa makusudi, hapana. Kwamba kila nikiingia sehemu nataka nionekane, hakuna kitu kama hicho na wala sipendi,”alisema Wema.
“Mimi huwa sipendi drama. Vyote hivyo vinatokea kwa malengo maalumu. Bila ya vyombo vya habari, nisingeweza kufahamika kiasi hiki,” aliongeza.
“Tatizo ni kwamba kila ninapokwenda ama kila ninachokifanya, kuna watu wananifuatilia,”alisisitiza na kuongeza kuwa, watu wengi wamekuwa wakimtafsiri tofauti na alivyo.
Akizungumzia maisha yake binafsi, Wema alisema anakipenda sana chumba anacholala na kitandani kwake, yupo mdoli, ambaye amemuelezea kuwa ndiye rafiki yake mkubwa. Mbali na kukipenda chumba chake cha kulala, Wema alisema nyumbani kwake anazo nywele bandia za kila aina, jozi kibao za viatu na vipodozi vya kila aina.
Mwanadada huyo mwenye sura na umbo lenye mvuto pia alisema anapenda sana kupika na ni hodari wa kupika vyakula vya aina mbalimbali.
Hivi karibuni, Wema alivikwa pete ya uchumba na mwanamuziki wa bendi ya Machozi, Mwinyi wakati wa onyesho lililofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya Maisha.
Tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi, hasa ikizingatiwa kuwa hii ni mara ya pili kwa Wema kuvikwa pete ya uchumba. Awali, alivikwa pete kama hivyo na msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’, lakini uchumba huo ulikufa katika mazingira ya kutatanisha.
Wema alizaliwa Septemba 28, 1988. Alianza kuwa maarufu mwaka 2006 baada ya kutwaa taji la mrembo wa Tanzania na kuiwakilisha nchi katika shindano la dunia.
Wema ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne wa Mzee Abraham Sepetu. Alianza elimu ya msingi hadi sekondari katika shule moja tu iitwayo 'Academic International' iliyopo maeneo ya Mikocheni, Dar es Salaam.
Kipaji zaidi cha Wema kiligundulika katika sanaa ya filamu, ambapo alifanikiwa kucheza vema katika filamu ya A Point of No Return akishirikiana na mchezaji filamu maarufu wa Kitanzania, marehemu Steven Kanumba.
Mwanadada huyo amekuwa akihusishwa kimapenzi na wasanii mbalimbali maarufu nchini, wakiwemo Mr.Blue, Charlz Baba, Kanumba, James Fredrick na Diamond.

Tuesday, June 5, 2012

KIGOGO WIZARA YA NISHATI AWANIA UONGOZI YANGA

KATIBU wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakhim Masu leo asubuhi amechukua fomu ya kugombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.

Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili amewataja wengine waliochukua fomu leo ni Mussa Katabaro, Muzamil Katunzi, Lameck Nyambaya, Edgar Fongo, Ahmad Waziri Gao na Yona Kevela.

Mapema jana, vigogo wengine watatu walichukua fomu za kugombea nafasi tofauti, hivyo kufanya uchaguzi wa Yanga utakaofanyika Julai 15, mwaka huu uzidi kuwa na msisimko.

Waliochukua jana ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Muhingo Rweyemamu, milionea Abdallah Ahmed Bin Kleb na kigogo wa zamani wa Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, Isaac Chanji.

Lakini kuna uvumi kwamba na milionea Yussuf Manji amechukua fomu ya kuwania Uenyekiti, ingawa Katibu Mkuu wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Francis Kaswahili anaendelea kukataa kwamba amechukua.

Idadi ya waliochukua fomu hadi sasa inafika watu 11, baada ya awali Ayoub Nyenzi kuchukua fomu ya kugombea Makamu Mwenyekiti, Jumanne Mwamenywa, John Jambele, Peter Haule, Gaudicius Ishengoma, Abdallah Sharia na Saleh Abdallah, wote Ujumbe.

Uchaguzi wa Yanga unaokuja baada ya Wajumbe wengi wa Kamati ya Utendaji iliyoingia madarakani mwaka juzi, kujiuzulu akiwemo Mwenyekiti, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga na mwisho wa zoezi la kuchukua ni kesho, wakati kurudisha ni kesho saa 10:00 jioni na usaili ni Juni 19, mwaka huu.

Kaswahili amesema kesho ikifika saa 10:01 hatapokea fomu wala kutoa fomu, kwani saa 10:00 ndio mwisho wa kurudisha fomu kwa wagombea wote.

Monday, June 4, 2012

Bongo Star Search kuanza ziara kusaka vipaji mikoani

ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star
Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika ukumbi wa Royal
Village.
Akizungumzia ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark
Production, Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika
ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.
Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano
kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia
Dar es salaam.
Alisema kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa
kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa
kuimba aina zote za nyimbo.
“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata
kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa
mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo,” alisema Ritha.

Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na Master Jay.

Huduma ya Airtel Supa 5 yazinduliwa kwa kishindo morogoro

Msanii wa kundi maarufu nchini la Tip Top Connection lenye makazi yake
Manzese, Dar es Salaam, Madee akiimba jukwaani kuburudisha umati wa
wakazi wa morogoro waliofurika uwanja wa shule ya msingi uwanja wa ndege
kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa
huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel. Huduma hiyo
itatambulishwa hivi karibuni katika mkoa wa Iringa, Arusha na Mwanza.

Sehemu ya umati wa wakazi wa morogoro uliofurika kwenye uwanja wa shule
ya msingi uwanja wa ndege kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel
Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano
kupitia Airtel. Huduma hiyo itatambulishwa hivi karibuni katika mkoa wa
Iringa, Arusha na Mwanza.



Mkazi wa Morogoro, Sarafina Millak akikabidhiwa simu aina ya sumsung na
Meneja Mauzo wa Airtel kanda ya Pwani, Aminata Keita mara baada ya kuibuka
kinara wa kucheza ‘sebene’ la bendi ya Mashujaa wakati wa uzinduzi wa
huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 iliyofanyika jana kwenye uwanja wa
shule ya msingi-Uwanja wa ndege mkoani Morogoro. Airtel Jiunge na Supa 5
Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Ukitaka
kujiunga na huduma hiyo ANDIKA SMS YENYE NENO ‘WIKI’ AU WIKI
UTUME KWENDA 15548.


Wateja wa Airtel wakiwa na zawadi zao za simu aina ya Sumsung mara baada
kununua moderm za Airtel zenye kasi ya 3.75G,shoto ni Meneja Mauzo wa
kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Morogoro,Aluta Kweka.


Msanii wa hip hop Roma akighani jukwaani kuburudisha umati wa wakazi wa
morogoro waliofurika uwanja wa shule ya msingi uwanja wa ndege
kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa
huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel.huduma hiyo
itatambulishwa hivi karibuni katika mkoa wa Iringa, Arusha na Mwanza



Wanamuziki wa bendi ya Mashujaa wakilishambulia jukwaa kuburudisha umati wa
wakazi wa morogoro waliofurika uwanja wa shule ya msingi uwanja wa ndege
kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa
huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel. Huduma hiyo
itatambulishwa hivi karibuni katika mkoa wa Iringa, Arusha na Mwanza.

HIZI NDIZO JEZI MPYA ZA AZAM FC

Jezi mpya za Azam FC, ambazo zipo katika mchakato wa kutengenezwa, zimekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kama facebook, twitter na Blogs mbalimbali nchini.
Mashabiki wengi wa soka wameonekana kuvutiwa na jezi mpya huku wasambazaji wa bidhaa za nguo na baadhi ya maduka wakiomba muongozo wa namna ya kuzipata.
Kimsingi jezi hizi zipo katika mchakato wa kutengenezwa, kwa sasa tunasubiri sampo kutoka China na baada ya hapo tukiridhika nazo ndipo tutatoa oda na inaweza kuchukua hadi miezi miwili kwa jezi kuwa tayari, kwa hiyo mashabiki wasitarajie kwamba zitatoka mapema, amesema katibu mkuu wa Azam FC Nassor Idrissa
Azam FC imejijengea heshima kwa kuwa inatoa toleo jipya la jezi kila msimu, huu ukiwa ni msimu wake wa tatu, ambapo msimu uliopiza jezi hizo zilidhaminiwa na Azam Cola na msimu huu itakuwa Azam Energy Drink.

Stars yajipanga kuikabili Gambia J'pili

Mshambuliaji wa timu ya Kilimanjaro Taifa Stars, Mrisho Ngassa akimtoka beki wa Ivory Coast, Siaka Tiene wakati wa mechi ya kusaka kufuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny, mjini Abidjan juzi ambapo Stars ilifungwa mabao 2-0.



Kikosi cha Taifa Stars ambacho juzi kilicheza na Ivory Coast mjini Abidjan na kupoteza kwa mabao 2-0, kinaendelea kujinoa kwa mechi ijayo dhidi ya Gambia itakayochezwa Jumapili (Juni 10 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa programu ya Kocha Kim Poulsen, Taifa Stars ilifanya mazoezi jana asubuhi kwenye uwanja wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ivory Coast (FIF), ambao uko pembezoni mwa jiji la Abidjan.

Timu hiyo itafanya tena mazoezi leo (Juni 4 mwaka huu) asubuhi kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani saa 1.30 usiku kwa ndege ya Kenya Airways kupitia Nairobi, ambapo itawasili Dar es Salaam, Juni 5 mwaka huu saa 1.40 asubuhi.

Kocha Kim, ambaye amekuja na wachezaji wote hapa ukiondoa wanne ambao ni majeruhi (Thomas Ulimwengu, Nurdin Bakari, Haruna Moshi na Nassoro Masoud Cholo) amesema hivi sasa wameelekeza akili yao kwenye mechi ijayo dhidi ya Gambia.

“Safari ya kujenga timu ndiyo imeanza. Mechi dhidi ya Ivory Coast imepita na ninawashukuru wachezaji kwa kucheza kwa mujibu wa maelekezo na kujituma. Mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa yaliyosababisha tuwape Ivory Coast mabao mepesi.

“Lakini kama nilivyosema mechi hiyo imepita, hivi sasa tunaangalia mechi ijayo dhidi ya Gambia. Hatuna muda mwingine wa kujipanga na ndio maana niliamua kuja na wachezaji wote Abidjan,” amesema Kim.

Mechi dhidi ya Gambia itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni. Gambia ilitoka sare ya bao 1-1 na Morocco katika mechi iliyochezwa juzi jijini Banjul.
Hata hivyo, Taifa Stars haitakuwa na nahodha wake msaidizi Aggrey Morris, ambaye alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 65 baada ya kupata ya pili ya njano kwenye mechi dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan.

Sudan Kusini yapata mwakilishi Miss East Africa 2012

Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Sothern Sudan katika mashindano ya Miss East Africa 2012 amepatikana. Mrembo huyo ni Akuot Philip Suzan (20) mwenye urefu wa futi 6.1 anaekaa Juba, Sudan na ni mwanamitindo nchini humo na anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha makelele Nchini Uganda mwaka huu.

Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika nchi mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritreani Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni Lula Teklehaimanot (19) na Ayisha Nagudi (23) ambaye ni mwakilishi wa Uganda.

Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012, ambayo yatazishirikisha nchi 16 za ukanda huu, ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.

Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Afrika. Fainali za mashindano ya Miss East Africa, ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania.

Twanga Pepeta yapata viongozi wapya

UONGOZI wa Kampuni ya African Stars Entertainment (ASET) imefanya mabadiliko kadhaa ya uongozi katika bendi yake ya Twanga Pepeta International. Mabadiliko hayo yalitangazwa jana na Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka alipokutana na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Dar es Salaam.

Katika mabadiliko hayo, Asha alimtangaza Muddy Pizzaro kuwa ndiye msemaji mpya wa bendi, Muddy K anakuwa meneja matukio wakati Omary Baraka anaendelea kuwa mkurugenzi mtendaji.

Katika mabadiliko hayo, Amigolas anakuwa meneja wa bendi, Luiza Mbutu anaendelea kuwa kiongozi wa bendi akisaidiwa na Saleh Kupaza.

Kiongozi wa wanenguaji anaendelea kuwa Maria Salome kwa wanawake na kwa wanaume anaendelea kuwa Sidy Boy.

Sunday, June 3, 2012

AZAM YAANIKA SILAHA ZAKE ZA MSIMU WA 2012/2013

Kikosi kamili cha Azam FC kwa ajili ya msimu ujao wa ligi wa 2012/2013 ni kama ifuatavyo:

Magolikipa ni Mwadini Ally, Deo Munishi 'Dida' Aishi Salum na Jackson Wandwi.

Mabeki wa pembeni kulia ni Ibrahim Shikanda na Erasto Nyoni na kushoto ni
Waziri Salum na Samih Haji Nuhu.

Mabeki wa kati ni Luckson Kakolaki, Said Moradi, Joseph Owino na Aggrey
Morris.

Viungo ni Kipre Bolou, Abdulhalim Humud, Himid Mao, Salum Abubakar,
Abdi Kassim Sadala, Ramadhani Selemani Chombo, Abdulghani Ghulam,
Ibrahim Rajab Jeba, Jabir Aziz Stima na Ibrahim Joel Mwaipopo.

Washambuliaji wa pembeni ni Kipre Tchetche, Mrisho Ngasa, Zahoro Pazi,
Khamis Mcha na George Odhiambo 'Blackberry'.

Washambuliaji wa kati ni Gaudence Mwaikimba na mchezaji bora wa Azam FC,

John Raphael Bocco
"Adebayor"

FLOYD MAYWEATHER AANZA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIEZI MITATU

Bondia Floyd Mayweather leo ameanza kifungo cha miezi 3 jela
alichohukumiwa mwezi Desemba mwaka jana kutokana na kuvunja sheria kwa
kufanya ugomvi. Wakati akielekea Jela Mayweather alisindikizwa na rafiki yake
kipenzi mwanamuziki 50 Cent.


Mayweather akitiwa pingu na polisi kuelekea kwenye karandinga.

"Nenda dogo nitakumiss kaka yako" 50 Cent na Mayweather.

Hiki ndio chumba atakachokaa Mayweather kwa miezi 3

Hizi ndio sare zake kwa kipindi chote atakachokaa jela.

Buya atwaa taji la Miss Manyara 2012

Mshindi wa taji la Redds Miss Manyara 2012, Buya Ernesi (katikati) akiwa na mshindi wa pili Dalina Sikawa (kushoto) na mshindi wa tatu, Lucy Stephano mara baada ya kutangazwa kwa matokeo ya mshindi wa taji hilo usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa CCM mjini
Babati.

Lightness ndiye Miss Dodoma 2012

Mshindi wa taji la Redd's Miss Dodoma 2012, Lightness Michael (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili, Berinda Mdogo (kulia) na
mshindi wa tatu Nulsa Magambo mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo

usiku wa kuamkia leo.

Taifa Stars yachapwa 2-0 na Ivory Coast

Mshambuliaji Didier Drogba wa Ivory Coast akijiandaa kutuliza mpira huku akiwa amezongwa na beki Kevin Yondan wa Taifa Stars.

Mshambuliaji Mbwana Samatta wa Taifa Stars akiruka hewani kupiga mpira kwa kichwa sambamba na beki wa Ivory Coast.

Moja ya kosa kosa zilizotokea kwenye lango la Ivory Coast wakati timu hiyo ilipomenyana na Taifa Stars jana.

Shaaban Nditi (kushoto) wa Taifa Stars akijaribu kumshibiti Solomon Kalou wa Ivory Coast.

TIMU ya soka ya Taifa,Taifa Stars jana ilipigwa mweleka wa mabao 2-0 na Ivory Coast katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za 2014.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny mjini Abidjan, Ivory Coast ilijipatia mabao hayo mawili, moja katika kila kipindi.

Bao la kwanza lilifungwa na Salomon Kalou katika kipindi cha kwanza kabla ya Didier Drogba kuongeza la pili katika kipindi cha pili.

Taifa Stars ililazimika kumaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 baada ya beki wake, Aggrey Morris kutolewa nje kwa kadi nyekundu na mwamuzi Slim Jedidi kutoka Tunisia kwa kosa la kucheza rafu mbaya.

Katika mechi hiyo, Kocha Kim Poulsen wa Taifa Stars alilazimika kufanya mabadiliko ya wachezaji wawili kutoka katika kikosi alichokichezesha katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Malawi iliyochezwa Mei 26 mwaka huu.

Kim aliamua kumchezesha Amir Maftah katika nafasi ya beki wa kushoto badala ya Waziri Salum na pia alimchezesha Mrisho Ngasa katika nafasi ya mshambuliaji wa kati badala ya Haruna Moshi, ambaye hakwenda Ivory Coast kutokana na kuwa majeruhi.

Friday, June 1, 2012

Taifa Stars ikiwa mazoezini Abidjan



Wachezaji wa timu ya Soka ya Taifa, Taifa Stars wakijifua kwenye Uwanja wa kituo cha michezo mjini Abidjan juzi kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast inayotarajiwa kufayika kesho kwenye uwanja wa Felix Houphouet-Boigny.(Picha kwa hisani ya Bongostaz)

Mrembo wa Nyamagana kupatikana leo

Cecy

Brenda

Amina

Aisha

Shindano la kumsaka mrembo wa kitongoji cha Nyamagana, atakayeshiriki katika shindano la kumsaka mrembo wa Mwanza anatarajiwa kujulikana leo usiku.

Shindano hilo linalotarajiwa kuwashirikisha warembo kadhaa wa kitongoji hicho, limepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Gold Crest.

Shindano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Stoppers Entertainment ya Mwanza na kutakuwepo na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, akiwemo Linah na Hafsa Kazinja.

Mshereheshaji mkuu wa shindano hilo atakuwa msanii maarufu wa kundi la Orijino Komedi, Emmanuel Mgaya almaarufu zaidi kwa jina la Masanja Mkandamizaji.

Nelly Kamwelu kuchangia harambee ya saratani ya matiti

MREMBO anayeshikilia taji la Miss Universe Tanzania 2011/2012 Nelly Kamwelu kwa kushirikiana na Mfuko wa Saratani ya Matiti Tanzania (Breast Cancer Foundation) leo atafanya harambee ya kuchangia mfuko wa saratani ya matiti itakayofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Harambee hiyo imepangwa kuanza saa 1.00 usiku kwa mujibu wa muandaaji wa mashindano ya Miss Universe Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Compass Commutations, Maria Sarungi Tsehai.

Maria alisema kuwa katika hafla hiyo kutakuwa na mnada wa kito cha Tanzanite ambayo imetolewa maalum na kampuni ya Richland Resources kwa ajili ya kuchangia mfuko huu. Pia picha ya Mrembo wa Miss Universe Tanzania itanadiwa katika mnada huo.

Mrembo Nelly Kamwelu toka achukue taji la Miss Universe Tanzania 2011, amekuwa akifanya kazi bega kwa bega na mfuko wa saratani ya matiti ikiwamo kusaidia kutoa elimu katika shule mbalimbali ili kupunguza au kutokomeza uwezekano wa kuenea kwa saratani ya matiti.

Mfuko huu umepanga kuendeleza elimu hii kwa shule za mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Rukwa, Iringa, Mtwara na Lindi.

Kwa kusindikiza hafla hii kutakuwa na maonyesho ya mavazi yaliyotolewa na wabunifu wa hapahapa nchini ambao ni Escado Bird, Kemi Kalikawe na Subira Wahure vilevile kutakuwa na burudani ya muziki kutoka msanii Enika na mchekeshaji Evans Bukuku. Pia mrembo mwenyewe Nelly Kamwelu atatoa burudani ya dansi aina ya Belly Dance.

Mabondia wa Tanzania wapandishwa viwango

Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi cha Marekani (IBF/USBA) limewaweka mabondia wa Tanzania katika orodha ya viwango .
Mabondia hawa ambao watakuwa miongoni mwa mabondia 15 bora duniani katika uzito wao ni: Francis Miyeyusho, Fadhili Ramadhani, Mbwana Matumla, Seba Temba, Allan Kamote, Pascal Bruno na Francis Cheka.

Katika kikao cha Kamati ya Viwango (Ratings Committee) ambacho kilikaa jana chini ya Uenyekiti wa William James, IBF/USBA iliridhishwa na viwango vya mabandia wa Kitanzania na kutoa ahadi kuwa watawaangalia kwa karibu zaidi katika kipindi cha mwaka mmoja ujao ili kuwaongeza katika orodha ya viwango.

Hii ina maana kuwa mabondia hao waliowekwa kwenye orodha ya viwango vya IBF vya mabara wanaweza kupigania ubingwa wa IBF wa Afrika na mabara wakati wowote. Afrika, Mashariki ya Kati ya Ghuba ya Uajemi iliwakilishwa kwenye kikao hicho na Rais wake Onesmo Ngowi toka Tanzania.

Katika vikao hivi vya viwango ni Marais wa mabara na viongozi wakuu wa IBF wanaohudhuria peke yao. Ngowi aliwapendekeza pia mabondia kadhaa wa Kenya, Uganda, DRC, Afrika ya Kusini, Namibia, Zimbabwe, Mali, Gabon, Benin, Bukina Faso, Ghana, Nigeria, Morocco, Cameroon, Ivory Cost, Tunisia, Misri, Dubai na Jordan.

Kumekuwepo na uchakachuaji mkubwa wa rekodi za mabondia katika bara la Afrika kwa mapromota na mawakala wa ngumi kuweka viwango vya mapambano ya uongo katika rekodi za mabondia wao kweney mtandao wa Boxrec.

Hii inawapa wakati mgumi sana mabondia wa Kiafrika kupata mapambano ya ngumi ya kimataifa. Afrika, Mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi inaongozwa na rais wake Onesmo Ngowi wa Tanzania.

Mrembo wa Mtwara kupatikana kesho

HAWA ni warembo watakaopanda jukwani kesho kuwania taji la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Mtwara katika shindano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Makonde Beach.

Hasheem Thabeet aahidi kujenga uwanja wa kisasa wa kikapu


Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Lord Baden Powell, Kanali Idd Kipingu akizungumza machache mbele ya wageni wake waliofika mapema leo shuleni hapo kwa ajili ya kuangalia namna ya kujenga uwanja wa mchezo wa mpira wa kikapu.

Mchezaji wa Kimataifa wa Tanzania, anayechezea timu ya Portland Trail Blazers ya Marekani kwenye Ligi ya NBA, Hasheem Thabeet akizungumza jambo mbele ya wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lord Baden Powell Memorial High School,wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kiwanja cha mpira wa kikapu shuleni hapo mapema leo Bagamoyo,nje kidogo ya jiji la Dar,kulia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania, Phares Magesa.Hasheem Thabeet ameahidi kuwajengea uwanja wa mpira wa kikapu shuleni hapo.

US Embassy in Dar Es Salaam today hosted Hasheem Thabeet and TBF Vice President Phares Magesa who was accompanied by TBF Assistant Secretary General Michael Maluwe, TBF Treasurer Ms. Marry Mbaga.
The US Embassy thanked Hasheem for agreeing to conduct basketball clinics in Tanzania. During the event US Embassy in Dar donated 50 balls to be used at Under 17 basketball Clinic to be held in Arusha June 9-10, 2012.
Cultural Affairs Officer and first Secretary of the US Embassy in Dar Es Salaam Ms. Danna Banks handed over the balls to TBF Vice President Phares Magesa in the presence of NBA Player Hasheem Thabeet, Portland Trail Blazer Centre.
Also the US state department through US Embassy in Dar es Salaam has given a grant to support administrative cost of running the Arusha Clinic, the grant was signed today by Mr. Magesa and Ms. Banks at the Embassy.
The Arusha Clinic will be conducted by one of the very best US based coach details will be released later. After the event at the Embassy Hasheem and Mr. Magesa went to Lord Barden Powell High School in Bagamoyo.
Hasheem promised to support various school projects including building of modern basketball court for the school. On behalf of TBF we than Hasheem for this great initiative.Hasheem will tomorrow start his clinic for 200 kids from 6 regions to be held at Don Bosco grounds.
We call upon other organizations to join us in developing our youth through various programmes like youth clinics, basketball courts construction/refurbishment etc.
Thank you,
Phares Magesa

TBF Vice President.

Taifa Stars yatua salama Ivory Coast, Kim asema mechi itakuwa ngumu

Kikosi cha Taifa Stars kimewasili hapa Abidjan (Mei 31 mwaka huu) mchana huku Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen akisema mechi dhidi ya Ivory Coast itakuwa ngumu.

Stars yenye wachezaji 21 ilikuwa iwasili hapa asubuhi, lakini ndege iliyobadilisha Nairobi ilichelewa kuondoka kwa saa tatu.

Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Taifa Stars na wenyeji Ivory Coast (Tembo) itachezwa Juni 2 mwaka huu Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny kuanzia saa 11 kamili jioni ambapo Tanzania itakuwa saa 2 kamili usiku.

Licha ya kwanza, Stars ililazimika kuacha wachezaji wawili dakika za mwisho (Haruna Moshi na Nassoro Cholo), Kim amesema kikosi chake ambacho kimefikia hoteli ya Ibis bado kimejipanga vizuri kwa ajili ya mechi hiyo.

“Tunaiheshimu Ivory Coast kwa vile ni timu ambayo inaundwa na baadhi ya wachezaji nyota wa dunia kama akina Drogba (Didier) na Yaya (Toure), lakini wajiandaa kupata wakati mgumu kutoka kwetu,” amesema Kim ambayo kikosi chake baada ya kuwasili hapa kilipata fursa ya kufanya mazoezi jioni.

Kikosi cha Stars kinaongozwa na nahodha wake Juma Kaseja akisaidiwa na Aggrey Morris. Wachezaji wengine waliopo hapa na kikosi hicho ni Mwadini Ally, Deogratius Munishi, Amir Maftah, Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Waziri Salum, Shomari Kapombe na Juma Nyoso. Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Salum Abubakar, Shabani Nditi, Edward Christopher, Mrisho Ngasa, Frank Domayo, Mbwana Samata, Ramadhan Singano, Simon Msuva na John Bocco.

Mbali ya Kim, Benchi la Ufundi lina Sylvester Marsh (Kocha Msaidizi), Juma Pondamali (Kocha wa makipa), Leopold Mukebezi (Meneja wa timu), Juma Mwankemwa (Daktari wa timu), Frank Mhonda (Physiotherapist) na Alfred Chimela (Mtunza vifaa).

Msafara wa Stars hapa unaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Crescentius Magori lakini pia yupoMwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dioniz Malinzi ambaye amekuja kushuhudia mechi hiyo.