KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 12, 2016

MANJI ASHINDA UENYEKITI WA YANGA KWA KISHINDO



WANACHAMA wa klabu ya Yanga, juzi walimchagua tena Yusuph Manji kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo baada ya kupata kura 1,468 kati ya 1,470.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam, Clement Sanga alichaguliwa tena kuwa makamu mwenyekiti baada ya kupata kura 1,428 kati ya 1,508.

Dalili za Manji kushinda uchaguzi huo zilionekana mapema kutokana na idadi kubwa ya wanachama kumuunga mkono. Hakukuwa na kura ya kumkataa wakati kura mbili ziliharibika. Manji hakuwa na mpinzani.

Nafasi ya makamu mwenyekiti ilikuwa na wagombea wawili, Sanmga na Titus Osoro, ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji kabla ya kuondolewa. Katika nafasi hiyo, Osoro aliambulia kura 80.

Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa kamati ya utendaji, idadi ya kura zikiwa kwenye mabano ni Siza Augustino Lymo (1027), Omary Said Amir (1069), Tobias Lingalangala (889), Salim Mkemi (894), Ayoub Nyenzi (889), Samuel Lucumay (818), Hashim Abdallah (727),Hussein Nyika (770).

Wajumbe 12 ambao kura zao hazikutosha katika kuwania nafasi hiyo ni David Luhago (582), Godfrey Mheluka (430), Ramadhani Kampira (182), Edgar Chibura (72), Mchafu Chakoma (69), George Manyama (249), Bakari Malima 'Jembe Ulaya' (577), Lameck Nyambaya (655), Beda Tindwa (452), Athumani Kihamia (558), Pascal Lizer (178)
na Silvester Haule (197).

No comments:

Post a Comment