KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, June 1, 2016

WAGABON KUZICHEZESHA STARS NA MISRI


Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri utakaofanyika Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.

Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.

Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.

Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE

Timu ya soka Taifa ya Wanawake ya Tanzania – Twiga Stars, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Rwanda, utakaofanyika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda.

Rwanda wameomba mchezo ufanyike ili kukiimarisha kikosi chao sambamba na kuboresha uhusiano wa nchi ambazo zote ni nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

No comments:

Post a Comment