KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 6, 2016

YUSUF MANJI, SANGA WAKOSA WAPINZANI UCHAGUZI MKUU YANGA

WANACHAMA 19  wa klabu ya Yanga, wamechukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga, Sam Mapande, alisema mjini Dar es Salaam, jana, kuwa, wanachama wawili wameondolewa kutokana na fomu zao kuwa na dosari.

Mapande alisema kamati hiyo ilikutana juzi kwa ajili ya kupitia majina yote ya wanachama walioomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi, ambapo majina mawili ndiyo yaliyoonekana kuwa na dosari.

Aliwataja wanachama, ambao majina yao yameondolewa kutokana na fomu zao kuwa na dosari kuwa ni Yusuf Mhandeni na Leonard Marango, waliokuwa wakiwania ujumbe wa kamati ya utendaji.

Uchaguzi mkuu wa Yanga, umepangwa kufanyika Juni 11, mwaka huu na nafasi zinazogombewa ni ya mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Kwa mujibu wa Mapande, uchaguzi huo utafanyika kwa kutumia kadi za zamani za klabu hiyo na katiba inayotambuliwa na serikali.

Mapande alisema usaili kwa ajili ya wanachama hao 19 waliochukua fomu za kuwania uongozi, ulitarajiwa kufanyika jana jioni.

Wagombea waliochukua fomu za kuwania uongozi hadi jana, nafasi wanazowania zikiwa kwenye mabano ni Yusuf Manji (mwenyekiti), Clement Sanga (makamu mwenyekiti).

Wengine ni Samwel Lukumay, Salum Mkemy, Beda  Tindwa, David Ruhago, Lameck Nyambaya, Ayubu Nyenzi na George Manyama (wajumbe).

Wengine ni Sylvester Haule, Liza Lymo, Hosein David, Hashim Abdalah, Athumani Kihamia, Pascal Laizer, Godfrey Mheluko, Bakari Malima, Mchafu Chakoma na Thobias Lingalangala.

Awali, uchaguzi huo ilikuwa usimamiwe na Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), lakini baadaye iliamriwa usimamiwe na kamati ya uchaguzi ya Yanga.

No comments:

Post a Comment